Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyompa silaha muuaji wa Lemax Bar iwajibike

Nakumbuka early 2003/4 kati ya hiyo miaka miwili mjomba'angu (sasa marehemu) baada ya ukwasi kuwa mwingi aliona ajiongezee ulinzi aka-apply naye amiliki silaha njia zote alifanikiwa ila police post ya pale mtaani (Mabibo kipindi hiko) alikuwa na kesi ya kumpiga mkewe na stuli habari yake ikaishia hapo.

Mpaka anafariki hakuwahi kupewa kibali, ni kusema baadhi ya watu kwenye system kukosa maadili ndo kunachangia. Kuna siku tena pale Kariakoo jamaa na ki-IST chake kaguswa kidogo kwenye bumper la nyuma na bus Eicher kashuka na chuma hata dereva wa daladala yenyewe hajasema neno yeye ana mkwaju mkononi kilichosaidia kulikuwa na police karibu wakaja wakaondoka naye.
 
Ni vigumu sana wanaotoa vibali vya silaha kujua mtu akishapata silaha ataitumia namna gani. Kama huyu jamaa alikuwa hana rekodi yoyote mbaya hiyo kamati unailaumu bure. Wa kulaumiwa ni 1. Watu walio karibu naye. Walitakiwa watoe ripoti polisi hata kwa kificho kuhusu tabia yake baada ya kumiliki silaha. 2. Mwenye Bar/wahusika wa bar aliyokuwa anakunywa. Huyu ndiye anabeba lawama kubwa zaidi kwa sababu alitakiwa aite polisi baada ya jamaa kuanza mawenge
 
Lawama zinarudi kwa watoa vibali na watu wa karibu na muuaji....Ukiskia ndugu yako anataka kumiliki silaha ogopa sana hiyo kitu... maana silaha ya moto kiukweli haina chaguo...mwenye silaha ya moto yoyote yule tayari anakuwa ameshaweka dhamira ya kuua.
 
Anaonekana alikua na vitu vyake kichwani kibao na alikua na lengo la kujiua muda mrefu alikua anatafuta sababu tu na alishajitabiria kuwa bastola ndio itakayomuua..kamuua mshikaji mwingine bila sababu ya msingi...
 
Kuna mmoja Sinza bar ya Dolphin anaitwa Wambura kuna siku miaka kadhaa nyuma alileta taharuki na bastola yake. Alimchapa mshkaji ya mkono.
Kweli Mkuu ilikuwa mida ya jioni tulikuwa tunaangalia mpira, jamaa wakapishana kauli dah jamaa akawekaa, ikamchana mkono, Wambura mkorofi namjua sana, anapenda kutembea na silaha hiyo kiunoni yaani ni mshamba, wakati watu waelewa
tunaziacha kwenye magari..
 
Angenyoosha mkono angepata kibali, miaka ya nyuma huko 2000s kuna mtu alikuwa anakaa Kibamba akaombea kibali Tabata ambako hajawahi hata kukaa akapata kibali
 
Duh noma mkuu kumbe nawe ulikuwepo ile siku 😂😂😂. Sinza na Chuga huu ujinga upo sana. Ni mambo ya kikolo sana.
 
Hapa Kuna masuala ya kula papuchi ya mwenzake , sio Bure
 
Kamati ya wapi hii yenye utaratibu rahisi hivi? Guys yeyote mwenye silaha Hata kama ni RPC na yupo na influence of alcohol kaa mbali. Pia
askari yeyote Anaelewa mazingira hatarishi, na wengi hujua mida gani Si ya masihara . Haya mengine mengi huku vijiweni ni kuchangamsha genge
 
Poor vetting...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…