University of Dodoma (UDOM)
Public Institution
- Feb 24, 2024
- 50
- 55
Mradi wa SAFARI unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umefanya kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri wa Kiufundi (TAC) iliyoundwa kuimarisha utekelezaji wa Mradi huo wenye lengo la kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI) kuboresha huduma za ultrasound kwa kina mama wajawazito, hususan maeneo ya vijijini.
Pichani: Wajumbe wa kamati
Kikao hicho kimefanyika leo Jumanne Mei 12, 2026 katika ukumbi wa Hoteli ya Gerwill iliyopo jijini Dodoma, ikiwakutanisha wawakilishi kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo Wizara ya Afya, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo Mradi huu unatekelezwa, Wataalamu wa Mionzi, Elimu na Wataalamu wa Mifumo.
Mradi wa SAFARI unafadhiliwa na Gates Foundation kwa kushirikiana na Liverpool School of Tropical Medicine (LSTM), pamoja na Wizara ya Afya Tanzania. Lengo kuu la mradi huo ni kuongeza usahihi wa uchunguzi wa afya ya uzazi, kuboresha huduma za afya kwa wajawazito na watoto, pamoja na kupanua upatikanaji wa huduma bora za ultrasound nchini.
Pichani: Dkt. Leonard Katalambula Mratibu wa Mradi
Akizungumza wakati wa warsha hiyo, Mratibu wa Mradi huo kutoka UDOM, Dkt. Leonard Katalambula, amesema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma, kupitia vituo vya afya vya kati ya 40 vilivyoanishwa kigeografia.
Amesema matumizi ya teknolojia ya Akili Unde katika huduma za ultrasound yatasaidia kuongeza ubora wa uchunguzi wa afya ya uzazi, kupunguza changamoto za upatikanaji wa wataalamu wa afya maeneo ya vijijini na kupunguza vifo vya akina mama na watoto nchini.
“Mradi huu unalenga kuleta mageuzi katika utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha wanawake wajawazito wanapata huduma bora kwa wakati,” alisisitiza Dkt. Katalambula.
Kamati ya Ushauri wa Kiufundi (TAC) inayosimamia utekelezaji wa mradi inawakilisha sekta muhimu zinazohusiana na afya ya uzazi na mtoto, radiolojia, huduma za uchunguzi, utafiti, fedha, tiba na uuguzi kwa lengo la kuhakikisha usimamizi madhubuti na utekelezaji wenye tija wa mradi huo.
Kwa ujumla, kikao hicho kimeonyesha dhamira ya pamoja ya wadau wa sekta ya afya na elimu katika kutumia teknolojia ya kisasa kuimarisha huduma za afya ya uzazi nchini, huku Mradi wa SAFARI ukitajwa kuwa chachu ya maboresho makubwa ya huduma za uchunguzi kwa wajawazito, hasa katika maeneo yenye changamoto ya huduma za kibingwa.
Pichani: Wajumbe wa kamati wakiwa katika picha ya pamoja.