Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Kamishna Jenerali wa Zimamoto: Changamoto ya maji Kariakoo ilisababisha kuchelewa kuzimwa kwa moto

Jeshi la zimamoto lina upungufu wa magari ya kisasa ya kupambana na moto serikali inabidi iwekeze sana kwenye hili jeshi,siombei lakini imagine kituo cha mafuta au gesi kinalipuka leo hii tutaweza kukizima kwa ustadi kweli au ndio tutabakia kusema Mungu atusaidie na sio kupambana na majanga ya moto kwa njia za kisasa zaidi ilikuokoa mali na maisha ya watu
Mkuu, ukizungumzia kituo cha mafuta, wanakupa majibu simple, utasikia "...mkiona moto kimbilia ndoo za mchanga"
 
Ondoa idara zote za zimamoto kutoka jeshini na peleka kwa serikali za ndani(metro,manisipaa)hiki kikosi kiendeshwe kiraia sio kijeshi na hii itasaidia kwa kila manisipaa kuwa na kikosi chake cha uokoji including fire dept.
 
Me nilijua gari la zimamoto linakuwa stand by na maji ikitokea dharula linakimbia haraka kwenye tukio kumbe ikitokea hatari ndo gari linaanza kutafuta maji???
Maji yakitumika lazima yaishe na yanapoisha lazima yakajazwe kwenye gar.
 
Kamishina aliyepita na Kange lugola ndio walipendekeza magari meengi mpaka chopa za kuzimia moto.kumbe hata pa kubebea maji hawana.
 
Hawa fire nimewakubali cheki wanavyowahi kwenda kuzima moto

Ova
 

Attachments

  • VID-20210711-WA0021.mp4
    3.2 MB
Jeshi la zimamoto lina upungufu wa magari ya kisasa ya kupambana na moto serikali inabidi iwekeze sana kwenye hili jeshi,siombei lakini imagine kituo cha mafuta au gesi kinalipuka leo hii tutaweza kukizima kwa ustadi kweli au ndio tutabakia kusema Mungu atusaidie na sio kupambana na majanga ya moto kwa njia za kisasa zaidi ilikuokoa mali na maisha ya watu
Imagine wanafuata maji JNIA, ina maana hata hata ofisini kwao mita chache toka Kariakoo hawana hydrants,
 
Nadhani fire kijografia wako Karibu Sana na posta ambako kuna bahari, kama maji ya bahari hayana shida uko ndio wangejitahidi kukimbilia kwani foleni yake sio kubwa kuyafikia .inabidi sasa waweke miundo mbinu huko baharini watafute wataalamu wataoweza kuyasafisha na yakawafaa maana kwa Maelezo haya maeneo yote ya city cinter yako hatarini yakishika moto kutokana na changamoto za maji. Tungeachana na miradi mengine isio na tija sana Kama ujenzi wa masanamu na hizo hela tukazielekeza kwenye mambo ya msingi Kama haya la kariakoo lifikishe salamu kwa washika mpini kuwa fire inahitaji kuwezeshwa kimiundo mbinu maana Tuko bize kuyakaribisha majengo marefu nchini lakini kama tunashindwa tu kuyawezesha magari ya chini kuwa na maji itakuwaje hayo majengo ambayo hadi helicopter ushirikishwa kuyazima yakiwaka siku moja .kweli tunahitaji fire wawezeshwe mambo yalokuwa nje ya uwezo wao. Nawapongeza sana kwa kujitahidi kuudhibiti moto
 
Kauli hii ni ya kuwaambia wafanyabiashara/wajasiriamali wa kariakoo kweli???? Fire wanakosa maji?? kauli hii ina heal vp mioyo ya watu hao??

Maji ya kufuata JNIA? walishindwa kuomba backup mpaka wafuate wao? Hatuna cilivi defence hapa mjini . Wasicheze na watanzania kufikia level hii
 
Back
Top Bottom