Kampeni dhidi ya Mkapa asishinde Tuzo ya uongozi bora

Kampeni dhidi ya Mkapa asishinde Tuzo ya uongozi bora

Kithuku,
Ningekuelewa kama mfano wako ungekuwa unahusu mtoto wa shule kupewa zawadi kwa kuwa wa kwanza bila ya kuiba mtihani au kuangalizia. Hapa tunazungumzia mtoto wa shule kufaulu mtihani na kuwa kwanza bila njia za ujanjaujanja.Watanzania wanasema Mkapa kaangalizia kwenye mtihani hivyo hastahili hiyo tunzo. Kuiba mtihani na kuangalizia ni makosa katika kum-qualify mwanafuzi katika ushindi. Hatutaki kuambiwa eti Mkapa ni bora kwa kuwa yeye amekuwa wa kwanza ingawa aliangalizia mtihani tu, lakini hakuiba mtihani ukilinganisha na wengine walioiba mtihani. Hapa kama hakuna mshindi halali mwaka upite kapa.
 
Kithuku,
HJuwezi kusema Mkapa akilinganishwa na marais wengine hali hujui kabisa hali ya UONGOZI wa hao marais wengine.
Unachotumia kitu gani wewe kupima Uongozi bora.
Mbali na wizi wake akiwa Ikulu , katika Utawala wa Mkapa kumetokea mauaji ya viongozi na wananchi ndani ya nchi hii jambo ambalo ni nchi chache sana ktk Afrika zimekuwa na migogoro ya ndani. Mkapa kaua wapinzani kuliko hata Nyerere alowaweka jela!
Ama na wewe umekuwa kama wazungu wanaofikiria kuwa Afrika ina chini 4 tu. South, west, East na North Africa.
 
Mbali na wizi wake akiwa Ikulu , katika Utawala wa Mkapa kumetokea mauaji ya viongozi na wananchi ndani ya nchi hii jambo ambalo ni nchi chache sana ktk Afrika zimekuwa na migogoro ya ndani. Mkapa kaua wapinzani kuliko hata Nyerere alowaweka jela

Mkuu Bob,

Hii ndio kumkoma nyani hasa giladi, hatuiwezi kuwa distarcted na tuzo, apate salama, lakini tuhuma zipo plae pale mpaka atakapozijibu!

SALUTE MKUU!
 
Kithuku issue hapa ni kumlinganisha Mkapa na marais wengine au kuwalinganisha marais wa Africa na vigezo vyao? Kama vigezo vya scale zao ni 9marks na Mkapa ndo kaongoza kwa kupata 5,bado haja qualify.
 
Nyangumi,
Hoja yako ya kuangalizia ama kuiba mtihani ni nzito, na kama hiyo ipo pasi shaka, pasi tuwapelekee wachambue.Hiyo hata kufutiwa ushindi ni sawa, lakini tuwe na hoja zinazothibitika kihalisia (objectively verifiable), vinginevyo mambo ya kuoneana kijicho yanaweza yakatawala mchakato mzima.

Mkandara,
Nakubaliana nawe kwamba ulinganisho wa haki baina ya BWM na marais wengine wa Afrika tunaweza kuufanya iwapo tu tunazo taarifa za kutosha kuhusu hao wengine. Sisi tunazo nyingi sana za huyu wa kwetu na kidogo tu za hao wengine. Nao raia wa nchi hizo nyingine wana habari nyingi sana za viongozi wao, na kidogo tu za huyu wa kwetu. Nadhani hali hizi mbili zinakatana. Hata huyo rais atakayeibuka na tuzo hiyo usidhani atakuwa anakubalika na raia wote wa nchi yake. Si ajabu saa hizi ninapochapa post hii wapo wengine wengi tu wa nchi nyingine wanabonyeza keyboard kuelezea jinsi marais wao wastaafu wasivyofaa kwa tuzo hizo, na mmoja wapo ni huyo atakayeshinda. Alisema Bwana Yesu "Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na nyumbani kwake mwenyewe". Simaanishi Mkapa ni nabii, la hasha, lakini nachukua msemo huu kwa muktadha wa hoja iliyoko mbele yetu, kwamba si ajabu tukamwona Mkapa hafai kwa tuzo hiyo, kumbe wapo wa nje ya nyumba yetu wanaoona ndiye hasa anayefaa.
 
Kithuku issue hapa ni kumlinganisha Mkapa na marais wengine au kuwalinganisha marais wa Africa na vigezo vyao? Kama vigezo vya scale zao ni 9marks na Mkapa ndo kaongoza kwa kupata 5,bado haja qualify.

Hii pia ni hoja muhimu sana. Kama vigezo vipo, na vina points, na kuna passmarks, inawezekana kabisa likawepo kundi la waliofaulu na miongoni mwao akawepo aliyefaulu kuliko wengine, akapata tuzo. Kama hakuna aliyefaulu basi inakuwa hakuna tuzo mwaka huo. Lakini sidhani kama huyu mwandaaji atakubali kuambiwa kitu kama hicho, nadhani amepania kabisa kumzawadia mmojawapo. So wakifeli wote, watatafuta the lesser devil!
 
Na kama Mkapa ndo atashinda katika hiyo lesser devils list,basi Africa tusitegemee kuendelea.
 
Kithuku,.
Mjomba hata sijakuelewa kabisa hapo juu. Unaposema sisi tuna taarifa chache kuhusu marais wa nchi nyingine ndivyo wao wasivyokuwa na taarifa za rais wetu?... hapa unalenga kusema nini maanake tunaoandika humu ni sisi Wadanganyika. Sijamwona mtu wa nje akizungumzia kuhusu rais wetu ama kumpongeza rais wao dhidi ya Mkapa. Sisi wenyewe alotukandamiza ndio wa kwanza kuinua mikono kumpa pongezi, na hoja yangu imekuwa ktk sura hiyo.

Nakuhakikishia hata majirani zetu Kenya na Uganda ukiwauliza kuhusu marais watatu yaani M7, Kibaki na Mkapa ama hata tukiongeza huyo wa Rwanda.. Mkapa atachukua nafasi ya mwisho kutokana na hili somo la UONGOZI bora... ukizungumzia maendeleo hata Rwanda leo wako mbele yetu acha hizo Uganda na Kenya. Ukizungumzia usalama nadhani Tanzania tumekuwa na matukio mazito ya kisiasa wakati wa Mkapa kuliko nchi jirani na ushahidi upo dhahiri ktk chaguzi zote zilizotokea yaani mwaka 1995 na 2000.
Sasa ni kipimo kipi unachotumia wewe kumpa pongezi hizi huyu Mkapa...
 
Jamani,

Kwani tumechelewa kuandaa petition dhidi ya Mkapa? Ninadhani tuki-sign petition inaweza saidia kumbomoa huyu Mkapa.

Ni wazo tu, sijui mnaonaje?
 
Mkandara,
taratibu kaka...huwezi kuwalinganisha Maraisi Museveni na Kagame, na huyu wa kwetu Mkapa. Hao wa wenzetu mikono yao inachirizika damu ya wananchi wao na ile ya Wacongo.

Hata kimaadili huwezi kumlinganisha Museveni na Mkapa. Museveni ana kashfa nyingi tu ktk manunuzi ya vifaa vya kijeshi, na ndugu zake kushiriki ktk uporaji wa madini DRC. Uhuni wa Museveni umesababisha Uganda kuhukumiwa ktk mahakama ya kimataifa ya the Hague.

Kuhusu hao wapinzani, Mkapa amemuua nani jamani? Au unazungumzia mauaji yaliyotokea Pemba. Hivi unafahamu kwamba wakati wa mauaji yale Mkapa alikuwa nje ya nchi?

Jamani Mkapa ana matatizo yake TUHUMA za wizi wa hapa na pale. Wizi wenyewe ni wa kisomi wa kutumia kalamu na mikataba. Mkapa hana tuhuma za kuiba kwa kutumia bunduki,mizinga,vifaru na madege ya kivita, kama Kagame na Museveni mnaojaribu kuwatukuza hapa.

NB:
Hivi mmefikia kudai hali ya Usalama na Kisiasa ni shwari Rwanda,Uganda,na Kenya, kuliko Tanzania?
 
Hata ya Mkapa inachirizika damu! au umesahau?
 
Mkuu naona umesahau mauji ya Pemba na Mwembe chai kwani zile damu zilikuwa za kondoo??

Mkapa utawala wake na mikono yake ina nuka damu pia!
 
Jokakuu,
Kila nitakaye mtaja utaniuliza ushahidi kwa hiyo sidhani kama kuna haja ya kufika huko.
Ukiachana na mauaji ya Pemba ama Mwembechai unajua kuna viongozi wangapi waliondoka kwa njia za kutatanisha baada ya kutofautiana na Mkapa kisiasa. Mmoja wao akiwa Dr. Omar Juma......makamu wa rais, sasa kama ni uchawi mtanishika mie lakini list is huge!. Nakuomba uelewe kitu kimoja sio lazima vifo viwe na mkono wake ila mauaji yametokea chini ya Utawala wake. Good governance haina maana kayafanya yeye kwa mkono wake. Leo hii tunamlaumu JK kwa sababu ya matendo ya viongozi wengine chini yake.

Hata hivyo hilo tuzo nimegundua kuwa ni mbinu ya mwekeshaji Mo Ibrahim ambaye ni mmliki mkubwa wa Celtel ambaye kwa ujanja wake aliweza kuingia nchini na kamba kubwa kumwajili Mtanzania kama CEO. Na target yao kubwa ni kuuwa kabisa shirika la simu la taifa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwa msaada mkubwa wa huyo Ben Mkapa..
Kwa hiyo sintashangaa kabisa kama Mkapa atachukua hilo tuzo pamoja na kwamba malalamiko yangu nimeyawakilisha. Na zaidi ya hapo mawazo yangu yanachukuliwa kama mawazo ya mtu mmoja tu...
 
Kuhusu hao wapinzani, Mkapa amemuua nani jamani? Au unazungumzia mauaji yaliyotokea Pemba. Hivi unafahamu kwamba wakati wa mauaji yale Mkapa alikuwa nje ya nchi?

Wakati haya mauaji yanatokea alikuwa rais wa nchi. Hata kama alikuwa nje ya nchi, lakini he was briefed. You must have heard of Presidential Daily Briefing (PDB). There is no handing responsibility to someone else, and the fact that the president has to make the decisions and accept the ultimate responsibility for those decisions.

Jamani Mkapa ana matatizo yake TUHUMA za wizi wa hapa na pale. Wizi wenyewe ni wa kisomi wa kutumia kalamu na mikataba. Mkapa hana tuhuma za kuiba kwa kutumia bunduki,mizinga,vifaru na madege ya kivita, kama Kagame na Museveni mnaojaribu kuwatukuza hapa.

Ama kweli ukipenda hata chongo huita kengeza. Wizi wa kisomi ndiyo wizi gani na unaahueni gani wakati athari za wizi ni zile zile? Kibaya zaidi, huu wizi unatukana intelligence za watu na ku-undermine their judgement. Matokeo ya wizi wa Mkapa ni sisi waafrika kutukanwa na kudharauliwa kuwa tuna low IQ. Na hata ukienda mbele ya sheria Mkapa ni mwizi tu. Tena huu wizi wa Mkapa mbaya zaidi kuliko wa jambazi litumialo bunduki.

Hakuna wizi wa kisomi, na usomi wa mtu does not justify wizi wa aina yoyote. Wizi ni wizi tu.
 
Wizi wizi tu, hakuna wizi ulio na afadhali!
 
Jokakuu,
Kila nitakaye mtaja utaniuliza ushahidi kwa hiyo sidhani kama kuna haja ya kufika huko.
Ukiachana na mauaji ya Pemba ama Mwembechai unajua kuna viongozi wangapi waliondoka kwa njia za kutatanisha baada ya kutofautiana na Mkapa kisiasa. Mmoja wao akiwa Dr. Omar Juma......makamu wa rais, sasa kama ni uchawi mtanishika mie lakini list is huge!. Nakuomba uelewe kitu kimoja sio lazima vifo viwe na mkono wake ila mauaji yametokea chini ya Utawala wake. Good governance haina maana kayafanya yeye kwa mkono wake. Leo hii tunamlaumu JK kwa sababu ya matendo ya viongozi wengine chini yake.

Hata hivyo hilo tuzo nimegundua kuwa ni mbinu ya mwekeshaji Mo Ibrahim ambaye ni mmliki mkubwa wa Celtel ambaye kwa ujanja wake aliweza kuingia nchini na kamba kubwa kumwajili Mtanzania kama CEO. Na target yao kubwa ni kuuwa kabisa shirika la simu la taifa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwa msaada mkubwa wa huyo Ben Mkapa.. Kwa hiyo sintashangaa kabisa kama Mkapa atachukua hilo tuzo pamoja na kwamba malalamiko yangu nimeyawakilisha. Na zaidi ya hapo mawazo yangu yanachukuliwa kama mawazo ya mtu mmoja tu...

Heshima mbele Mkuu, ndo maana mi nilisema kabla hatujamjadili mkapa, hebu tuangalie thana nzima ya hiyo zawadi, kwa nini ije wakati huu, na was it the best alternative to use that money? nadhani tukiweza kufikia muafaka hapo tutaweza kujua nini hasa kipo nyuma ya hii tuzo!
 
Masatu,
Ndugu yangu ebu fikiria kitu kimoja hapa. Mkapa anatakiwa kupewa tuzo kama kiongozi BORA AFRICA!...yaani kweli tunaweza kusimama na kutetea mtu huyu kupokea tuzo hilo hali sisi wenyewe tunatafuta njia za kumfikisha mahakamani?...Kisha basi tunasifu kwa sababu kaukuza uchumi wa nchi yetu. Uchumi ambao hakuna hata Mdanganyika mmoja anaweza kutuonyesha kwa ushahidi huo huo zaidi ya takwimu zilkizotolewa na Utawala wake. What if there was nothing ktk federal reserve...
Huyu rais kafanya Biashara akiwa IKULU! hii pekee inaweza mwondoa ktk contenders lakini Wadanganyika mnaamua kulifumbia macho kama vile ni kitu cha kawaida!..
Mjomba najua wewe CCM lakini please simama kama walivyosimama akina Butiku, Mwinyi, Malecela, Ulimwengu kukemea UONGOZI mbaya.. iwe Mkapa ama yeyote yule ambaye atakiuka misingi ya UONGOZI.

Mkuu naona ushanitafutia chama haya labda nikubaliane na uchaguzi wako....

Ukiachana na mauaji ya Pemba ama Mwembechai unajua kuna viongozi wangapi waliondoka kwa njia za kutatanisha baada ya kutofautiana na Mkapa kisiasa. Mmoja wao akiwa Dr. Omar Juma......makamu wa rais, sasa kama ni uchawi mtanishika mie lakini list is huge!. Nakuomba uelewe kitu kimoja sio lazima vifo viwe na mkono wake ila mauaji yametokea chini ya Utawala wake. Good governance haina maana kayafanya yeye kwa mkono wake. Leo hii tunamlaumu JK kwa sababu ya matendo ya viongozi wengine chini yake.

Mkandara, Mkandara acha kutufanya watoto wadogo tunakuheshimu sana huu upupu mwingine katafute mahala pa kuupeleka sio hapa
 
Masatu,
Nilijua tu mjomba lazima uje inapofikia sehemu kama hizi...
Cha ajabu ni kwamba wewe huandiki hoja yoyote ila hutafuta mahala unapofikiria kuna walakin kimawazo lakini huna side ya pili ya picha hiyo. Ndio yaleyale ulotaka ushahidi kuhusu Mafisadi hadi Butiku na mwinyi waliposema ukaingia mitini... Giiii! mbona usiwaulize wao pia ushahidi ama waje na maneno ya kiutu uzima?
Sasa hapa unasema nisiwafanye watoto wadogo, wewe unaelewa ukweli upi wa kiutu uzima.
Mjomba kuwa unaandika basi mawazo yako wewe yanayopingana na wengine at least tunaweza kuangalia ukweli uko wapi lakini hii habari ya maandishi mekundu toka kwa wengine haielezi kitu chochote.
 
Mkandara, ninayo andika ni mawazo yangu lau unafikiri si ya kwangu then siwezi kuku lazimisha.

Hili la Mkapa kuhusika na kifo cha marehemu Makamu wa Rais Dr Omar Juma wala sina haja ya kutaka ushahidi ( after-all huna ) nitakachokuomba hapa ni tupatie basi walau motives behind Mkapa kuhusika na kifo kile thats ili iwe nini na kwa faida gani?

Kuhusu Butiku mkuu unataka kutulazimisha tuamini kuwa kila alisemalo Butiku ( for that matter kila wasemalo wanasiasa wastaafu) ni msahafu na sahihi na tukubaliane nalo? Butiku katoa mawazo yake kama Mtanzania, kama unavyofanya wewe kama ninavyofanya mimi whats big deal abt it? Unadai nimeingia mitini mkuu nipo tele, sina tu forum ya kujibizana na Butiku kama ninavyobishana na wewe hapa.

Once again mkuu unachemsha...
 
Back
Top Bottom