Duh mjadala umebadilika na kuwa wa wenye ndoa na wasio na ndoa?!!! Makubwa
Hata hivyo ninachiokiona hapa ni vitu viwili. Wapo wanaotetea kuwa mume asamehewe (Ingawaje mwenyewe hajaonyesha kutaka kusamehewa!) na wapo wanaosema asisamehewe (Japokuwa mwenyewe hajaomba msamaha!).
Kuna kina Pillu na Tuko ambao wanashutumu wasio na ndoa, napenda tu kuwakumbusha dada zangu kuwa sio wote walio na ndoa wana ndoa! Wengine wana mizigo ambayo WANATAMANI sana kuishusha ila tu hawana hizo guts kutokana na sababu mbalimbali, wanaishi kwenye ndoa ambazo maisha yao ni sawa na jehanam lakini hawana jinsi zaidi ya kuendelea kuishi hivyo wakimpendeza binadamu mwenzao.
Ninapata picha kuwa tunajisahau kuwa maisha (na viumbe vyake) ya sasa yamebadilika sana. Wanandoa wa kizazi hiki si wanandoa wa kizazi cha wazazi wetu (ambacho naamini kabisa ndicho wanachojaribu kukizungumzia kina dada Pillu hapa). Kizazi cha sasa kimejaa wanandoa wa dot.com. kuanzia mapenzi hadi majukumu.
Natamani kuamini kuwa Pillu na dada Tuko na wengineo ambao mmekuja na hoja ya wenye ndoa na wasio na ndoa, ni wale wanandoa wa enzi hizo, wanandoa ambao wanaelewa maana halisi ya ndoa kutokana na nyakati zao au la sivyo ni wanandoa walioolewa na wanaume wa enzi hizo (In a positive way tafadhali).
Wanaume ambao kwanza atafanya juu chini asikudhalilishe mkewe,
wanaume ambao hupenda heshima ianzie kwake nyumbani, asiyewezakuwaza kumtongoza mtogto wa kazi achilia mbali kubaka.
Wanaume waliopelekwa jandoni wakafundishika, ambao hata akiamua kucheat basi atacheat kwa makini sana na ikitokea amedakwa ni mwanaume ambaye yuko radhi kuyamalizia chumbani na mkewe kwa kukiri na kuomba msamaha.
Wanaume wa dot com ndio kama hawa, kwanza hajaona ugumu kula kwenye zero grazing!, pili kafumwa analeta ubabe wa kutaka kugawana mali yaani hajutii kabisa kosa na wala haonyeshi kukiri, haya huo msamaha mnaotaka huyu binti autoe anausamehe kwa kosa gani lililokiriwa??
Wanaume wa dot com kwa taarifa yenu hawajafundwa kulearn from their mistakes, bali wamefunzwa (from peers) kulearn from misamaha ambayo kwa bahati mbaya hawaichukulii kama misamaha bali huichukulia kama udhaifu wa mwanamke. Kwao ukimsamehe atasema umekubali yaishe kwa kuwa kwake umefika hupindui hugeuzi na hivyo kumpatia picha kuwa anawezafanya lolote usireact.
Tuko na Pillu mnalo somo zuri sana katika hili tukio ambalo tunatamani sana kujifunza lakini badala ya kusimamia kwenye debate ya wenye ndoa na wasio na ndoa ni vema mkatrupa hizo experience zenu za ni namna gani amsamehe (mtu ambaye hajaomba msamaha), aongee naye au anyamaze tu maisha yaendelee (itaeleweka kuwa amesamehe?) au kama anapaswa kuongea naye aongee naye nini?
Tupeni na upande wa pili wa shilingi kuwa mwanaume huyo afanyeje, maana ashakuja na kudai mke apige mahesabu ya mali walizochuma ndoa iishie hapo, je bado mnataka asamehewe kwa kosa ambalo mwenyewe hajaona kama amekosea??
- Katika situation klama hii, huyu binti inayesemekana amebakwa anaangukia wapi?
Ni mtazamo wangu tu, samahani kama kuna nlomkwaza but kusema ukweli nina mengi ninayoyatamani kuyajua kutoka kwenu, yatanisaidia sana kuidumisha hii ndoa yangu ya mkeka niliyoipata mkesha wa sikukuu.