Kamau: Rais Magufuli adhibitiwe na EAC, amevuka mipaka!

Hakuna gazeti linalodharauliwa na Wakenya kama Taifa leo, nimefika huko mara nyingi, huwa nikinunua hilo Gazeti wananishangaa na kunicheka sana, hivyo hiyo siyo newsworthy kwa Mkenya.
Acha ujinga jikite kwenye mada, yaliyoelezwa yote ni kweli.Pinga hoja kwa hoja
 
Sijui kuhusu Msiba lkn Tanzania hakuna ,,classes” baina ya Wasomaji Magazeti kila mtu anaweza kununua Gazeti lolote na kusoma bila ya kujificha, Kenya ni tofauti, ukisoma Taifa leo unaonekana wewe ni mtu wa chini kabisa kwenye jamii ambaye haujui English language na hivyo wa kudharauliwa.
Vp hapa ukinunua la Musiba aka Tanzanite !!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na WANDERI KAMAU

MNAMO Novemba 5, 1984, kinara wa ODM Raila Odinga alifahamishwa kuhusu kifo cha mamake, Bi Mary Juma ikiwa imepita muda wa miezi miwili tangu afariki.

Mary alifariki mnamo Septemba 1984, lakini Bw Odinga hakuwa na ufahamu wowote kuhusu tukio hilo kwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Shimo la Tewa, jijini Mombasa.

Alikuwa na mfungwa mwenzake, Bw George Anyona alipopata habari hizo za kuhuzunisha.

Kwa jumla, ilikuwa vigumu kwa wafungwa kuwasiliana na jamaa zao wakati huo kutokana na ulinzi mkali waliowekewa na serikali ya Rais Mstaafu Daniel Moi.

Kwa mujibu wa simulizi nyingi za watu waliojipata kama wafungwa wa kisiasa katika utawala wa Mzee Jomo Kenyatta na Bw Moi, walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa kuandika kwenye shashi ndipo wasijulikane na serikali.

Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama.

Hali hiyo hiyo ndiyo imemkumba mwanahabari Eric Kabendera kutoka Tanzania, anayeendelea kuzuiliwa na serikali ya Rais John Magufuli, kwa tuhuma za kuandika habari za “uongo na kuwapotosha” wananchi.

Bw Kabendera amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, huku juhudi zake zote kuomba msamaha Rais Magufuli zikigonga mwamba.

Serikali pia imepuuzilia mbali rai za mawakili wake kumwachilia kwa dhamana ili kuendelea na kesi yake akiwa huru.

Majuma mawili kabla ya kifo chake, Bi Verdiana Mjwahuzi alikuwa amemwomba Rais Magufuli kumsamehe mwanawe, hasa baada ya Bw Kabendera kumwandikia barua akimwomba msamaha.

Licha ya juhudi hizo zote, Bw Magufuli alifumbia macho kilio hicho cha mama kwa niaba ya mwanawe.

Taswira hii bila shaka inaondoa dhana ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kwamba, Bw Magufuli ni “ufufuo na msisimko” wa aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Bw Julius Kabarage Nyerere.

Badala yake, ameibuka kuwa kiongozi wa kiimla anayeendesha taifa hilo kwa mfumo wa kidikteta.

Chini ya utawala wa Bw Magufuli, uhuru wa wanahabari umedidimia pakubwa, huku baadhi yao wakitoweka wasijulikane waliko.

Mfano dhahiri ni mwanahabari Azory Gwanda, aliyetoweka Novemba 2017 katika hali ya kutatanisha. Hadi sasa, haijulikani aliko mwanahabari huyo.

Kando na wanahabari, Tanzania pia imekuwa ikiwahangaisha viongozi wa upinzani, mmoja wao akiwa aliyekuwa mbunge wa Singinda Mashariki, Bw Tundu Lissu.

Mnamo Oktoba 2017 gari la Bw Lissu lilimiminiwa risasi zaidi ya 30 baada ya kuondoka kwenye kikao cha Bunge jijini Dodoma.

Bw Lissu, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alipoteza kiti chake akitafuta matibabu katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Bila shaka, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wafaa kusimama kidete kupinga dhuluma anazoendeleza Bw Magufuli dhidi ya wapinzani wake. Kwa sasa anairejesha kanda hii katika enzi ya giza.

[email protected]

Mjumbe hauawi jamani ni kupashana habari za majirani zetu wanavyo tuona. Lakini mwandishi anasahau kuwa EAC almost 90% + ya tawala ni za kidictator. Nani amfunge Paka kengere?
Peleka huko ass thread yako!
 
Kama anavyodharuliwa jiwe??

Maana nae hajui English [emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp hapa ukinunua la Musiba aka Tanzanite !!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Linanunulika sana hilo la Tanzanite kika siku copy zake zinaisha nenda pale Mnara wa Askari waulize wauza magazeti watakuambia magazeti yanayonunuliwa sana la kwanza ni Mwananchi then Tanzanite!
 
You must declare interest!
Jirani akikuponda mara nyingi ni wivu tu!
 
Wanadharau lugha ya Kiswahili hivyo hawawezi hata kukipa umakini chochote kilichoandikwa na Gazeti la Taifa leo achilia mbali hata kulisoma, isitoshe Taifa leo ni kama the nation hivyo maudhui siyo ishu, ishu ni lugha ya Kiswahili wanaona kama wanajishusha kusoma Gazeti lilliloandikwa kwa Kiswahili.
OK, kwa hiyo kwako wewe ambaye kiswahili una kienzi umekubaliana kabisa na mauzui ya andiko hilo? Hilo ndio la muhimu maana watakaosoma kwa kiswahili watawaeleza wengine taarifa hiyo kwa lugha wazipendazo.
Mfano mzuri ni hapa JF, kuna vitu tunaletewa kujadili wakati waletao wamevisoma kwenye taka iitwayo Uhuru au Mzalendo ambao wengine acha kuyasoma hata kuyagusa hatukumbuki ni mwaka gani.
 
Eric Kabendera kutoka Tanzania, anayeendelea kuzuiliwa na serikali ya Rais John Magufuli, kwa tuhuma za kuandika habari za “uongo na kuwapotosha” wananchi.
Kweli hili gazeti linapaswa kudharauliwa na wakenya.
Kama angetuhumiwa kwa makosa haya kwanini dhamana yake izuiliwe?

Mwandishi na Mhariri walichukua muda wao kujaribu kutafuta hati ya mashitaka anayo tuhumiwa Erick Kabendera na kupelekea kukosa dhamana ya kusikilizwa kesi yake akiwa nje ya jela?
 
Sijui kuhusu Msiba lkn Tanzania hakuna ,,classes” baina ya Wasomaji Magazeti kila mtu anaweza kununua Gazeti lolote na kusoma bila ya kujificha, Kenya ni tofauti, ukisoma Taifa leo unaonekana wewe ni mtu wa chini kabisa kwenye jamii ambaye haujui English language na hivyo wa kudharauliwa.
Wacha maneno mingi wewe, jiwe anafeli kwenye vitu ambavyo wala hakupaswa kufeli. Hata bila hilo gazeti ukweli wa kinachoendelea ndio huo, amejishushia credit kwa hofu, ubabe na umimi wake tu.
 
Utanyooka tu wewe fisadi
 
Wanadharau lugha ya Kiswahili hivyo hawawezi hata kukipa umakini chochote kilichoandikwa na Gazeti la Taifa leo achilia mbali hata kulisoma, isitoshe Taifa leo ni kama the nation hivyo maudhui siyo ishu, ishu ni lugha ya Kiswahili wanaona kama wanajishusha kusoma Gazeti lilliloandikwa kwa Kiswahili.
Punguza urongo
 
Kama anavyodharuliwa jiwe??

Maana nae hajui English [emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app

Lkn anajadiliwa kwa english Kenya kwenye media zote ila Tundu Lisu ndo anayedharauliwa hajawahi kujadiliwa ( Kenya) kwa english hata siku moja pamoja na kujipendekeza kwake kote kwa Wakenya, kwanza hata hawamjui!
 
Huoni ulivyonyooka? Umejaa stress tu. Magu anaendelea kupiga kazi tu kama kawa!!
Yaani hata kwa maandishi tu, nani anastress kati yetu mkuu. Unatumia nguvu sana kutetea vitu vya kitoto na ndio maana mnajibu kwa mihemuko.
 
Sisi tunaendelea kula nchi wala hatuna stress ndiyo maana tunaendelea kujenga nchi kwa nguvu kubwa!
 
Ni vizuri kama unakula nchi, ukumbuke pia wakosoaji nao wanakula nchi na wanajenga familia zao na nchi yao kwa nguvu kubwa
 
Back
Top Bottom