Uchaguzi 2020 Kampeni za Boniface Jacob (CHADEMA) zinasikitisha, anaomba achaguliwe kwa kigezo cha uzawa

Uchaguzi 2020 Kampeni za Boniface Jacob (CHADEMA) zinasikitisha, anaomba achaguliwe kwa kigezo cha uzawa

..kuna watu hawa-fit Dsm/mijini na hawa-fit vijijini walikozaliwa.

..unaweza kukuta mhusika ameondoka kijijini wakati amemaliza shule ya msingi.

..na anatembelea kijijini muda mfupi wakati wa likizo tu, tena siyo kila mwaka.

Nilichotaka kusema ni kwamba ni vizuri Mgombea alijue vizuri eneo analotaka kuliongoza changamoto zake mfano mimi mahali nilipokulia ukiniuliza nikwambie changamoto zake nitakwambia vizuri sana kwa maana nazijua, ni sawa na kutaka kwenda kugombea uongozi kwa mfano Mtwara wanakolima korosho au Mbeya wanakolima Maparachichi wakati haujui chochote kuhzsu hilo eneo na changamoto zinazowakabili watu wa eneo hilo utawezaje kutatua tatizo? Lkn fikiria mtu aliyezaliwa na kukulia hilo eneo labda hata wazazi wake ni Wakulima wa korosho au Maparachichi huoni kwamba anaweza kuwa mtu mwenye manufaa zaidi klk mgeni?
 
Mwalimu Nyerere alisema ukianza kubagua watu kwa namna yoyote hile hi dhambi Ni mbaya Ni sawa ukianza kula nyama ya mtu kamwe hutoacha.

Mpaka boni anakimbilia hoja ya uzawa maana yake ameshikwa pabaya na prof na anachokifanya Ni kuomba kura za huruma kwa watu wa Ubungo
Pamoja na hayo yote lakini ndio desturi ya binaadam ilivyo kuwa anapenda kitu ambacho ana ufaham nacho kuliko kile kigeni, hata kama Kitila anamzidi kete Boniface bado hawa watu wazawa wa eneo husika wataangalia Upande wao zaidi- ni nani anayajua mazingira yetu vizuri atakua huyo mzawa na si vinginevyo
 
Inategemea uko Dar ya wapi, lkn sehemu kubwa ya Dar wengi ni wazawa au wamekulia hasa vijana, anyway tusipoteze muda mwingi sana hapo hatuendi mahali, umeielewa hoja yangu lakini?
Hoja yako ni kujua kero za eneo husika, ili kutatua kero lazima uzijue vizuri, mtu yeyote awe mzawa asiwe mzawa ni rahisi sana kuzijua kero maana kero nyingi zinajulikana. Ukiwa tu na uwezo wa kusimamia utatuzi wa kero ni kigezo tosha cha kugombea popote Tanzania kama wewe ni mtanzania
 
Sawa, sijasema haiwezekani kwa mgeni kufanya miujiza lkn ukiwa mzawa wa eneo au kama umekulia eneo husika kuna tofauri na mtu mgeni ambaye halijui hilo eneo vizuri, na ndiyo maana hata kwenye kampuni kubwa wale viongozi waliokulia kwenye Kampuni na kufika juu kuanzia chini huwa ni wazuri zaidi klk wale wakuja walioletwa tu na kupewa u CEO. Mfano mtoto aiyesoma Shule ya Kata na kufika juu anaweza kuwa Waziri mzuri wa Elimu kuliko yule aliyesoma International school, linapokuja swala la kutatua matatizo ya wanafunzi , ...
 
Pamoja na hayo yote lakini ndio desturi ya binaadam ilivyo kuwa anapenda kitu ambacho ana ufaham nacho kuliko kile kigeni, hata kama Kitila anamzidi kete Boniface bado hawa watu wazawa wa eneo husika wataangalia Upande wao zaidi- ni nani anayajua mazingira yetu vizuri atakua huyo mzawa na si vinginevyo
Kama kujua kero ingekuwa ni kigezo cha kuondokana na kero duniani kusingekuwa na kero. Cha msingi ni njia za kutatua changamoto, wafanyakazi wengi wa waajiriwa na ambao ni wateuli wa viongozi wa serikali wengi siyo wazawa wa eneo husika lakini ufanisi wa kazi unatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.
 
Tunachojua ni kwamba serikali iliyatenga majimbo na kata zote zinazoshikiliwa na upunzani.
na awamu ijayo itakuwa hivyo hivyo.
so boniface mdogo wangu wa MABIBO ajikaze tu.
 
Bila unafiki, ukimsikiliza Kitila Mkumbo (PhD) kwenye jukwaa then ukaenda kwa Boni utaona tofauti kubwa sana. Nadhani shule na exposure vinachangia. Boni haelezi strategies zake (what, how, when...)

Ubungo ni kama imetengwa kimyakimya hasa kwenye miundombinu ya barabara za mitaani. Na hili la wabunge wa CHADEMA kukimbia jimbo kila wanapomaliza muda na kuchota mafao yao imekuwa moja ya sababu zinazowakera sana wana Ubungo

Boniface anaweza kuadhibiwa kwa makosa (real or perceived) aliyofanya Kubenea
Ubungo na Mbeya (M) tunataka wasomi wenye PhD
 
Sawa, sijasema haiwezekani kwa mgeni kufanya miujiza lkn ukiwa mzawa wa eneo au kama umekulia eneo husika kuna tofauri na mtu mgeni ambaye halijui hilo eneo vizuri, na ndiyo maana hata kwenye kampuni kubwa wale viongozi waliokulia kwenye Kampuni na kufika juu kuanzia chini huwa ni wazuri zaidi klk wale wakuja walioletwa tu na kupewa u CEO. Mfano mtoto aiyesoma Shule ya Kata na kufika juu anaweza kuwa Waziri mzuri wa Elimu kuliko yule aliyesoma International school, linapokuja swala la kutatua matatizo ya wanafunzi , ...
Naweza kutumia hiyo hoja ya kampuni nikaelezea vizuri namna mtu wa kutoka nje anaweza kuliendeleza kampuni kuliko mtu wa ndani hasa linapokuja kutatua changamoto kwa kampuni iliyokwama kwavile anaweza kutumia njia zile zile zilizokwamisha kampuni, na akitokea mtu kutoka kampuni iliyofanikiwa anaweza kukwamua ambayo imekwama.
 
Sawa, lkn nijuavyo mimi traditional companies nyingi zinafwata huo mfumo nilioulezea yaani insider anatokea chini mpaka Juu, ni mara chache sana wanachukuwa mtu wa nje na kumpa kazi kubwa, isitoshe huwezi kupanda juu kwenye ngazi ya uongozi kwenye kampuni iliyokuwa makini kama haujaonyesha uwezo wa kutatua changamoto zilizopo, na ndo maana hata ukienda kwenye maduka ya Wahindi mjini ambayo yapo tangia tunakuwa mpaka leo hii utakuta dukani kuna mtoto wa mwenye duka, akitoka Shuleni anafikia dukani, na ndiyo hawa akina Mo, Rostam, Asas, Abood hata Bakhresa & Co., hawachukui outsider hao, ...
 
CCM tumechemka kumleta mtu kutoka Singida aje kugombea Ubunge Ubungo, wakati kuna wana-CCM wazawa wa hapa Ubungo.

Alichokisema Bonny ndiyo maoni ya wengi hapa Ubungo.

Kitila angeachwa agombee huko kwao Singida, halafu huku Ubungo angeachwa hata Sypirian Mrema au Emmanuel Maluli ambao walipata kura chache.

Boni nae aende mbeya kwao
 
Yule mwili umemzidi San
Obesity huwa unapunguza Sana uwezo was kufikiri
 
Unajua akina “Mrema” au “Maluli” originally ni watu wa wapi? Hoja ya uzawa ama la ni non issue kabisa

Augustine Lyatonga Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Temeke ya Dar es Salaam miaka ya nyuma kidogo. Nadhani ulikuwa mdogo mno miaka hiyo

Nilichokiandika ninauhakika nacho broo!

Kati ya list ya Wabunge wa Ubungo ni Hussain Mmassy(2000), Charles Keenja, Mnyika, na Lamwai.

Asilimia kubwa ya wakazi wa Ubungo ni wa asili moja na akina Lamwai, Mrema, Keenja na Mmassy.

Mimi nipo Ubungo na ninachokiandika nina utafiti nacho.

Hivi unajua kwamba Jimbo la Ukonga akina Mwita, Marwa na Mura ndiyo hushinda huko?

Kama hujaelewa usiniite tena dogo!
 
Back
Top Bottom