Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga amesema sababu ya kuchukua muda mrefu kudhibiti moto katika Soko la Kariakoo ni kutokana na kutokuwa na sehemu za kuchukulia maji ndani ya Kariakoo hivyo iliwalazimu kuyafuata Airport.
Changamoto ya mfumo wa maji uliopo katika eneo la Kariakoo umetajwa kuwa chanzo cha moto uliozuka katika Soko Kuu la biashara Kariakoo kutodhibitiwa mapema.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema lilitumia saa sita kudhibiti moto huo kutokana na kufuata maji umbali mrefu kutoka Kariakoo mpaka Airport.
Akizungumza leo Jumapili Julai 11, 2021 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto, John Masunga amesema kutokana na umbali mrefu wa kufuata maji hayo ilileta ugumu katika kupambana na moto huo.
“Jeshi la zimamoto tuliwahi kufika katika eneo hili kabla ya saa 3 usiku na kuanza kuzima moto, lakini kwa bahati mbaya eneo hili la Kariakoo mifumo ya maji haifanyi kazi.
“Kutokana na changamoto hii tulikuwa tunaweza kupata maji Airport huko ndiko tulikokuwa tunafuata maji, kazi ilikuwa ngumu na tukafanikiwa kuudhibiti saa 8 usiku,” amesema Kamishna Masunga.
Amewataka wananchi kuchukua hatua mapema kwa kupiga namba 114 pindi yanapotokea majanga ya moto ili kuweza kudhibiti mapema kabla haujasambaa.
Kamishna Masunga amesema changamoto nyingine ambayo walikutana nayo ni msongamano wa watu katika eneo la tukio wakati magari ya zimamoto yakiwasili na hivyo kusababisha usumbufu.
PIA SOMA:
1. News Alert: - Soko la Kariakoo lateketea kwa moto
2. News Alert: - Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu