Elections 2015 Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

Elections 2015 Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

​Hao ndugu wa Mgonjwa wakomae tu hapo,madaktari wasitoe ripot fake,ila kwa tukio hilo kama mtoa mada alivyoeleza ni kwamba Ndugai hana chake na kizimbani atapanda pasipo shaka.Nimtakie safar njema ya mahakamani....Ila pia inaonesha kwamba Dodoma atakuwa anaenda kutembea na si kikazi.WADAU "CHEO NI DHAMANA"
 
1. Huyo daktari pole yake kwanza. . . . .Lakini unamrekodi mtu bila.ruhusa yake nawe huna tahadhari yeyote as if unampiga mwanao picha ya birthday??!!!
2. Unaambiwa leo utanikoma bado tu. . . . .nimecheka hapo alipokuwa akikusanya nguvu. . . . Nguvu zipi kwa mtu mzima kama yule??!!!

Anyways. . . . Sheria ichukue mkondo wake kama rushwa na cheo kitamlinda ikumbukwe kuwa "corrective measures" zimekuwepo kabla ya mahakama. . . . . . . .
 
Watu waongo sana, hv ukipigwa na gogo usitoke ngeu...? Acheni kuwa kama mabinti .. sema alimtishia labda, ktk kuamua ndio mkutano ukavunjika...!!! Midume mingine kama mijike tu...!!!

Yaani upigwe na gogo..? Unajua gogo ww..? Yaani hawa wagogo ni shida, watu waongo waongo sana.... gogo unajua ukubwa wake..?
 
Ndugai amezoea kuishi kiubabe. Lazima adhibitiwe mapemaaaaa!!!!
 
Wsira ampiga ngumi mwenyekit wa ccm wa mkoa kwa tuhuma za kumpaka matope.

Kangi ampiga mtu mangumi katika kampeni kwa tuhuma za kumsema vibaya.

Ndungai ampiga mtu na gongo kichwani katika hofu ya kuanikwa maovu yake.

Baada ya ccm kuvuruga mfumo wa katiba, sheria na kanuni za nchi bungeni, sasa viongozi wa ccm wahalalisha maisha bila kufuata sheria wala taratibu. Walijiweka juu ya sheria za nchi wakiwa maofisini, sasa wajiweka juu ya sheria wakia uraiani katika maisha ya kawaida.

Hawa bado ni raia sahihi au ni miharifu iende jela? POlisi mko wapi?
 
Hata Arusha watia nia walizichapa. Ni Sera ya ccm.


Jimbo La Makete Pia Mbunge Anaemaliza Muda Wake Kamsukuma Mtia Nia Kwenye Kampeni Za Kura Za Maoni Hadi Kadondoka Eneo La Mang'oto,
Kisa Kasema Ukweli Maana Mh Mahenge Aliwadanganya Wananchi Kuwa Analeta Umeme Baada Ya Kuona Wafanyakazi Wa Mkongo Wa Taifa Wakichimba Mifereji
 
Ubabe wa bungeni kumbe mpaka jimboni? Sikio la kufa....


Alifikiri bado yuko bungeni akiwafokea na kuwakemea akina Lisu.
Unyenyekevu kwa hawa ma ccm ni ndoto. Duu huyu akikatwa huku ataibukia wapi kwa staili hii ya kutumia mgongo?
 
Yaani upigwe na gogo..? Unajua gogo ww..? Yaani hawa wagogo ni shida, watu waongo waongo sana.... gogo unajua ukubwa wake..?
Jay One tofautisha Gongo na gogo!. Wewe mwalimu wako wa kiswahili hakufanya kazi sawasawa.
 
Maskini Dr wameanza kukupiga, hebu jirudie zako huku tuendeleze gurudumu la maendeleo
 
Back
Top Bottom