Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama HK Vision set ya camera nane ni laki 8 sidhani kama Camera 40 zinafika hata million 50 za kitanzania. Kweli serikali yetu kama kichwa cha mwendawazimu. Kila mtu anajinyolea tu.Katika kuhakikisha biashara zinafanyika saa
24, Jiji la Dar es Salaam limeingia mkataba na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unaogharimu jumla ya shilingi milioni 514 wa usimikaji wa mifumo ya kamera za ulinzi katika barabara na maeneo ya Kariakoo ambapo jumla ya kamera 40 zitakazofanya kazi kwa saa 24 zitafungwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo kwa ajili ya ufuatiliaji wa hali ya usalama na udhibiti wa matukio ya kihalifu.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema lengo la mpango huo ni kuimarisha usalama wa wanachi na wafanyabiashara na kuongeza ufanisi wa shughuli za kibiashara.
Amesema, kamera hizo hizo zitasaidia kurahisisha utambuzi wa matukio, kuimarisha ufuatiliaji wa wahalifu na kutoa ushahidi wa haraka inapohitajika.
My take:
Hawa watu wanaliibia sana hili Taifa na ifike wakati wenye akili kwenye vyombo vya dola waungane na Wananchi Wazalendo wachukuliwe hatua.
Baada ya Wizi mkubwa uliofanywa kwa kuongeza gharama za ujenzi wa viwanja vya michezo, leo umesainiwa mkataba kufunga Kamera 40 tu Kariakoo kwa gharama ya milioni 514.
Acha niendelee kuwaamini CHADEMA kuwa No Reform No Election. Nchi hii inaibiwa sana
View attachment 3240972
Wamesema camera zitakuwa ngapi labda vipi kuhusu kijumba Cha kuchunguza matukio na vifaa vyake zikoje vipi kuhusu mafunzo kuendesha mradiKama HK Vision set ya camera nane ni laki 8 sidhani kama Camera 40 zinafika hata million 50 za kitanzania. Kweli serikali yetu kama kichwa cha mwendawazimu. Kila mtu anajinyolea tu.
Na kawaida ya pesa ikifura na yale ma -Cardiovascular disease huwa hayachezi mbali na na-Cancerous nayo huwa yanapiga jaramba sio mchezo mchezo. !Waliompa dili siyo wajinga!
% yake ni 51.4m/-!
Siyo pafupi!
Awamu ya mama ni deals, deals, deals!
Akiondoka watu wamefura hela!
Vyote hivyo tunavitengenezea bajeti ili tuendane na wakati !!Wamesema camera zitakuwa ngapi labda vipi kuhusu kijumba Cha kuchunguza matukio na vifaa vyake zikoje vipi kuhusu mafunzo kuendesha mradi
Acha kuwa zwazwa hizo bei kazitoa wapi? Muulize hilo swali akikujibu ni taggMkuu kwa mchanganuo na ufafanuzi wa aina hii unaondoa mashaka na sintofahamu kwa wananchi. Hongera sana Mkuu, umeeleweka!!
Unadhani hatuwajui mnavyocheza na makaratasi?Ili huu mjadala uwe na maana, hebu tufanye uchambuzi mdogo hapa kwa bei na gharama za soko zilizopo kwa sasa. Hii itasaidia kupima kwa uhakika.
Nitafanya uchambuzi wa shughuli hii kwa ununuzi kamera za kiwango cha juu, tukichukua gharamani za vifaa, installation na huduma za ziada baada ya ufungaji.
Hii itatufanya tuweze kuona kama bei ya Tsh milioni 514 ni halali au ni ya juu kuliko inavyostahili.
1. UFUNGA KAMERA ZA CCTV ZA KIWANGO CHA JUU
Kamera 40 zitafungwa katika soko la Kariakoo kwa madhumuni ya kuimarisha usalama.
Kamera hizi zitahakikisha maeneo yote muhimu ya soko yanachunguzwa na kurekodiwa kwa video, hivyo kusaidia kupambana na wizi, ghasia, na uhalifu mwingine.
Kamera zitahakikisha usalama wa wateja na wafanyabiashara katika soko kubwa na lenye shughuli nyingi.
Aina ya Kamera Zitatumika
Kamera ni lazima ziwe za ubora wa picha wa juu, kuhakikisha kuwa picha zinakuwa wazi hata kwenye giza, zina uwezo wa kupiga picha kwa umbali mrefu, na zina teknolojia ya kutambua harakati.
Nitachambua baadhi ya kamera za kiwango cha juu ambazo zinaweza kutumika kwenye mradi huu.
2. AINA ZA KAMERA ZA KIWANGO CHA JUU NA BEI ZAKE
(A) Axis Communications Q-Series
- 4K resolution (Picha za ubora wa juu)
- Bei: Tsh 10,000,000 - 20,000,000 kwa kila kamera
- Sifa:
- Infrared night vision
- AI Motion Detection
- Face Recognition Technology
- IP67-rated (Inafaa kutumika kwenye hali mbaya ya hewa)
- Cloud storage kwa usalama wa data
- Kiasi cha Kamera: 40 kamera
- Jumla ya Gharama kwa Kamera 40: 40 × Tsh 15,000,000 = Tsh 600,000,000 (Bei ya wastani kwa kila kamera).
(B) Bosch MIC IP Fusion 9000i
- 40x optical zoom
- Bei: Tsh 8,000,000 - 15,000,000 kwa kila kamera
- Sifa:
- Thermal imaging (Mwangaza wa joto kwa ulinzi wa hali ya juu)
- Weather-resistant
- Real-time video streaming
(C) Hikvision DarkfighterX Series
- Kiasi cha Kamera: 40 kamera
- Jumla ya Gharama kwa Kamera 40: 40 × Tsh 12,000,000 = Tsh 480,000,000.
- Super low-light performance
- Bei: Tsh 7,000,000 - 12,000,000 kwa kila kamera
- Sifa:
- True color night vision
- Smart IR technology
- IP67 rating
3. GHARAMA ZA USAKINISHAJI, VIFAA VYA ZIADA, NA HUDUMA ZA BAADA YA USAKINISHAJI
- Kiasi cha Kamera: 40 kamera
- Jumla ya Gharama kwa Kamera 40: 40 × Tsh 10,000,000 = Tsh 400,000,000.
(A) Gharama za Usakinishaji na Wiring
Usakinishaji wa kamera za CCTV unahitaji nyaya za umeme, switches, na vifaa vya kuunganishia ili kuhakikisha kila kamera inafanya kazi ipasavyo.
Hii itajumuisha wiring kutoka kwenye NVR (Network Video Recorder) hadi kwa kamera. Hii inaweza kugharimu Tsh 70,000,000 kwa mradi mkubwa kama huu.
(B) Mfumo wa Kuhifadhi Video (NVR / Server)
Kamera 40 za CCTV zitahitaji server au NVR (Network Video Recorder) ili kuhifadhi video inayoendelea kurekodiwa kutoka kwenye kamera. Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kuhifadhi video kwa siku kadhaa ili kurahisisha upatikanaji wa video endapo kutahitajika kwa uchunguzi wa uhalifu.
- Gharama ya NVR/Server: Tsh 50,000,000 (kwa uwezo wa kuhifadhi video kwa muda mrefu, na salama).
(C) Gharama za Monita na Vifaa vya Kuonyesha Video
Kwa ufanisi, itahitaji monita (screens) kwa ajili ya kuangalia video za kamera, ambapo vituo vya kudhibiti usalama vitahitaji kuunganishwa na monita za ubora wa juu.
- Gharama za Monita: Tsh 10,000,000.
(D) Huduma za Matengenezo ya Baada ya Usakinishaji
Baada ya kuanzishwa kwa kamera, itahitajika huduma ya matengenezo na usimamizi wa vifaa, ili kuhakikisha kwamba vifaa vinaendelea kufanya kazi ipasavyo na kuwa na matengenezo ya mara kwa mara.
- Gharama za Huduma ya Matengenezo (kwa mwaka): Tsh 20,000,000.
4. UWEZEKANO WA GHARAMA YA TSH MILIONI 514
Gharama za Vifaa (Kamera)
Tuchukulie tunatumia Hikvision DarkfighterX Series kwa bei ya wastani ya Tsh 10,000,000 kwa kamera.
- Jumla ya Kamera 40: 40 × Tsh 10,000,000 = Tsh 400,000,000
Gharama za Usakinishaji na Vifaa Vya Ziada
Jumla ya Gharama:
- Usakinishaji & Wiring: Tsh 70,000,000
- NVR/Server: Tsh 50,000,000
- Monita: Tsh 10,000,000
- Huduma ya Matengenezo: Tsh 20,000,000
Tsh 400,000,000 (kamera) + Tsh 70,000,000 (usakinishaji) + Tsh 50,000,000 (NVR/Server) + Tsh 10,000,000 (monita) + Tsh 20,000,000 (huduma) = Tsh 550,000,000.
5. MAJUMUISHO
Kwa kutumia kamera za kiwango cha juu kama Hikvision DarkfighterX Series, gharama halisi ya mradi huu ni karibu Tsh 550,000,000, ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 514 zinazozungumziwa.
Hivyo, kazi yetu kwenye hili ni kujua ni aina gani ya kamera na vifaa vingine vitakavyotumika kwa shughuli hii ili kuona gharama iliyotajwa itaendana na bei husika.
Ova
ulinzi na usalama wa watu, makazi na biashara zao ni muhimu zaid ya upotoshaji wowote ule unaolinganisha pesa, maisha na uhai wa mwanadamu,WIZI MZURI NI USEME TUTAFUNGA KAMERA KARIAKOO YOTE KWA THAMANI YA SHS BILIONI MOJA, USITAJE IDADI YA KAMERA, HUU TUNAUITA UIZI MZURI, LAKINI UNAPOTAJA NA IDADI YA KAMERA HAPO NDIPO UNAKOSEA
Msisahau kwamba camera inaona na kutoa mrejesho pengine kwa kile kilicho onwa lakini hazikamati, je mmeandaa usafiri ama mgambo kwaajili ya hayo matukio?Vyote hivyo tunavitengenezea bajeti ili tuendane na wakati !!
kwamfano,Kozi nzuri ni PROCUREMENT AND SUPPLY.Hakika pesa zinapigwa.
ni muhimu pawepo pa kuanzia hususani kariakoo kulingana na potentiality ya kwa uchumi wa mtu moja moja na kwa taifa kwa ujumla 🐒Mkuu kwani Kariakoo ndio Tanzania nzima, na Kamera 40 zitaona mitaa na vichochoro vyote vya Kariakoo???
zipo za hadi 30m gentleman,Mkuu ujue kwa fedha ya Bilioni 1, hapa una maanisha Kamera 1 shilingi milioni 25,700,000/=. Duh!!
kwa mfano,Mkuu ni kamera 4,000 au 400 au 40??
Mchanganuo wa kina kwa lugha nyepesi unahitajika kufafanua kwa wananchi kuhusu matumizi ya fedha hii ya milioni 514.
Hii fedha Sio mchezo ati??
Wanao lalamika kuhusu bei je wanajua kwamba ulinzi wa siri kwa kutumia CCTV unaweza kufanyika hata kama kuna Giza Totoro?ni muhimu pawepo pa kuanzia hususani kariakoo kulingana na potentiality ya kwa uchumi wa mtu moja moja na kwa taifa kwa ujumla 🐒
Wamesema camera zitakuwa ngapi labda vipi kuhusu kijumba Cha kuchunguza matukio na vifaa vyake zikoje vipi kuhusu mafunzo kuendesha mradi
SawaHata ukiweka server na control room infrastructure bado million 500 ni nyingi mno. Labda kama camera watazoweka ni tofauti na hizi tunazozifahamu sisi.