Uchaguzi 2020 Kampeni meneja wa CCM 2020 ni nani? Nayaona makosa ya kiufundi mengi sana

Uchaguzi 2020 Kampeni meneja wa CCM 2020 ni nani? Nayaona makosa ya kiufundi mengi sana

Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
892
Reaction score
683
Habari wakuu,

Kampeni meneja wa CCM uchaguzi huu ni nani? Nayaona makosa mengi mno kwenye uchaguzi kipindi hiki.

Kwa maeneo waliyofanya kampeni mpaka sasa hivi, watu wameshasahau kilisemwa nini.

CCM huwa wana mpangilio wa kampeni zake kwa miaka yote, huko nyuma imekuwa cha kushangaza kuna majimbo eti mengine weekend ya Septemba 26 ndio yamezindua kampeni rasmi ni maajabu.

Kampeni inayoongozwa na Mh Mgombea wa CCM msemaji Mkuu ni Kampeni Meneja ambaye hayupo hii inafanya kampeni kwenda kinyume na wagombea kuongea watakavyo hawagawani majukumu nani aseme nini na nani afukie wapi

Kuna haja sasa team iliyofanya kampeni 2015 itafutwe kwa nguvu ili waje wafukie mashimo haya.

Asante
 
eti ndio huyu mwenye miwani na kitambi
119475389_715314762531488_7085147251043382146_n.jpg
 
Kwa kifupi Bashiru, Pole pole na Magufuli sio wanasiasa hata kidogo, wameparamia hiyo fani. Mimi niko upinzani Ila Nape, mzee Makamba na Kinana walikuwa wanasiasa ndani ya CCM. Asikudanye mtu siasa ni fitina.

Habari ya ununuzi wa ndege, SGR, barabara na ujenzi wa mahospitali ni wajibu wa serikali hakuna jipya hapo. CCM inahitaji msaada ili kupambana na TL. Vinginevyo kuna ujio wa KANU Tanzania.
 
Mkuu
CCM imeshakufa kwa sasa kampeni meneja ni yule yule ambaye amewapola chama chao kina Mangula japo yupo kama koti limetundikwa kwenye kisiki, Membe , Mzee makamba, Nape japo ni mchumia tumbo,
Endelea kuwashauri labda wanaweza wakampa Pascal Mayalla au Musiba
 
Kwa kifupi Bashiru, Pole pole na magufuli Sio wanasiasa hata kidogo wameparamia huyo fani .mimi Niko upinzani Ila Nape,mzee makamba na kinana walikuwa wanasiasa ndani ya CCM. Asikudanye mtu siasa ni fitina.
Habari ya ununuzi wa ndege, SGR , barabara na ujenzi wa mahospitali ni wajibu wa serikali hakuna jipya hapo. CCM unahitaji msaada ili kupambana na TL. Vinginevyo Kuna ujio wa KANU tanzania


Kabisa njia nyeupe kabisaaaaa, yaani jukwaani wanashangaza sana kila mtu anasema hovyo. Hawajipangi mtiririko wa wasemaji hawapo wamebaki kusema sema kwenye mitandao tu.
 
Habari wakuu,

Kampeni meneja wa CCM uchaguzi huu ni nani? Nayaona makosa mengi mno kwenye uchaguzi kipindi hiki

Kwa maeneo waliyofanya kampeni Mpk sasa hivi watu wameshasahau kilisemwa nini

Ccm huwa wanampangilio wa kampeni zake kwa Miaka yote huko nyuma imekuwa cha kushangaza kuna majimbo eti mengine weekend ya 26 ndo yamezindua kampeni rasmi ni maajabu

Kampeni iyoongozwa na Mh Mgombea wa CCM msemaji Mkuu ni Kampeni Meneja ambaye hayupo hii inafanya kampeni kwenda kinyume na wagombea kuongea watakavyo hawagawani majukumu nani aseme nini na nani afukie wapi

Kuna haja sasa team iliyofanya kampeni 2015 itafutwe kwa nguvu ili waje wafukie mashimo haya

Asante
Acha wafe mkuu haya majizi unayatakia mema ya nini?
 
Habari wakuu,

Kampeni meneja wa CCM uchaguzi huu ni nani? Nayaona makosa mengi mno kwenye uchaguzi kipindi hiki.

Kwa maeneo waliyofanya kampeni mpaka sasa hivi, watu wameshasahau kilisemwa nini.

CCM huwa wana mpangilio wa kampeni zake kwa miaka yote, huko nyuma imekuwa cha kushangaza kuna majimbo eti mengine weekend waWaWya 26 ndio yamezindua kampeni rasmi ni maajabu.

Kampeni inayoongozwa na Mh Mgombea wa CCM msemaji Mkuu ni Kampeni Meneja ambaye hayupo hii inafanya kampeni kwenda kinyume na wagombea kuongea watakavyo hawagawani majukumu nani aseme nini na nani afukie wapi

Kuna haja sasa team iliyofanya kampeni 2015 itafutwe kwa nguvu ili waje wafukie mashimo haya.

Asante
Wanatafutana kwa tochi na hawaonani kwa vumbi wanalotimuliwa kwa maneno machache tu,Uhuru,haki na maendeleo,itafika mahali hats mchana wajua Kali hawata weza kuonana.
 
Chadema tuwanasikia wakituambia
"Uhuru haki na maendeleo ya watu"

Ccm sijui Wana kauli mbiu ipi?
Juzi nilimsikiliza Dr. Marcos Albanie akiwa mwanza (ambae alijitambulisha kama mshauri wa Tundu Lissu) alisema kwa wiki tatu hizi za mwanzo CCM wamekuwa kwenye defensive position, sasa kinachofata awamu ya pili wao kama chadema wanaenda kupasua kichwa cha ccm.
 
Kwani ccm hadi iandae kampeni meneja wa nini? Kwani kunaupinzani Tanzania mwaka huu mpaka ccm itumie nguvu kubwa kupambana?? Sisi tunajua mpinzani wetu ni mabeberu. Ila tutawagalagaza asubuhi saana.
Wewe una banduliwa jogoo la mwanzo alfajiri ukiamka LISU kashatangaazwa na wananchi wanashangiria

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom