mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 11,005
- 20,805
Mama mia!!! Tumekwisha..Taarifa inaonyesha kwamba Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imepitisha majina mawili ya kuwania Uenyekiti wa Simba , huku wagombea wengine wakienguliwa (sifahamu vigezo vilivyotumika ) , waliopitishwa ni Mangungu na Juma Nkamia , maana yake ni kwamba kati ya wawili hawa mmojawapo atakuwa Mwenyekiti wa Simba.
Simfahamu Mangungu kwahiyo sitamjadili .
Bali Juma Nkamia hana uwezo na wala hajawahi kuwa na uwezo wa kuongoza timu kubwa kama Simba , Nkamia ni mtu aliyejaa ubinafsi asiyeamini katika umoja , ni mtu wa majungu ambaye akipewa nafasi hiyo ataigawa Simba mapande mapande , hapaswi kupewa cheo kikubwa kama Uenyekiti wa Simba , Nkamia amekuwa kiongozi wa chini wa Simba miaka iliyopita , lakini tabia yake ya kuropokaropoka ilimfanya akang'olewa.
Pamoja na kuwa Mbunge katika bunge lililopita , lakini Nkamia hakuwa na ushawishi wowote ndani na nje ya bunge , hoja zake bungeni zilizimwa kama mshumaa jangwani , huku wananchi wa Jimbo lake wakiongoza kwa umasikini nchini Tanzania , mtu kama huyu hafai kuongoza timu ya Kimataifa kama Simba
Itaendelea...
Hivi huyo Juma Nkamia ana shughuli gani ya kumuingizia kipato zaidi ya hicho anachogombea?
Tunafahamu fika kwamba mwenyekiti sio muajiriwa wa klabu,,
Hivyo basi ,,hatokuwa na mshahara kutoka simba.,na wala halipwi chochote.
Je? kama hana chanzo chochote cha pesa ,,
Anagombea hiyo nafasi aisaidie club au club ndy imsaidie yeye kutatua maisha yake?
Nasikia anaishi hotel miaka yote,,hata kiwanja hana,,
Sasa kiongozi kama huyo wa nn ktk club kubwa kama simba?
Ifikie kipindi tuchaguwe viongozi kwa uwezo wao wa kifedha,,na sio kufuga wabadhirifu ndani ya club.