Kampeni: Kiba rudisha tuzo mbili ulizopewa (sio ulizoshinda)

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Kama Siti alivua taji la Miss Tanzania baada ya kuonekana kuna udanganyifu kwenye wasifu wake .

Na wewe tuzo ya utunzi bora mrudishie Barnaba, tuzo ya utumbuizaji bora mpelekee Diamond.

Hizo tuzo umepewa sio kwa sababu ya uwezo wako,ila kwa sababu ya maamuzi wa mabepari wa mziki Tanzania.

Hebu jiulize umefanya utumbuizaji gani kwa mwaka jana had ustahili tuzo ya mtumbuizaji bora ?

Umetunga nyimbo gani za maana hadi ustahili tuzo ya mtunzi bora.

Rudisha tuzo ulizopendelewa ili kujenga heshima yako ,pambana kwa kazi sio fitna.

Mimi ni shabiki wako ila upepo unaovumishwa haufanini na kiwango chako .
 
idawa

Kiba hajapewa tuzo wapigaji kura ndo walipendekeza hvyo.....mimi nafikir kampen yako ungeielekeza kwa waandaji wa KTMA wabadilishe mfumo wa upigaj kura na sio kuleta bla blaa hapa watanzania wamemchagua mm nafikir tatzo ni mfumo tu,, unasema kiba katunga nyimbo gan za maaana???

Hata kama una chuki sio kiivyo mkuu jitahid kuzuia mihemko yako ili ujadili hoja kwa kubalance hivi nyimbo ya mwana unaiona kwa waswas nini? Ckatai barnaba ni mtunz mzur sana ila pia kutumia kiswanglish nayo tatizo mwana mwanzo had mwisho kiswahil kuntu pia barbana kura hazikutosha vp kuhus zle 7 za mond alistahil zote?? Au kiba tu ndo kosa limefanyika?
 
Last edited by a moderator:
Tasnia ya filamu na muziki wa tanzania umeshavurugwa...
Watu wenye akili timamu wanaongozwa na mtu mmoja kufanya maamuzi...
Hivi Wema ana nguvu gani hadi amewachota akili watu wenye degree zao kufanya maamuzi anayotaka yeye??...
 
Tasnia ya filamu na muziki wa tanzania umeshavurugwa...
Watu wenye akili timamu wanaongozwa na mtu mmoja kufanya maamuzi...
Hivi Wema ana nguvu gani hadi amewachota akili watu wenye degree zao kufanya maamuzi anayotaka yeye??...

Wema na wenzake ni mamburura tu .
 
Tasnia ya filamu na muziki wa tanzania umeshavurugwa...
Watu wenye akili timamu wanaongozwa na mtu mmoja kufanya maamuzi...
Hivi Wema ana nguvu gani hadi amewachota akili watu wenye degree zao kufanya maamuzi anayotaka yeye??...

Kwani wema ndie anayepiga kura kwenye izo tuzo ?

Anawajambisha na nyinyi mnaingia chaka
 
Tujitafakari kwanza woote mnaonung'unika kuhusu kiba je mlimpigia diamond kura au no blaablaa tu!!!😌😌
 
Ha haaa kiba anatakiwa arudishe tuzo zoteeee
Hakustahil hata moja
 
Kwikwikwiiiiiiii chukueni mkeka mkae kabisa maana mtangoja sanaaaaaa
 

umeongea points...

washabiki hao wa barnaba je?walipiga kura
mi juzi nimeshuhudia vijana wanabishana kuhusu hilo

wawili wanasema wamempigia kura aly k,wale wengine hawakumpa barnaba wala yoyote!!
hivi angeshindaje bila wao kupiga kura..?!!

jamani aly ameshinda kwa kura!

huyo wema sepetu mnaemtukana kila siku!!

nyie humu eidha ni wazazi au wazazi watarajiwa!!

mtakuja kukuta watoto wenu wameharibikiwa mkashangaa sana kujifanya mnajua kuwalea kumbe kuna mtu ulimsononesha siku za nyuma
hvyo dhambi ya kumtusi na kumkashifu mtoto wa mwanaume au mwanamke mwenzio itakutafuna kupitia kwa wanao
 
Kweli jsmani hizo tuzo si zake wampe barnaba na diamond nilijiuliza sana inakuwaje ametunga nini kimasomaso tu ndo mtunzi bor nampenda kiba lkn tuwe wa kweli nimeona shoo zake kawaida sana hajamfikia diamond tena ule wimbo wa mwana dar ndio hata video haindani na alichoimba au ile ndo performance
 
Tuzo moja ya mtunzi bora ni ya Christian Bella na nyimbo ya nani kama mama, tuzo ya mtumbuizaji bora ni ya diamond. Period
 

Kwel kabisa chuki zisitufanye tupoteze utu, kitu chochote kinachoamuliwa kwa kura za watu kura nying ndo hushinda hata kama tukishindanisha ndege na baiskel upi usafir wa haraka na kura nying zikaenda kwa baiskel..baiskel ndo imeshinda kwa kura mimi nadhan tatizo liko kwenye mfumo na vigezo vya washirik kwenye categories, sion sabab ya kumlaum kiba sasa kama aliwekwa kwenye categories hzo mbn hamkuandamana atolewe kabla ya cku ya tuzo?

Au baada ya kushinda ndo walijua alikuwa kwenye hzo categories? Watanzania bhana na tusipo angalia hata kwenye uchaguz mkuu wa Rais tutamchagua mtu akishashinda tutakuja tena kulalamika na kuandamana kwamba hafai badala ya kuandamana au kupinga kipind hik cha kuteuliwa na vyama muda wa kulalamikia tume ya uchaguz ni huu na sio baada ya uchaguz bt sory kwa kuingiza siasa hapa ila ni mfano wa Watz tulivyo!
 

Kuna majaji wanaamua mwishoni nani apewe.
 

Andika tuone zile 7 kwanini hakustahili ueleweke na sie wadau vizuri, andika kwa kila moja unaona kwanini.
 

ndo maana ccm inaongoza miaka yote
maana wana mtaji wao wa wapiga kura...wazee wapo wapiga kura yani humwambii kitu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…