Kampeni dhidi ya Mkapa asishinde Tuzo ya uongozi bora

Aombe msamaha? Kwa kosa lipi? Kama kwa dhamira yake haoni kosa alilolifanya kwa nini aombe msamaha. Yeye anaona hana makosa. Anayedhani ana makosa apeleke hoja kwenye chombo kinachoweza kuthibitisha kama ana makosa au la. Hii habari ya kila mtu kujipachika uhakimu na kuanza kuhukumu watu ndio JK aliikataa hivi karibuni, na inavyoelekea, kuna wakati utafika hizi tuhuma zitazoeleka hadi zile za kweli zitaanza kuonekana pia ni za uongo, na zote zitapuuzwa. Watu wamekalia kuhukumu tu huyu fisadi huyu fisadi, this is ridiculous! Inanikumbusha hadithi niliyosoma nikiwa mtoto mdogo ya mtoto aliyekuwa anachunga mbuzi nyikani, alipoona upweke umemzidia, akaona afanye ujanja aite watu kwa namna ambayo lazima wangekuja tu. Akapiga kelele "wolf, wolf!", watu wakajazana pale kwa kuelewa mtoto anaomba msaada anakabiliwa na mbwa mwitu. Akaulizwa "mbwa mwitu yuko wapi?", akawa anajichekelesha tu, wakaondoka. Baada ya muda akapiga kelele tena, "wolf, wolf!" watu wakajaa tena kama mwanzo, lakini hakukuwa na mbwa mwitu. Wakajua sasa huu kumbe ndio mchezo wake. Baada ya muda kidogo akaja mbwa mwitu kweli, akaanza kumshambulia mtoto. Kapiga kelele weeeee, hakuna aliyekuja maana walishazoea huyu huwa anajipigia tu mikelele hovyo. Akararuliwa na mbwa mwitu.
Sasa nanyi ndugu zangu msije kutufanya turaruliwe na mbwa mwitu hivi hivi kwa sababu ya kutuzoesha kelele. Tupige kelele kukiwa na suala la kweli, na si tu kujaza watu kwenye forum. Maana tukiendelea hivi, baadae watu watazoea, hata tukiandika nini watasema, aah wamezoea hawa kujiandikia!

Licha ya mapungufu fulanifulani tena madogo aliyoonesha wakati wa uongozi wake, ninaamini Mkapa aliitumikia nchi hii kwa uadilifu wa kupigiwa mfano (hasa kama atalinganishwa na viongozi wengine wa Afrika), na anastahili kutuzwa si tu na huo mpango wa Mo Ibrahim, bali pia hata sisi watanzania tunapaswa kumuenzi. Yes, Mkapa for the prize.

Ndugu Kithuku,
Naona kinamna fulani hivi unakubali kuwa kuna tuhuma... ila hukubaliani na adhabu wanazozitaja watu 'kama hiyo ya kutopata tuzo'. Kama unakubali naomba basi utaje aina ya adhabu au uwajibikaji anaotakiwa mtu aufanye mtu anayetuhumiwa na wengi katika jamii yake.

Kingine ni kuwa, nimatumaini yangu unakubali kuwa uzembe, rushwa na aina nyingine mbalimbali za kutowajibika ipasavyo ndizo zinatufikisha pahala ambapo hata Mh.Rais wetu akiulizwa kwanini Watanzania bado ni duni anasema hana jibu.... ombi langu nikuwa ungeulizwa wewe hilo swali ungelijibu vipi na hatua zipi ungezichukua kuhusiana na wale wanaotuhumiwa kuwa wamehusika na ufisadi wa aina fulani katika jamii yao?! Ahsante.

SteveD.
 
Ndugu Kathuku,

Ndugu Steved, ni kweli kama ulivyoninukuu. Mimi nashauri kwamba hao wanaojishughulisha na masuala ya kumpa tuzo, tuwaache waendelee na mipango yao ya tuzo. Kama wataona kwa vigezo vyao mwenye kustahili tuzo hiyo ni yeye, watampa, wakiona ni mwingine watafanya wanavyoona wao inafaa. Sisi tushughulikie ya kwetu ya ndani. Kama tuna matatizo naye huyu mzee tuyashughulikie huku ndani kama ni kumshitaki, kulalamika tume za maadili, sijui tume gani, namaanisha vyombo vyetu vya ndani tupate uhakika wa tuhuma kama zina ukweli, na kama kuna hatua zifuate kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu. Hivi hujawahi kuona mtoto ambaye shuleni ameshinda mtihani kuliko wote, kawa wa kwanza, lakini huko nyumbani alikojoa kitandani ule usiku wa siku ya mtihani? Sasa kama ni mwanao, unadhani jana kakojoa kitandani nyumbani, na leo kashinda mtihani shuleni walimu wanataka kumpa zawadi, utaenda kuwaambia eti msimpe zawadi huyu ni kikojozi? Wampe zawadi yake, akirudi nyumbani namwambia mwanangu zawadi umepata sawa, hongera, lakini hebu tuambie nani kakojoa kitandani jana?

Huo ndio ushauri wangu.
 
Kithuku, kwenye mfano wako ni kuwa- tayari utajua ni mtoto wako amefanya hivyo, unless kama una watoto wawili au watatu na wote wawe wanalala kitanda kimoja. Kizuri kingine ni kuwa adhabu kama ya kosa la kukujoa tayari utakuwa unaijua wewe kwani ni mzazi, kama mtoto anahitaji kuchalazwa viboko kulingana na mazingira yake, basi viboko vifanye kazi yake maana alisha onywa na nikuwa kukojoa kwake si ugonjwa pia kopo la kukujoa alipewa ila uzembe au ubishi wake umemfanya akojoe. Na kama mtoto ananguvu ya kufua mashuka yake basi na ayafue hata kama hayata takata, na jingine kama mtoto ndiyo amefanya hivyo kwa mara yake ya kwanza, basi inabidi asamehewe, aombe msamaha na aulizwe kile kilicho msibu ili utatuzi upatikane.

Nikirudi kwenye swala la Mh. Mkapa; dunia yetu hii ni ndogo, tuzo hiyo anayoweza kupata sawa imetolewa nje ya nchi au 'shuleni', lakini madhara ya tuzo hiyo yanaweza kuonekana 'shuleni na nyumbani' kama hayatatatuliwa. Kwani mtoto huyo atakuwa mzembe na hatawajibika katika kutumia choo ipasavyo na ikitokea ameenda kulala kwa ndugu au rafiki, aibu hiyo ndiyo itajijenga na itajitokeza kutokana na kutoishughulikia ipasavyo.

Kithuku, statement yangu hapo juu unaweza iona contradictory kiaina fulani kulingana na mfano uliotumia, lakini kikubwa ni kuwa 'tuzo hiyo' ikipatikana inaweza kutumika kama kihalalisho cha tuhuma na yote maovu yaliyokwisha semwa awali, kwani 'tabia mbovu ya mtoto' itakuwa si hivyo tena bali itakuwa 'tabia mbaya ya mtu mzima mwenye uwezo wa kurushia ngumi wampingao'.

SteveD.
 
MWK there are 7 wonders of the world, hili sasa litakuwa ajabu la 9 la dunia kwa Mkapa kushinda kwa uongozi bora!!

Ninaiunga mkono campaign yako kwa asilimia 110.

DOWN WITH BEN MKAPA, UP WITH HOPE!!!
 
Kithuku, mi ningeena shuleni kuwaaambia wasimpe zawadi kwa vile mtoto wangu ni kikojozi, hadi atakapojifunza kutokukojoa kitandani ndo anaweza kustahili zawadi!

Nijuavyo mimi zawadi za mashuleni, ukiachilia mbali academic achievements, pia ni kuangalia maadili ya mwanafunzi, kama ana tabia mbaya ya kupiga wenzie, kuwatukana, kuwachokoza chokoza, kuwaibia vikalamu vyao na madaftari nk, na waaalimu wanalijua hili, unadhani bado watataka kumpa zawadi hata kama amefanya vizuri kwenye,tuseme, hesabu? Kwa waalimu wenye upeo, hawatampa zawadi!
 
Kithunku, mi ningeena shuleni kuwaaambia wasimpe zawadi kwa vile mtoto wangu ni kikojozi, hadi atakapojifunza kutokukojoa kitandani ndo anaweza kustahili zawadi!

Nijuavyo mimi zawadi za mashuleni, ukiachilia mbali academic achievements, pia ni kuangalia maadili ya mwanafunzi, kama ana tabia mbaya ya kupiga wenzie, kuwatukana, kuwachokoza chokoza, kuwaibia vikalamu vyao na madaftari nk, na waaalimu wanalijua hili, unadhani bado watataka kumpa zawadi hata kama amefanya vizuri kwenye,tuseme, hesabu? Kwa waalimu wenye upeo, hawatampa zawadi!

Hapana jamani. Kigezo kinachotumika kumpa mwanao zawadi shuleni ni kufaulu mtihani. Kama kafaulu mtihani wake, apewe zawadi yake. Kigezo cha kumuadhibu nyumbani ni uthibitisho kwamba kati ya watoto watatu waliokuwa wanashirikiana naye chumba, yeye ndiye aliyekojoa kitandani. Basi kama kweli alikojoa kitandani, itendwe kama itakavyoonekana inafaa, kama ni kufua mashuka afue, kama kumng'ong'a na kumwimbia "kikojozi kakojoa, n.k". Hapo atajifunza mawili, kwanza kufaulu mtihani ni jambo jema, na pili kukojoa kitandani ni jambo baya. Kwa hiyo ataacha hiyo tabia mbaya ya kukojoa kitandani, na ataendelea kujitahidi kwenye masomo. Katika mtihani aliofaulu shuleni mtihani wa kukojoa kitandani haukuwepo. Apewe zawadi yake, na huku nyumbani tumpongeze, akishaifutika zawadi yake kibindoni, tunaendelea na shughuli yetu ya kumsakama kikojozi hadi aache, na pia ili tuwaonye watoto wengine watakaolala kwenye chumba hicho, kwamba faulu mtihani lakini usikojoe kitandani. Athari ya kumnyima zawadi yake aliyoifanyia kazi kiasi hicho ni kumkatisha tamaa yeye na wenzake wanaomfuata, tukajikuta tunapata watoto ambao nyumbani ni vikojozi na shule wanashika mkia.

Nikirejesha mfano huu kwa huyu mhe BWM, tusipotambua mchango wake tutakatisha tamaa hata wengine wenye nia ya kufanya bidii (licha ya mapungufu yao fulanifulani), hivyo tunapata viongozi ambao wenyewe mafisadi, na uchumi wanaua vilevile. Mimi nadhani bora nusu shari kuliko shari kamili.
 
Halafu naitwa Kithuku(jina halisi), sio kathuku(sijui ndege huyu!) wala kithunku. Asanteni.

Brian Jonathan Yared Kithuku. Wanaonifahamu popote walipo, salam. Ukiniandikia PM naweza kukupa email yangu.
 
Kithuku, Miye nimesharekebisha baadhi ya sehemu nilizokosea jina lako. Hata hivyo samahani sana.

....he he he, kuhusu ndege jina lake ni 'kasuku' 🙂 unaweza kumfundisha maneno akakariri na kuyasema apendapo yeye... niliyemjua mimi alikuwa wa jirani, nilikuwa namnyemelea jirani akiondoka na kumfundisha 'maneno ya nguoni'😀 , sikuchapwa viboko kwani sikukamatwa!!!!!

SteveD.
 
Kithuku, kwanza samahani kwa kukosea jina lako ndugu yangu, nami pia nimerekebisha, ni haraka haraka hii ya kutype...

unajua nini, mi ninavyoona, kama akinyimwa hiyo zawadi itasaidia sana pia wanaomfuata wajue kwamba:
-wakifanya umachinga ikulu kuna wa kuwauliza
-kiburi si maungwana..
Kinyume na hayo ni kuwalea pia viongozai ambao watakuwa wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa nje ya nchi huku wananchi tukiumia, halafu watakuwa wanapata zawadi, yes, na tutaendela kusema madamu amepata zawadi basi amefanya vizuri, la sivyo asingepata zawadi?

Labda pengine sikuuelewa mfano wako, lakini nadhani hapa bado hastahili zawadi hiyo HATA kwa vigezo ambavyo vimewekwa:

unaweza kuangalia kwenye hii website http://www.moibrahimfoundation.org/the-index.asp na unambie kama huyu mzee anaweza kuqualify vipi? withot any subjective judgement of course?
 
Kuna rafiki yangu amenambia kwamba Africa haiwezi kubadilika kamwe kwa sababu ya mind set ya wananchi wake!...Yaani Ubadhilifu utazidi kuwepo na utapongezwa kwa vitendo pamoja na kwamba watu wanapinga kwa kauli zao. Wezi walioiba mabenki hupongezwa wanapojenga majumba na kutunza familia zao. NI sifa kubwa ya mwafrica kuwa jambazi linalotanua...
Huu Mfano wa Mkapa umenipa picha hasa kuona kwamba humu JF mnapongeza Mkapa kupewa tuzo kama hilo pamoja na kwamba mnaelewa mabaya alokufanyieni.
On the other hand, sijawahi kuona jambazi lijnaloiba na kuua lakini halina mazuri!..Jambazi linaloiba na kuwalisha wanawe, likajenga mahekalu huwa linapunguziwa adhabu kwa macho ya Mdanganyika hata kama kinachotakiwa kuhukumiwa ni Ujambazi wenyewe na sio nje ya hapo.
Yes, sasa nakubali kuwa Africa ina wakati mgumu sana na pengine yawezekana usia mzuri kwetu ni kujiunga na mafisadi maanake mwisho wa yote bado utapewa sifa kwa vitendo viovu vilivyoonyesha mafanikio kidogo.

Mwafrika wa Kike mimi naomba hiyo address ya hao watayarishaji nitapeleka tuhuma zote hizi zinazomkumba huyu Mkapa!
Ionekane roho mbaya potelea mbali... hafai!...
 
Thank you Mkandara, In Tanzania we need more people like you who will call a SPADE a SPADE. Once again thank you and God bless you.
 
Ukweli ni kwamba apate hiyo tuzo au asipate, hakuna suluhu mpaka atakapotinga mahakamani, hatuwezi kukubali kuwa distracted na maneno ya tuzo, apate salama, lakini tuhuma bado zipo pale pale tu!

Tunamsubiri, aje ajibu tuhuma zake kwenye mahakama za wananchi bongo!
 
Kuna rafiki yangu amenambia kwamba Africa haiwezi kubadilika kamwe kwa sababu ya mind set ya wananchi wake!...Yaani Ubadhilifu utazidi kuwepo na utapongezwa kwa vitendo pamoja na kwamba watu wanapinga kwa kauli zao. Wezi walioiba mabenki hupongezwa wanapojenga majumba na kutunza familia zao. NI sifa kubwa ya mwafrica kuwa jambazi linalotanua...
Huu Mfano wa Mkapa umenipa picha hasa kuona kwamba humu JF mnapongeza Mkapa kupewa tuzo kama hilo pamoja na kwamba mnaelewa mabaya alokufanyieni.
On the other hand, sijawahi kuona jambazi lijnaloiba na kuua lakini halina mazuri!..Jambazi linaloiba na kuwalisha wanawe, likajenga mahekalu huwa linapunguziwa adhabu kwa macho ya Mdanganyika hata kama kinachotakiwa kuhukumiwa ni Ujambazi wenyewe na sio nje ya hapo.
Yes, sasa nakubali kuwa Africa ina wakati mgumu sana na pengine yawezekana usia mzuri kwetu ni kujiunga na mafisadi maanake mwisho wa yote bado utapewa sifa kwa vitendo viovu vilivyoonyesha mafanikio kidogo.

Mwafrika wa Kike mimi naomba hiyo address ya hao watayarishaji nitapeleka tuhuma zote hizi zinazomkumba huyu Mkapa!
Ionekane roho mbaya potelea mbali... hafai!...

Hivi watayarishaji wanapokea maoni? I dont think so, sidhani kama ni sawa na BBA au mashindano ya u-miss, nafikiri majaji akina SALIMU AHMED SALIM ndo wanapitia rekodi za hawa marais.
 
On the other hand, sijawahi kuona jambazi lijnaloiba na kuua lakini halina mazuri!..Jambazi linaloiba na kuwalisha wanawe, likajenga mahekalu huwa linapunguziwa adhabu kwa macho ya Mdanganyika hata kama kinachotakiwa kuhukumiwa ni Ujambazi wenyewe na sio nje ya hapo.

Hey kazi kweli kweli... yashafika huku!
 
Kuna rafiki yangu amenambia kwamba Africa haiwezi kubadilika kamwe kwa sababu ya mind set ya wananchi wake!...Yaani Ubadhilifu utazidi kuwepo na utapongezwa kwa vitendo pamoja na kwamba watu wanapinga kwa kauli zao. Wezi walioiba mabenki hupongezwa wanapojenga majumba na kutunza familia zao. NI sifa kubwa ya mwafrica kuwa jambazi linalotanua...
Huu Mfano wa Mkapa umenipa picha hasa kuona kwamba humu JF mnapongeza Mkapa kupewa tuzo kama hilo pamoja na kwamba mnaelewa mabaya alokufanyieni.
On the other hand, sijawahi kuona jambazi lijnaloiba na kuua lakini halina mazuri!..Jambazi linaloiba na kuwalisha wanawe, likajenga mahekalu huwa linapunguziwa adhabu kwa macho ya Mdanganyika hata kama kinachotakiwa kuhukumiwa ni Ujambazi wenyewe na sio nje ya hapo.
Yes, sasa nakubali kuwa Africa ina wakati mgumu sana na pengine yawezekana usia mzuri kwetu ni kujiunga na mafisadi maanake mwisho wa yote bado utapewa sifa kwa vitendo viovu vilivyoonyesha mafanikio kidogo.

Mwafrika wa Kike mimi naomba hiyo address ya hao watayarishaji nitapeleka tuhuma zote hizi zinazomkumba huyu Mkapa!
Ionekane roho mbaya potelea mbali... hafai!...

Kaka Mkandara unaweza kuwapata hawa jamaa wa Mo Foundation kwa namba zifuatazo;
+ 44 207404 5344.
+ 44 798443 3486.
+ 44 (0)207 2421 6143
Au watafute kwa e-mail info@moibrahimfoundation.org au Mwandikie huyu jamaa hapo chini ambaye ndiye Mratibu wa shughuli zote huko London robert.watkinson@portlandpr.co.uk Jamaa wanachaguliwa Jumatatu,kwa maana hiyo taarifa zozote ziingie huko mapema.
 
Mimi nadhani ya kuwa kuna haja ya kuangalia - je ufisadi wa Mkapa - can it be proved? Amewahi kupelekwa mahakamani? otherwise it's just gossip mongering. Mi nadhani hata Chissano atakuwa hajakubalika na watu wote Msumbiji! So, let us be more objective, hate or love the person, this award will be decided by facts and figures. Lakini kama mtawaandikia kwa kutuma facts kwamba aliiba this much na kupeleka to this account etc, basi inaweza ika-matter.
Tuelekeze nguvu zetu kwenye masuala ambayo yanaweza kuzaa matunda, not waste energy. Whoever wins from Africa hata kuwa perfect! Awe Chissano au Mkapa or whoever! Let us change what we can as we cannot undo the past. I think that Mo Ibrahim is just trying to buy influence in African countries with his award! If it is in his interest atampa hata Bashir wa Sudan! Ni hela yake, he can do what he wants!
 
BMW ana nafuu kubwa saana kimatendo kuliko marais wengi kwenye hiyo orodha.Na pia alijijengea heshima kedekede mbele ya mataifa makubwa na watu maarufu kama akina Kofi.Japo huku kwetu ameonekana kuchafua record yake,Bado anaungwa mkono na anaweza kubeba hiyo tuzo
 
Susuviri,
It just a matter of time....
Hata Hitler na Idd Amin walikufa bila kufikishwa mahamakani. Kisha kama nilivyosema sisi Wadanganyika (waafrika) wenyewe tunakuwa mawakili wa wahalifu ambao wametufanyia sisi mabaya! Ajabu ya Mwafrika maanake hata Hitler alionmekana mbaya kwa kuwafanyia watu wa nje ama wa kuja na alipendwa sana na raia wake. Tofauti ya mwafrika tunamkumbatia yule aliyetunyonga...Urithi ulotokana na Utumwa! Na yawezekana kweli sisi Waafrika tuna low IQ kulingana na wataalam.

Mjomba ebu tushtue kidogo, Ulitegemea kweli Mkapa afikishwe mahakamani wakati analindwa na KATIBA?...How can you prove nje ya mahakama kama sio vitu tunavyoviona kwa macho yetu. Nambie wewe atafikishwa vipi mahakamani nje ya katiba kama sio kuomba yasiyowezekana. Unauliza watu wasiokuwa wanasayansi kama wanaweza kuprove jua linalowaka kuwa ni JUA sio sayari nyingineyo!

Masatu,
Ndugu yangu ebu fikiria kitu kimoja hapa. Mkapa anatakiwa kupewa tuzo kama kiongozi BORA AFRICA!...yaani kweli tunaweza kusimama na kutetea mtu huyu kupokea tuzo hilo hali sisi wenyewe tunatafuta njia za kumfikisha mahakamani?...Kisha basi tunasifu kwa sababu kaukuza uchumi wa nchi yetu. Uchumi ambao hakuna hata Mdanganyika mmoja anaweza kutuonyesha kwa ushahidi huo huo zaidi ya takwimu zilkizotolewa na Utawala wake. What if there was nothing ktk federal reserve...
Huyu rais kafanya Biashara akiwa IKULU! hii pekee inaweza mwondoa ktk contenders lakini Wadanganyika mnaamua kulifumbia macho kama vile ni kitu cha kawaida!..
Mjomba najua wewe CCM lakini please simama kama walivyosimama akina Butiku, Mwinyi, Malecela, Ulimwengu kukemea UONGOZI mbaya.. iwe Mkapa ama yeyote yule ambaye atakiuka misingi ya UONGOZI.

Mwawado,
Shukran sana! ninafanya kweli...
 
Licha ya mapungufu fulanifulani tena madogo aliyoonesha wakati wa uongozi wake, ninaamini Mkapa aliitumikia nchi hii kwa uadilifu wa kupigiwa mfano (hasa kama atalinganishwa na viongozi wengine wa Afrika), na anastahili kutuzwa si tu na huo mpango wa Mo Ibrahim, bali pia hata sisi watanzania tunapaswa kumuenzi. Yes, Mkapa for the prize.

Ni mapungufu gani hayo madogo madogo?
 
Ni mapungufu gani hayo madogo madogo?

Kwa hakika Mkapa akilinganishwa na viongozi wengine wa Afrika (ambao wote pamoja naye wana madhambi fulani fulani), bado mzigo wake wa dhambi utakuwa mdogo sana ukilinganisha na wenzake, hii ndiyo maana yangu ninaposema mapungufu yake ni madogo.

Na kama kila mwaka huyu tajiri atafanikiwa kutusaidia kumzawadia kiongozi mwenye dhambi chache kuliko wenzake, labda kuna siku (as time tends to infinity) tutampata kiongozi asiyekuwa na dhambi hata moja!
 
Back
Top Bottom