Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Kwa hiyo machinga/wananchi ndio wenye wajibu wakuweka matoleo ya maji kwa ajili ya fire?
Hata ramani hazijui za matoleo ya maji hapo mjini.
Uchumi wa kati!
 
Hawa zimamoto ni manunda kikosi chenye hadi kamishna si wangefuata maji hapo fire.
Mm naona hakuna haja ya hiki kikosi hivi waliwahi kusaidia wapi?
Kariakoo kitovu cha biashara nchini hamna matoleo ya maji kweli na kamishna anazubutu kutamka haya bwana kazi iendelee
 
Hili nalo linahitaji katiba Mpya...

Taifa hili linahitaji kuongozwa na viongozi wababe kuanzia Rais na mawaziri wake...Watanzania wanahitaji ubabe walau kwa miaka 50 hivi ili akili zikae sawa na fikra ziwe sharp...tukiendelea kubembelezana basi tutachukua miaka milioni mbili kufikia maendeleo ya dunia...

Leo hii eneo kama Kariakoo halina fire hydrants wala mifumo ya kisasa kusuppress moto immediately...Jiji la dar halina standby unit kwa ajili ya sensitive areas 24/7 ..halafu mnataka tubembelezane maofisini au tufokewe huku tukibembelezwa...Mijeledi muhimu (trump aliposema Africa inahitaji miaka 100 kutawaliwa alimaanisha ukatili maana tuliiruka hii stage mapema ikiwa bado inahitajika)
 
Jeshi la zimamoto lina upungufu wa magari ya kisasa ya kupambana na moto serikali inabidi iwekeze sana kwenye hili jeshi,siombei lakini imagine kituo cha mafuta au gesi kinalipuka leo hii tutaweza kukizima kwa ustadi kweli au ndio tutabakia kusema Mungu atusaidie na sio kupambana na majanga ya moto kwa njia za kisasa zaidi ilikuokoa mali na maisha ya watu
Jeshi halina bajeti lile hata magari ni shida, moto unatokea wenyewe maji hawana.
Jeshi liko unpopular mtu akiunguliwa nyumba anakimbilia Polisi badala ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

The same mtu akipata ajari ya gari anaita Polisi, Zimamoto wanaokoa nini ikiwa hawana equipment za kumsaidia mtu aliyepata ajali ili afike hospital kupata huduma?

Hawana boti, hawana ambulance huo uokoaji wanafanyaje hasa??
Wana madaktari wa huduma ya kwanza?
Wana kikosi cha wazamiaji? Mbona meli zetu, mitumbwi inazama wanaitwa watu wa kitaa kuja kuzamia na sio Zimamoto?

Jeshi linaajiri watu wa taaluma za shule mara procurement, uhasibu, civil engineering hizi za nini sasa? Matokeo yake watu wakimaliza kozi wanavaa nyota kazi imeisha wanakula salary tu ila ufanisi na specialization sifuri
 
Jeshi la zimamoto lina upungufu wa magari ya kisasa ya kupambana na moto serikali inabidi iwekeze sana kwenye hili jeshi,siombei lakini imagine kituo cha mafuta au gesi kinalipuka leo hii tutaweza kukizima kwa ustadi kweli au ndio tutabakia kusema Mungu atusaidie na sio kupambana na majanga ya moto kwa njia za kisasa zaidi ilikuokoa mali na maisha ya watu
Kwa jeshi letu la zima moto, tatizi lao ni zaidi ya magari, maji wanayafuata wapi?kama jana kariakoo nzima haina sehemu ya kuchukulia maji hadi walikuwa wanaenda kuyachukua uwanja wa ndege!!kweli sehemu kama kariakoo hakuna fire hydrants?!!
 
Wakulaumiwa sio zimamoto, zimamoto hawana jukumu la kujenga miundombinu. Lawama zote nazielekeza kwa utawala dhalimu wa CCM
Wakulaumiwa ni hao zimamoto
Nafahamu kwamba jeshi la zima moto linajukumu la kufanya ukaguzi na kutoa ushauri kuhusiana na viashiria vyote vinavyoweza sababisha moto au kuathiri zoezi la zima moto.
Je walishafanya ukaguzi huo hapo Kariakoo na Kama walifanya walishauri au walichukua hatua gani.
Manake juzijuzi tu walipita ofisini kwetu kutukagua wakatushauri na kutupiga faini kwa sababu hatukuwa na vifaa vya kuzima moto
 
Jeshi halina bajeti lile hata magari ni shida, moto unatokea wenyewe maji hawana.
Jeshi liko unpopular mtu akiunguliwa nyumba anakimbilia Polisi badala ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji...
Kama haya ni kweli Kuna baadhi ya kampuni binafsi za ulinzi wana magari ya zimamoto kwanini wasingesaidia?
 
Kama haya ni kweli Kuna baadhi ya kampuni binafsi za ulinzi wana magari ya zimamoto kwanini wasingesaidia?
Kusaidia mpaka uguswe kama hujaguswa huwezi kusaidia na situation ya mjini hapa kila mtu hufanya mambo yake unaweza kupigwa ngeta pale Kariakoo mchana kweupe mpaka ukafa watu wanapita kando tu.

Hayo ndo maisha ya hapa mjini
 
Kamishna Jenelari wa Zimamoto John Masunga amesema walichelewa kuuzima moto ulioteketeza soko la Kariakoo kwa sababu walilazimika kufuata maji Air port kule Kipawa.

Masunga amesema Kariakoo yote haina matoleo ya maji

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Kazi hapa imekwama kulikoni ndugu yangu John.
 
Chadema badala ya kupigania magari ya kuzima moto yawe mengi hapa nchini na pia maji yapatikane.

Wanaona umuhimu zaidi kupigania mitukano ya hadhara.
 
Nchi hii bwana,
Bungeni wataalamu huwa hawaeleweki.
Kwenye taasisi nako,maji kariakoo hakuna hadi airport

Halafu unatoa speech yakujikinga na majanga ya moto
 
Miaka yote hamjaweza kuwa na visima vyenu wenyewe.Moto unatokea Mara ngapi Hadi msiwe na maji ya tahadhari.
 
Chadema badala ya kupigania magari ya kuzima moto yawe mengi hapa nchini na pia maji yapatikane.

Wanaona umuhimu zaidi kupigania mitukano ya hadhara.
Unawaza vyama wa kati ndivyo vinaongoza nchi.umechanganya agenda
 
Kinachosababisha moto ni nishati, oxygen au fuel. Ukitoa kimoja kati ya hivi moto unakufa. na Sheria za usalama wa moto zinasema, nyumba ya biashara kama ni ya kupangisha yenye watu wasiozidi watano. Mwenye nyumba ni lazima aweke blanket la kuzimia moto jikoni.
Watu wakizidi watano kuwe na blanket na fire extinguisher.

Watu 50 ni lazima kuwe na horse pipes katika ujenzi. Haya ni mambomba yanayotoa maji kwa pressure kubwa na yasipoangaliwa vizuri yanaweza kuleta mafuriko. Ni watu waliopitia mafunzo tu ndiyo wanatakiwa kuya operate.
 
Back
Top Bottom