Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Kama tungekuwa na visima vitano vinavyozungika soko. Vyenye pampu za 50m3/h . Wala tusingekuwa tunajadili moto mdogo kama ule wa jana.

Ila pia kuna mabomu ya kuzimia moto, unalitupa ndani. Likilipuka linazima moto kwa kuondoa . Oxygen.
 
Nadhani fire kijografia wako Karibu Sana na posta ambako kuna bahari, kama maji ya bahari hayana shida uko ndio wangejitahidi kukimbilia kwani foleni yake sio kubwa kuyafikia .inabidi sasa waweke miundo mbinu huko baharini watafute wataalamu wataoweza kuyasafisha na yakawafaa maana kwa Maelezo haya maeneo yote ya city cinter yako hatarini yakishika moto kutokana na changamoto za maji. Tungeachana na miradi mengine isio na tija sana Kama ujenzi wa masanamu na hizo hela tukazielekeza kwenye mambo ya msingi Kama haya la kariakoo lifikishe salamu kwa washika mpini kuwa fire inahitaji kuwezeshwa kimiundo mbinu maana Tuko bize kuyakaribisha majengo marefu nchini lakini kama tunashindwa tu kuyawezesha magari ya chini kuwa na maji itakuwaje hayo majengo ambayo hadi helicopter ushirikishwa kuyazima yakiwaka siku moja .kweli tunahitaji fire wawezeshwe mambo yalokuwa nje ya uwezo wao. Nawapongeza sana kwa kujitahidi kuudhibiti moto
Tatizo hatuna viongozi wanaofikiri kwa lengo jema la kuondoa changamoto tumizonazo kama Taifa.

Kila mtu anawaza kiki tu.

Media zetu zinaiharibu hii nchi kwa kuwapa kiki viongozi tulio nao.

Nchi ya kiki, we can't think straight.
 
Tatizo hatuna viongozi wanaofikiri kwa lengo jema la kuondoa changamoto tumizonazo kama Taifa.

Kila mtu anawaza kiki tu.

Media zetu zinaiharibu hii nchi kwa kuwapa kiki viongozi tulio nao.

Nchi ya kiki, we can't think straight.
Leo asubuhi nilikuwa natokea ⛪ nkapita kule buguruni malapa kule chini kwenye mabwawa ya maji taka nkakuta ujenzi wa mfereji unaendelea nkajiuliza na nkajijibu mwenyewe kweli tukiwa na viongozi makini mambo yanaenda big up Sana kwa MMBUNGE wa ilala zungu Huyu jamaa anastahili kufia madarakani sio muongeaji sana ila unakuta ndani ya Jimbo lake miradi inaonekana. Vuka tu ule mto msimbazi uingie Kigogo iliyo chini ya kinondoni barabara za mitaani hazieleweki najiulizaga sana kuhusu wabunge walio kinondoni sijui kwanini uisahau Kigogo hata kupitisha greda mitaani kunawashinda .mkuu kweli viongozi makini wako wachache mno
 
Magari ya washawasha hapa Tanzania hayajawahi kukosa maji japokuwa yale maji yake ni more technical na ni gharama zaidi ila magari ya zimamoto ambayo maji yake ni ya kawaida hayana maji.Mtu mweusi ni Kima aliechangamka🐒🐒🐒
 
Gari si lilitakiwa liwe na maji ama
Liko moja tu hapo mjini?.

kuzima kwa Co2 je?

anyways wengine sie sio wataalamu
 
Chadema badala ya kupigania magari ya kuzima moto yawe mengi hapa nchini na pia maji yapatikane.

Wanaona umuhimu zaidi kupigania mitukano ya hadhara.
Hiyo sio kazi ya CHADEMA

Mbona magari ya maji ya kuwasha hayaishiwi maji?
 
Yaani hata apo fire hawana sehemu za kuchukulia maji
Yaani nyumba ya daktari haina hata panadol!!hii nchi bwana utadhania tulidondoshwa tu hapa kwa bahati mbaya tu, halafu mijitu ilikuwa ina waza kuleta drones za kuzima moto, na ulikuwa ukiisikiliza ikitetea hoja zao hizo, utadhania hivi vitu vidogo kama visima vya maji yalishamaliza!!!
 
Me nilijua gari la zimamoto linakuwa stand by na maji ikitokea dharula linakimbia haraka kwenye tukio kumbe ikitokea hatari ndo gari linaanza kutafuta maji???
Ata mimi nilikuwa na wazo kama lako ngoja niendelee kusoma maoni ya wadau nijue nani wakulaumiwa
 
Hakuna sehemu ukieleza ukweli kama JF unapoteza hata habari yako.
Ndio maana watu wamekimbilia mitandao mingine !.
JF ukweli wa habari kwa sasa una angaliwa watu,unaanglia nani kasema.

Kama siri ya lugola ingekuwa hapa ishatolewa au ingekuwa ya youtube na watazamaji
 
Yaani nyumba ya daktari haina hata panadol!!hii nchi bwana utadhania tulidondoshwa tu hapa kwa bahati mbaya tu, halafu mijitu ilikuwa ina waza kuleta drones za kuzima moto, na ulikuwa ukiisikiliza ikitetea hoja zao hizo, utadhania hivi vitu vidogo kama visima vya maji yalishamaliza!!!
Yaan ofisi ni majengo tu na sehemu ya kupaki gari bila vitendea kazi dah kwaivo wakisikia janga ndo kuwasha magari kuelekea kipawa kuchota maji ndo warudi
 
Gari si lilitakiwa liwe na maji ama
Liko moja tu hapo mjini?.

kuzima kwa Co2 je?

anyways wengine sie sio wataalamu
Siku zote huwa yanakuwa na maji tayari ya kuanzia , yanasubilia tukio, ila sasa yakiisha hayo aliyo nayo sehemu ya kuchukulia mengine ndio balaaa!!na yale magari yao akifungua tu koki, lita 15, 000 ni dakika 5 tu yameisha!!ndio pale WANANZENGO, wanasema limekuja na maji nusu!!nayule aliyoko mbali na tukio ila aliliona gari likielekea kwenye tukioa, atakwambia gari limekwenda bila maji!!kwani anaona ndani ya dk 10, limegeuza!!!kwa moto mkubwa maji hayaepukiki kamwe, hizo chemikali lazima zitachanganywa kwenye maji kutegemeana na kundi la moto.
 
Yaani sisi wa pembezoni ya mji hali itakuwaje?

Makato yote haya wanayochukua yanafanya kazi gani?
 
Yaan ofisi ni majengo tu na sehemu ya kupaki gari bila vitendea kazi dah kwaivo wakisikia janga ndo kuwasha magari kuelekea kipawa kuchota maji ndo warudi
Hahahaaha!!pale linapokuwa limepaki huwa lina maji full ya kuanzia tu!!balaa ni pale yanapoishaa!!
 
Afu waoga haoo wanaogopaga kuungua wanamwaga maji ata ayafiki
Hahaaa!!una kuta hata hivyo vitendea kazi vyenyewe ni utata mtupu, hiyo mipira yenyewe unakuta inavuja balaa, maji mengi yanaishia chini!!ki uweli ktk majeshi , zimamoto na magereza yamesahaurika kabisa!!
 
Nafikiria ikiwa yametumika masaa 6 kuudhibiti moto mita 300 tu toka fire headquarters je sisi wa kisemvule,bunju, na chamazi itakuwaje?
 
Kama haya ni kweli Kuna baadhi ya kampuni binafsi za ulinzi wana magari ya zimamoto kwanini wasingesaidia?
Miaka ya nyuma 2015-, ktk jiji la dar es salaam maeneo mengi ulikuwa unayakuta magari binafsi ya kuzima moto , kama night support, yalikuwa standby , na matukio ya moto yalikuwa yakitokea wanashirikia na hayo ya serikali, ila miaka hii ni nadra sana kuyaona, sijui walikutana na zile sera za ujamaaa, zikawatoa sokoni!!!
 
Ila wale jamaa wakiandamana tu maji ya kuwasha yanapatikana fasta tu
 
Back
Top Bottom