Uchaguzi 2020 Kampeni za Boniface Jacob (CHADEMA) zinasikitisha, anaomba achaguliwe kwa kigezo cha uzawa

Mbeya kwa Wasafwa ndiyo maana Tulia tunampiga mapema kabla ya sadaka ya misa ya kwanza.

Mkuu uchaguzi mwaka huu ni Jumatano usije ukakosea siku...japo naamini tarehe huwezi sahau
 
nikiri wazi people's ukiuliza suala la hela yaan unavuruga kila kitu
 
Ubungo ni jimbo la upinzani kwa muda mrefu,safari hii sijui linaelekea wapi.
 
Mkuu mpe kura kitila Mkumbo halafu utakuja kuona maendeleo ya ghafla ktk jimbo lenu

Kiufupi jamaa anakarama ya uongozi nampenda sana jinsi alivyo na uwezo wa kujenga hoja

Over
Uwezo wa kujenga hoja hana ndio maana alikimbia ACT...CCM hata ukiwa bubu unabebwa,Ukiwa mzinzi(Anfifiro) unabebwa,Ukiwa Mwizi unabebwa
 
Kura yangu kwa Jacob
 
Uwezo wa kujenga hoja hana ndio maana alikimbia ACT...CCM hata ukiwa bubu unabebwa,Ukiwa mzinzi(Anfifiro) unabebwa,Ukiwa Mwizi unabebwa
Nimesema Kitila anauwezo wa kujenga hoja pia siyo mbinafsi
 
Wasafa wamefurushwa pale mjini kwahiyo Tulia ana nafasi nzuri ya kumshinda huyo Mkinga!
Ukabila umehamia kwenye siasa Rasmi,mnaenda kutambika?Kauli hizi zinadhihirisha kuwa siasa chafu nchi hii imerejeshwa na watu wabaguzi na waliofilisika kisera.
 
Nimesema kitila anauwezo wa kujenga hoja pia siyo mbinafsi
Angekuwa sio mbinafsi angebaki ACT kujenga chama badal ya kauhadaika kwa vipande 30..pia alitakiwa akagombee kwa SIngida ilka kwa sababu ya ubinafsi wananchi kule wamemkataa kahamia mjini...
 
Kwenye uzawa namuunga mkono, hata Meya wa Dar au Mji wowote ule ni vizuri awe amezaliwa na kukulia kwenye mji husika
Kwani mkoa wa dar una asilimia ngapi ya watu ambao ni wazawa, wengi ambao wako dar wametoka sehemu nyingine hivyo hiyo hoja ya wazawa haina maana yoyote
 
Kwani mkoa wa dar una asilimia ngapi ya watu ambao ni wazawa, wengi ambao wako dar wametoka sehemu nyingine hivyo hiyo hoja ya wazawa haina maana yoyote

Asilimia kubwa ya wakazi wa Dar wamezaliwa na kukulia Dar, hivyo ni wazawa wa Dar, na kwa maoni yangu mimi Mbunge au Meya wa eneo fulani anapaswa alielewe eneo analotaka kuliongoza vizuri sana, na hii inawezekana tu kama Mgombea akiwa amezaliwa na kukulia au hata tu kukulia eneo husika, na hii ni kwa Mikoa yote Tanzania ilipaswa iwe hivyo, mimi siwezi tu kutoka hapa na kutaka kwenda Meya wa Tunduma au Arusha wakati sipajui Tunduma au Arusha, sizijui changamoto zao, sijui watoto shule wanahitaji nini, n.k., ...
 
..Kitila angeachwa agombee huko kwao Singida, halafu huku Ubungo angeachwa hata Sypirian Mrema au Emmanuel Maluli ambao walipata kura chache.
Unajua akina “Mrema” au “Maluli” originally ni watu wa wapi? Hoja ya uzawa ama la ni non issue kabisa

Augustine Lyatonga Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Temeke ya Dar es Salaam miaka ya nyuma kidogo. Nadhani ulikuwa mdogo mno miaka hiyo
 
Sina takwimu kamili lakini nachoona kila sehemu ambacho nilikaa au kuzunguka naona wengi siyo wazawa wa hapa dar, hata shughuli nyingi za kiuchumi zinasimamiwa na ambao ni watukuja
 
Na wanainchi wengi hawataki hizo what, how, when ndio tatizo

Ndio maana hata PhD wengi kwenye uongozi wanafeli
 
..kuna watu hawa-fit Dsm/mijini na hawa-fit vijijini walikozaliwa.

..unaweza kukuta mhusika ameondoka kijijini wakati amemaliza shule ya msingi.

..na anatembelea kijijini muda mfupi wakati wa likizo tu, tena siyo kila mwaka.
 
Sina takwimu kamili lakini nachoona kila sehemu ambacho nilikaa au kuzunguka naona wengi siyo wazawa wa hapa dar, hata shughuli nyingi za kiuchumi zinasimamiwa na ambao ni watukuja

Inategemea uko Dar ya wapi, lkn sehemu kubwa ya Dar wengi ni wazawa au wamekulia hasa vijana, anyway tusipoteze muda mwingi sana hapo hatuendi mahali, umeielewa hoja yangu lakini?
 
Sina takwimu kamili lakini nachoona kila sehemu ambacho nilikaa au kuzunguka naona wengi siyo wazawa wa hapa dar, hata shughuli nyingi za kiuchumi zinasimamiwa na ambao ni watukuja

..Dsm ina watu wa makabila mbalimbali ambao unaweza kuwaita wazawa.

..kwa mfano mtu aliyezaliwa Dsm na yeye amepata familia hapahapa huwezi kusema siyo mzawa.

..Boniface Jacob asili ya wazazi wake ni Kyela, lakini yeye amezaliwa, amesoma, na ameanzisha familia, hapa Dsm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…