Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,273
Aombe msamaha? Kwa kosa lipi? Kama kwa dhamira yake haoni kosa alilolifanya kwa nini aombe msamaha. Yeye anaona hana makosa. Anayedhani ana makosa apeleke hoja kwenye chombo kinachoweza kuthibitisha kama ana makosa au la. Hii habari ya kila mtu kujipachika uhakimu na kuanza kuhukumu watu ndio JK aliikataa hivi karibuni, na inavyoelekea, kuna wakati utafika hizi tuhuma zitazoeleka hadi zile za kweli zitaanza kuonekana pia ni za uongo, na zote zitapuuzwa. Watu wamekalia kuhukumu tu huyu fisadi huyu fisadi, this is ridiculous! Inanikumbusha hadithi niliyosoma nikiwa mtoto mdogo ya mtoto aliyekuwa anachunga mbuzi nyikani, alipoona upweke umemzidia, akaona afanye ujanja aite watu kwa namna ambayo lazima wangekuja tu. Akapiga kelele "wolf, wolf!", watu wakajazana pale kwa kuelewa mtoto anaomba msaada anakabiliwa na mbwa mwitu. Akaulizwa "mbwa mwitu yuko wapi?", akawa anajichekelesha tu, wakaondoka. Baada ya muda akapiga kelele tena, "wolf, wolf!" watu wakajaa tena kama mwanzo, lakini hakukuwa na mbwa mwitu. Wakajua sasa huu kumbe ndio mchezo wake. Baada ya muda kidogo akaja mbwa mwitu kweli, akaanza kumshambulia mtoto. Kapiga kelele weeeee, hakuna aliyekuja maana walishazoea huyu huwa anajipigia tu mikelele hovyo. Akararuliwa na mbwa mwitu.
Sasa nanyi ndugu zangu msije kutufanya turaruliwe na mbwa mwitu hivi hivi kwa sababu ya kutuzoesha kelele. Tupige kelele kukiwa na suala la kweli, na si tu kujaza watu kwenye forum. Maana tukiendelea hivi, baadae watu watazoea, hata tukiandika nini watasema, aah wamezoea hawa kujiandikia!
Licha ya mapungufu fulanifulani tena madogo aliyoonesha wakati wa uongozi wake, ninaamini Mkapa aliitumikia nchi hii kwa uadilifu wa kupigiwa mfano (hasa kama atalinganishwa na viongozi wengine wa Afrika), na anastahili kutuzwa si tu na huo mpango wa Mo Ibrahim, bali pia hata sisi watanzania tunapaswa kumuenzi. Yes, Mkapa for the prize.
Ndugu Kithuku,
Naona kinamna fulani hivi unakubali kuwa kuna tuhuma... ila hukubaliani na adhabu wanazozitaja watu 'kama hiyo ya kutopata tuzo'. Kama unakubali naomba basi utaje aina ya adhabu au uwajibikaji anaotakiwa mtu aufanye mtu anayetuhumiwa na wengi katika jamii yake.
Kingine ni kuwa, nimatumaini yangu unakubali kuwa uzembe, rushwa na aina nyingine mbalimbali za kutowajibika ipasavyo ndizo zinatufikisha pahala ambapo hata Mh.Rais wetu akiulizwa kwanini Watanzania bado ni duni anasema hana jibu.... ombi langu nikuwa ungeulizwa wewe hilo swali ungelijibu vipi na hatua zipi ungezichukua kuhusiana na wale wanaotuhumiwa kuwa wamehusika na ufisadi wa aina fulani katika jamii yao?! Ahsante.
SteveD.