Uchaguzi 2020 Kampeni yenye #Miaka5YaKazi inayoendeshwa na Msemaji Mkuu wa Serikali yadolola huko Twitter


Mkuu utetezi wako ni mzuri mno, ila nadhani ufafanuzi hautoshi. Ni bora umfafanulie kuwa wewe unasifia majengo ya hospitali au huduma za afya? Maana kama ni majengo kweli yapo kadhaa, au kama neno kadhaa litapunguza ladha ya sifa zinazomwagwa, ngoja tuseme majengo/hospitali nyingi kuliko hapo awali. Kisha umwambie kuwa kwa sasa mmeanza na majengo/hospitali, kisha itafuata hatua ya dawa. Hapo utakuwa umemuweka sawa. Inawezekana ww na yeye mnatofautiana kwenye mambo kadhaa, wakati ww unasifia wingi, yeye kwake huenda amejikita kwenye ubora wa huduma za afya na sio wingi wa majengo/hospitali.
 
Usisahau kitanda kwa kitanda...Msije usiku lakini mtatuvugia mechi....
 

Unadhani kati ya walimu na madarasa nini huanziasha shule?
 

Ujinga mtupu
 
Nyinyi ni Wezi. Mchwa wenye meno ya chuma. Mwenyekiti wenu Ana weledi wa kuiba na hana kiasi toka 1995 ni kuiba tuuuu.

Argrrrrrrrr mnakera
Kwa nini unasema hivyo ngusero?
 
Kumbe siku hizi maendeleo ni kuishi nyumba nzuri na kuvaa vuzuri!! Hilo sio jukumu la serikali ndugu!.

"Mjinga" mwingine huyo 👆 👆👆 hapo jamani...

Kama wewe unafikiri siyo jukumu la serikali, unadhani kwanini kila nchi inakuwa na serikali?

Na sijui kama unaelewa hata maana ya "serikali" na kazi yake wewe....!
 
Unadhani kati ya walimu na madarasa nini huanziasha shule?
Mkuu, mbona hivo tena!! Swali gani SASA hili

Nionyeshe shule Nami nikuonyeshe walimu!!

Hunionyeshi shule, Nami sikuonyeshi walimu, vitu Hivi Vyote huendana mkuu
 
Anapalilia kibarua cheke,anajua akiingia mwingine yeye atakua hana kazi tena
 
Mkuu, mbona hivo tena!! Swali gani SASA hili

Nionyeshe shule Nami nikuonyeshe walimu!!

Hunionyeshi shule, Nami sikuonyeshi walimu, vitu Hivi Vyote huendana mkuu

Kwa taarifa yako watu hupata elimu popote kisha majengo hufatia

Watua huanzia chini ya miti, walimu wakafundisha taratibu watu wakaelimika ujenzi ukapiga hatua na baadaye vyuo vikuu vikaimarishwa. Watoto wakalipiwa ada na vifaa bora vya kufundishia.

Tunawatoto wanamaliza vyuo siku hizi sio kwamba wabovu bali wamepewa elimu ya hovyohovyo na kudidimiza ndoto zao.

Watoto wamejazana mitaani hawana ajira wala hawajuwi kesho yao ipoje. Hawana mitaji kujiajiri nk. Ujinga ujingaujinga tu wanaambiwa wajiajiri! Kwa njia ipi bila mitaji. Huu ni upuuzi na unafiki wa mchana kweupeee.

Watu huanzia kusali/kuswali chini ya miti au kwenye mabanda chakavu, elimu yao ikapanuliwa, imani ikawajaa, kisha ushawishi wa hatua za ujenzi kushika hatamu na majengo kusimama

Huwezi kununua madenge bila kuwa na watu wenye uelewa, uwezo kifedha na hamasa kuyapanda. Utapata hasara daima. Adhabu anabebeshwa mlipa kodi kwa lazima atake asitake.

Elimu bora kwanza, ilikufungua milango ya ufahamu kwa watoto wetu. Sio BRN!!!!

Afya bora kwanza, madawa bora, madaktari wenye elimu bora na kulipwa vizuri bila kusahau vitendea kazi bora. Bila kuwalipa vizuri madaktari na manesi, .... wataiba vifaa tiba, watadai rushwa nk. Mlala hoi atakufa tu.

Lazima serikali iwe na :-
1. Sera bora, sera yakinifu ambazo zinaeleweka masikioni mwa watanzania nakwamba zinatekelezeka kwa vitendo Sio nadhalia.

2. Mikakati endelevu (strategies) bora ikilinda na kulinda maslahi mapana ya kizazi hiki na kijacho.

Taifa lolote bila uwekezaji kwa jamii yake
1. Mitaji
2. Elimu
3. Afya
4. Miundombinu ya kimkakati bila ubaguzi na ilenge kuwanasuwa asilimia kubwa ya watanzania (wakulima)

Miundombinu yakibaguzi, yakikanda, isiozingatia mizania nikama kuwekeza majogoo wakuku katika ufugaji bila mitetea. Uzazi wake nikitendawili.

Leo nitaishia hapa japo ninamengi mno
 
Unapopevuka akili hauhitaji kuelekezwa Kila kitu na mama, akikuelekeza unachokiona au kukijua unaweza usikiweke sana akilini, Mama muelewa atafurahi kwa kuwa mtoto wake kaanza kukua.
 
Watu wanapotosha sana, maendeleo ya vitu lazima yaende sambamba na ustawi wa jamii, hilo liko hivyo na hakuna anayebisha.

Lakini hii serikali inawekeza zaidi ktk vitu pasipo kujali ustawi wa watu, mfano wanajenga reli mpya wakati reli hii iliyopo haijatumika kihivyo na wala haijachoka kiasi cha kushindwa kukidhi lengo, tatizo la hii reli ya wakoloni ni kukosa ukarabati tu.

Kwenye swala la bwawa, umeme wa maji unasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na mataifa mengi leo hayawekezi tena kwenye umeme wa maji, tungeweza kuwekeza kwenye umeme wa gesi tungeokoa mazingira na kuja kucheza kamari ya ukame.

Kutumia pesa nyingi kununua ndege ni miscalculation kubwa kwani kununua tu ndege kwa kutegemea kuwa watalii watazipanda na kuja kutalii bila kuitangaza nchi yako ni kujidanganya na hata huo utangazaji pia ni uwekezaji unaohitaji pesa nyingi ambazo hatuna na matokeo yake tuliona ndege ikienda India ambako hawana utamaduni wa kutalii.

Hizo fedha walizopoteza kwenye hiyo miradi wangezitumia kwenye kuleta mapinduzi ya kilimo tungepunguza umaskini kwa asilimia 80.

Sasa mradi kama wa kujenga uwanja wa ndege Chato mantiki yake ni nini kama sio utumiaji mbaya wa madaraka.
 
Kwa mzee ukila vizuri, ukivaa vizuri na unaishi kwenye kibanda tandale kwa tumbo unajiona umepiga hatua kweli?
Kama hakuwahi kuwa hivyo kwa nini asiseme amepiga hatua?Hivi weye akili zako zipo "oraita"?
 
Mpaka kwenye mwezi wamefika na kurudi kujiandaa kwenda Mars miaka 5 ijayo kukamilisha mafanikio ya Awamu ya Tano ikiwa SGR itakuwa imefika Mji kasoro bahari, madege yamefikia 11 yamepark Chato, Stiegler's Gorge imekamilika 40%, Ikulu ya Dodoma mfano wa Tower of Pisa imehamiwa. Mabadiliko ya Katiba kuongeza vipindi vya kutawala yatafikiwa kabla ya Uchaguzi wa 2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…