Uchaguzi 2020 Kampeni yenye #Miaka5YaKazi inayoendeshwa na Msemaji Mkuu wa Serikali yadolola huko Twitter

Uchaguzi 2020 Kampeni yenye #Miaka5YaKazi inayoendeshwa na Msemaji Mkuu wa Serikali yadolola huko Twitter

Huwezi kuongelea afya bila
-madawa... basic
-Madakitari wakitaabika, mishahara duni
-Vitendea kazi agharabu basic duni au hakuna
Unazidi kujidhihirishia kuwa wewe hauko Sawa mkuu

Swali dogo tu hapo, unaleta dawa bila kuwa na Majengo ya kulaza na kuwatibia wagonjwa, utakuwa unafanya kazi ya kuwatembelea nyumbani kwao kuwatibu?

Ili madawa yaje, lazima kuwepo jengo maalumu la kuziweka dawa na eneo la kukutana na wagonjwa!

Vitu na watu ni na maji na samaki, elewa hivyo mkuu
 
Mkuu umenena vyema sana, ukweli wanaujua lkn wanapinga tu. Huwezi kuitwa nchi iliyoendelea kwa Sababu eti nchi ina chakula cha kutosha, eti kwa Sababu watu ni watanashati, eti kwa Sababu watu wana uhuru wa kuropoko bila mantiki, you will only be called a developed country, only if, una huduma nzuri za afya, maji, usafirishaji, elimu, umeme.

Maendeleo ya watu na vitu ya nakwenda pamoja huwezi kuacha kimoja kukiwa hoi bin taaban ukajisifu kuwa unaleta maendeleo kama ni hivo makaburu wangekuwa wana tawala afrika kusini hadi leo. Na msingi wa kwanza wa maendeleo ni watu kuwa huru kwanza bila hilo angalia Gaddafi ilikuwaje sababu ya watu kukosa uhuru wa kutoa mawazo yao. Nyerere alisema kwa vitendo kila anachoansiaha kilitanguliza neno uhuru mfano uhuru na Umoja, uhuru na kujitegemea au uhuru na maendeleo hapo alitaka kusimamia umoja, kujitegemea na maendeleo lakini angalia matumizi ya neno uhuru, ni kwasababu alifahamu kuwa uhuru ndo kila kitu vingine vinafuata.
 
Hebu soma ulichokiandika kwa umakini halafu jitafakari kama weye ni mzima kiakili.
Mkuu, kabla sijaandika nilitafakari sana tena zaidi ya sana kwahyo sioni haja ya kutafakari upya, Magufuli amejitahidi kufanya au kuboresha hayo yote niliyoyaandika, kwanza ieleweke sio kila sehemu magufuli Kama vizuri lkn huwezi ku-downgrade jitihada zake za kuleta maendeleo ya nchi na kuwafikishia wananchi huduma za msingi. Some leaders especially Lissu is preaching freedom wherever he stands, in reality no man/human is free (the principal of nature). We all bounded to natural laws that limit and guide us on everything. So as long you're under this circumstance you can't be all you want cause the nature itself will act against you at some point. Ni hivo tu mkuu
 
Kina Nyerere walij

Kina Nyerere walijenga miundo mbinu huku wakitoa huduma za kijamii tena bila malipo kuanzia elimu,afya,mabwawa ya umeme,Reli ya TAZARA na hata bomba la mafuta la TAZAMA.Haya yanayofanywa na awamu hii ya tano ni ukandamizaji wa raia/Wananchi kwa visingizio hafifu mno.Maisha yanaweza kusubiri/kusimama kwa muda gani ili ujenge miundo mbinu?Miradi hii imekuwa ikihubiriwa kwa miaka mitano na bado haiwezi kukamilika hata 2025,Watanzania waendelee kusubiri hadi wakati huo bila ajira,nyongeza za mishahara,kupandishwa vyeo,kulipa wakandarasi na madeni ya ndani na nje hadi baada ya 2025?CCM haya mawazo mnayatoa wapi?
Vipaumbele vyenu ni kuzindua kila kitu ikiwemo nyimbo za kampeni kabla ya kampeni yenyewe?Msajili amezibwa macho na masikio.Je,wakitaka kufanya hayo wapinzani watakuwa salama?
Hata hayo maendeleo ya watu hayawezi kuisha ni muendelezo tu sababu kila siku watu wanongezeka umri, watu wanazaliwa, wanamaliza vyuo, watu wanastaafu.

Maendeleo ya vitu huwa yanapita na baada ya muda unaweza kuhitaji kutokana na ongezeko la watu ndio maana baada ya muhimbili na ocean road kuelemewa zikajengwa temeke, amana na mwananyamala.
 
Lakini hakuacha watu wafukarike kwa kisingizio cha kujenga miundombinu alikuwa anajenga huku wafanyakazi wanaongezewa mishahara wastaafu wanalipwa mafao yao yakitokea maafa watu wanapewa chakula cha msaada kutoka nchi marafiki siyo kuwasimanga kwanza ni kujali watu sababu hayo maendeleo ni ya nini kama siyo ya hao watu.
Hata enzi za nyerere walikuwepo watu waliokuwa wanalalamika kama wewe. Japo wewe leo unasifia.
 
Wewe mpuuzi unaelewa Japan njia waliyopitia kufika hapo walipo?

Unafaham njia waliopita wote walioendelea?

1. Sera bora

2. Mikakati bora (strategies)

3. Discipline

Hebu jadili kila kimoja ukilinganisha na maendeleo ya Taifa letu

Hizo nchi za chini ziliboreshewa kwanza miundo mbinu. Leo hii mtu anaishi munich anafanya kazi berlin. Anapanda tu treni ya umeme.

Hizo nchi zina barabara za juu na chini ili kupunguza foleni watu wawahi kwenye shughuli za kiuchumi.

Hizo nchi zina huduma za afya kila mahali na huduma za maji na umeme wa uhakika ili watu wajiajiri na viwanda vitengeneze ajira.

Hiyo ni miundo mbinu.
 
Mkuu, kabla sijaandika nilitafakari sana tena zaidi ya sana kwahyo sioni haja ya kutafakari upya, Magufuli amejitahidi kufanya au kuboresha hayo yote niliyoyaandika, kwanza ieleweke sio kila sehemu magufuli Kama vizuri lkn huwezi ku-downgrade jitihada zake za kuleta maendeleo ya nchi na kuwafikishia wananchi huduma za msingi. Some leaders especially Lissu is preaching freedom wherever he stands, in reality no man/human is free (the principal of nature). We all bounded to natural laws that limit and guide us on everything. So as long you're under this circumstance you can't be all you want cause the nature itself will act against you at some point. Ni hivo tu mkuu
Umejitahidi kujikongoja na umekiri kwamba mjomba wako anafeli sehemu That's all!
 
Wewe mpuuzi unaelewa Japan njia waliyopitia kufika hapo walipo?

Unafaham njia waliopita wote walioendelea?

1. Sera bora

2. Mikakati bora (strategies)

3. Discipline

Hebu jadili kila kimoja ukilinganisha na maendeleo ya Taifa letu
Duh..we ni ke au me??

Sera bora ndio nini,discipline ndio nini, mikakati ndio nini?? Kwa hiyo ukifanya hivyo tayari maendeleo??
 
Unazidi kujidhihirishia kuwa wewe hauko Sawa mkuu

Swali dogo tu hapo, unaleta dawa bila kuwa na Majengo ya kulaza na kuwatibia wagonjwa, utakuwa unafanya kazi ya kuwatembelea nyumbani kwao kuwatibu?

Ili madawa yaje, lazima kuwepo jengo maalumu la kuziweka dawa na eneo la kukutana na wagonjwa!

Vitu na watu ni na maji na samaki, elewa hivyo mkuu

Vyote vinatakiwa kufanyika pamoja ndiyo maana kuna muda wa kuandaa mipango huwezi kupanga kujenga majengo tu bila kupanga kuongeza mishahara kwa wafanyakazi na kununua vifaa tiba sasa hayo majengo peke yake yatakuwa ya kazi gani watu si wataendelea kufa. Vyote hivyo vinalenga kuwaendeleza wananchi mmoja mmoja si vinginevyo. Sasa kama uwezezaji wa trion zaidi ya 100 na wananchi ndo hawa waliyo hoi bin taaban Kuna Faida gani ya hayo matumizi
 
Wewe mpuuzi unaelewa Japan njia waliyopitia kufika hapo walipo?

Unafaham njia waliopita wote walioendelea?

1. Sera bora

2. Mikakati bora (strategies)

3. Discipline

Hebu jadili kila kimoja ukilinganisha na maendeleo ya Taifa letu

Kama hivo kwenye kampeni wasiwe wanasema mkinichagua mimi nitaboresha mishahara yenu nitalipa wastaafu kwa wakati nitaboresha huduma za afya na maji. Wasema nitabana matumizi ya mishahara na malipo ya wastatafu huduma za maji na vifaa tiba ili tuweze kujenga kwanza miundombinu ambayo hatuna, ili wananchi waamuwe kama wachague huyo mtu au la. Sasa kuwapa matumaini halafu baada ya kuingia madarakani unasema siwezi kuongeza mishahara najenga flyover hapana siyo sawa
 
Vyote vinatakiwa kufanyika pamoja ndiyo maana kuna muda wa kuandaa mipango huwezi kupanga kujenga majengo tu bila kupanga kuongeza mishahara kwa wafanyakazi na kununua vifaa tiba sasa hayo majengo peke yake yatakuwa ya kazi gani watu si wataendelea kufa. Vyote hivyo vinalenga kuwaendeleza wananchi mmoja mmoja si vinginevyo. Sasa kama uwezezaji wa trion zaidi ya 100 na wananchi ndo hawa waliyo hoi bin taaban Kuna Faida gani ya hayo matumizi
Sasa umeanza kuitumia akili yako vema

Jiulize tena swali hili, wewe ukianza kujenga nyumba yako, Je utaweza kubaki kwenye matumizi yako ya awali kabla hujaanza kujenga?

Je, hutabana matumizi yako ya siku Kwa siku? Na je ukimaliza kujenga, maisha yako yatabaki hivyohivyo?

Sisi tulikoseaga tokea huko nyuma Sana, Jifunze Kwa Mungu Kwanza, Mungu hakumuumba Mwanadamu Kwanza, badala yake alimwekea Kwanza miundombinu yote wezeshi Ndiyo akamleta duniani, Wewe huwa unajifunza nini kwenye maisha yako?
 
Hivi maendeleo ni kondomu Hadi zitumike nguvu kubwa Sana kuwalazimisha watu kuyaona tangu ukoloni hatujawahi ona maendeleo yakinadiwa, vitu vilifanyika Tena vikubwwa na pasipotambo zozote.
Hapa ndo tofauti ya propaganda na Hali halisi
 
Mkuu nimekuelewa ni kweli maendeleo ya vitu na watu yanakwenda pamoja, lkn Usisahau hili mkuu kila mtu au serikali ina vipaumbele vyake, labda mm Ndio sijui, je mm Nikipata hela iwe ya kwangu niliyoivujia jasho mwenyewe au ya mkopo nitakimbilia kuwekeza kwenye nn (VITU) mfano Kama Sina uwanja nitanunua, Kama sina nyumba nitajenga, au kuwekeza sehemu nyingine inayoweza kuzalisha hela tena (Huo ni uwekezaji kwenye vitu), kiujumla kila mtu au serikali ina vipaumbele vyake as long Kama vitaleta manufaa badae acha afanye. Kwenye Uhuru mkuu, Kiasili mwanadamu hana uhuru kamili, fatilia hata tawala za enzi hizo, na hivyo Ndivyo asili ilivyo, no one will guarantee you total freedom 100% narudia tena hakuna.
Maendeleo ya watu na vitu ya nakwenda pamoja huwezi kuacha kimoja kukiwa hoi bin taaban ukajisifu kuwa unaleta maendeleo kama ni hivo makaburu wangekuwa wana tawala afrika kusini hadi leo. Na msingi wa kwanza wa maendeleo ni watu kuwa huru kwanza bila hilo angalia Gaddafi ilikuwaje sababu ya watu kukosa uhuru wa kutoa mawazo yao. Nyerere alisema kwa vitendo kila anachoansiaha kilitanguliza neno uhuru mfano uhuru na Umoja, uhuru na kujitegemea au uhuru na maendeleo hapo alitaka kusimamia umoja, kujitegemea na maendeleo lakini angalia matumizi ya neno uhuru, ni kwasababu alifahamu kuwa uhuru ndo kila kitu vingine vinafuata.
 
Maendeleo maana yake ni:-
-Maendeleo ya watu (watanzania)
Kuishi nyumba nzuri
Kuvaa vizuri
Maji safi na salama
Elimu bora
Afya bora
Uhakika kuishi kwa amani, bila hofu, kukosolewa na kukosowa kwa uhuru bila vitisho, kuumizana, kufungana, nk

Maendeleo ya vitu hayakidhi viwango kuitwa maendeleo popote duniani endapo njaa, maradhi, ujinga na umaskini bila kuwepo usawa na haki, nisawa na kujaza maji ndani ya gunia yakivuja muda wote yasijae.
Vitu vingine mseme kwa adabu na ukweli kutoka ndani ya mioyo yenu nachambua tafsiri yako ya maendeleo uliyoitoa kama ya mtu taahira nikianza na moja, maendeleo ya watu hutambulika pamoja na vitu vilivyowazunguka na ndiyo maana watu wengi hukimbilia mijini kuyafuata maendeleo ambako
huduma za jamii zinapatikana kwa urahisi ukisema maendeleo ya vitu hayakidhi viwango kuitwa maendeleo nakuona ni taahira kwa sababu kijijini kwako hakuna uwanja wa ndege na kwa ajili hiyo hakuna ndege zitakazofika kwenu na kwakuwa ndege hazifiki kwenu hutaweza kusafiri kwa haraka iwe kibiashara , masomo au magonjwa kitendo cha wewe kutoka ulipotakiwa kufika kwa muda mfupi kitakupngezea gharama na muda ambao uneutumia kufanya jambo jingine hivyo kujiongezea kipato au kukamilisha mambo mengi kwa muda mfupi. Kitendo cha kuwa na ndege siyo anasa bali ni maendeleo yatakayorahisisha usafirishaji wa madawa watu na huduma zingine iko wapi maana yako ya kusema maendeleo siyo vitu? Nyumba nzuri serikali haiwezi kukujengea bali serikali inatengeneza mfumo utakaokufanya wewe upate fedha kirahisi ili ujenge nyumba unayoitaka kwa hiyo kitendo cha kuimarisha miundo mbinu barabara na reli lengo ni wewe ufikishe nyanya zako sokoni kabla hazijaharibika uuze na urudi haraka kwa mkeo kabla hujakutana na malaya wakakuibia fedha zote , lakini pia ukafunge mzigo mwingine haraka uje upate fedha kabla soko halijavurugika, sasa unaposema miundo mbinu inayojengwa na serikali siyo maendeleo unathibitisha pasipo chembe ya shaka kwamba wewe ni TAAHIRA. Afya na hayo mengine unayoyapigia kelele ndiyo hayo serikali inafanya ila nguo nzuri utanunua kwa kufanya kazi zilizorahisishwa na miundo mbinu imara ya Reli , Anga na barabara hakuna nchi duniani inayonunulia watu wake mavazi labda ni kwa baba yako tu.
 
Mkuu, pongezi sana kwa kuelezea vizuri. Watu wengine hawaelewi kwamba kwenye kufanya jambo lolote lile kubwa huwa kuna Kipindi cha mpito.
Sasa umeanza kuitumia akili yako vema

Jiulize tena swali hili, wewe ukianza kujenga nyumba yako, Je utaweza kubaki kwenye matumizi yako ya awali kabla hujaanza kujenga?

Je, hutabana matumizi yako ya siku Kwa siku? Na je ukimaliza kujenga, maisha yako yatabaki hivyohivyo?

Sisi tulikoseaga tokea huko nyuma Sana, Jifunze Kwa Mungu Kwanza, Mungu hakumuumba Mwanadamu Kwanza, badala yake alimwekea Kwanza miundombinu yote wezeshi Ndiyo akamleta duniani, Wewe huwa unajifunza nini kwenye maisha yako?
 
Kumbe siku hizi maendeleo ni kuishi nyumba nzuri na kuvaa vuzuri!! Hilo sio jukumu la serikali ndugu!.
Uko sawa. Lakini usisahau kuwa jukumu la msingi la Serikali ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ili Wananchi waweze kufanya shughuri zao za kujitafutia kipato. Kama unawakopa korosho yao, mauzo ya mazao wanategemea Madalali wanyonyaji, pembejeo kama mbolea mpaka mfuko Tshs. 62,000, ajira zinapungua.....ni dhahiri maisha yatakuwa duni ikiwa ni pamoja na kukosa kula Bata...
 
Back
Top Bottom