Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Siku zote huwa yanakuwa na maji tayari ya kuanzia , yanasubilia tukio, ila sasa yakiisha hayo aliyo nayo sehemu ya kuchukulia mengine ndio balaaa!!na yale magari yao akifungua tu koki, lita 15, 000 ni dakika 5 tu yameisha!!ndio pale WANANZENGO, wanasema limekuja na maji nusu!!nayule aliyoko mbali na tukio ila aliliona gari likielekea kwenye tukioa, atakwambia gari limekwenda bila maji!!kwani anaona ndani ya dk 10, limegeuza!!!kwa moto mkubwa maji hayaepukiki kamwe, hizo chemikali lazima zitachanganywa kwenye maji kutegemeana na kundi la moto.
Yafungwe tela la maji nyuma kama tank za mafuta
 
Kama ni ivyo kikosi cha Zimamoto kiwe kitengo ndani ya wizara ya maji,kwa hapa dar nashauri dawasco iwe na kitengo cha zimamoto ili likitokea janga la moto tena tuwaulize hao dawasco wamekosaje maji ilihali wao wanamaji muda wote
 
Yani kamishina bora angekaa kimya kuliko kuongea utumbo

Kutoka makao makuu ya jeshi la zima moto hadi soko la kariakoo ni kilomita moja

Yani huoni hata aibu unasema makao makuu ya jeshi la zima moto hakuna maji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamishna Jenelari wa Zimamoto John Masunga amesema walichelewa kuuzima moto ulioteketeza soko la Kariakoo kwa sababu walilazimika kufuata maji Air port kule Kipawa.

Masunga amesema Kariakoo yote haina matoleo ya maji

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Kwani maji ya bahari hayafai kuzimia moto?
 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga amesema sababu ya kuchukua muda mrefu kudhibiti moto katika Soko la Kariakoo ni kutokana na kutokuwa na sehemu za kuchukulia maji ndani ya Kariakoo hivyo iliwalazimu kuyafuata Airport.

Changamoto ya mfumo wa maji uliopo katika eneo la Kariakoo umetajwa kuwa chanzo cha moto uliozuka katika Soko Kuu la biashara Kariakoo kutodhibitiwa mapema.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema lilitumia saa sita kudhibiti moto huo kutokana na kufuata maji umbali mrefu kutoka Kariakoo mpaka Airport.
Kwa hiyo hata ofisi yake hapo fire hana hydrants wakati magari yanaishi hapo
 
Na fala mwingine anataka kutumia million mia mbili kununua taa za ofisi usikute hata ofisi yake haina fire extinguisher
Huyu wa taa ni yupi tena! Viongozi wetu wameingiwa na ugonjwa gani!?
 
Hili litakuwa fundisho maana asiseme watu pia aseme na meza za machinga mtaa wa pemba ziligharimu sana sana fire kufanya kazi zake kwa ufanisi
Nb;mji upangwe upyaa kuna mahali tunakosea kama Taifa.
 
Mifumo Mingi ya maisha Yetu iko hovyo hovyo...tunadhani kujenga mabarabara na Ma SgR pekee ndio maisha kumbe kuna mambo chini huku tunatakiwa kuyaweka sawa.

hatupangi Miji...Hatuna Mipangilio ya Maisha kwamba hapa Ni eneo la makazi basi Bar zisiwepo ..Leo hii kuna utitiri wa Vituo vya mafuta Hata katikati ya makazi ya watu..Ni change of land Use basi Kituo kinawekwa hivi jamii hii ya kituo kila sehemu inajitambua??

Ikitokea Moto nini tutafanya?? Je hawa wanaotakiwa kuzima nao watafanyaje kazi kama Maeneo hata ya kupitisha gari yamejaa machinga??? Kuna shida kubwa ya kuangalia kama nchi...

Suala la Machinga ni bomu lingine ambalo kila Mwanasiasa anataka kufaidika Nalo....Kusema ni wanyonge kumbe mnalea bomu...
 
Yule dada X wa kiba na daimond
Kusema ukweli tumerogwa!

Screenshot_20210712-112657_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom