LGE2024 Kampeni za uchaguzi huu ni kama unasikiliza taarabu, zimejaa mipasho mwanzo mwisho!

LGE2024 Kampeni za uchaguzi huu ni kama unasikiliza taarabu, zimejaa mipasho mwanzo mwisho!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam ndugu zangu

Wanasema mtembea bure sio sawa na mkaa bure, katika harakati zangu za mtu mweusi ndani ya hizi siku mbili nimejikuta nakumbana na Wagombea kadhaa wa Chama cha Mapinduzi na CHADEMA, Nilidhani kwamba kampeni hizi zitahusisha sera za Wagombea kuwaeleza nini hasa Watafanya ili kuwashawishi Wananchi kuwachagua.

Mtu Mweusi Mwingine aliwahi kusema:
- LGE2024 - Kuwe na utaratibu wa kutoka kazini mapema kipindi cha kampeni za uchaguzi ili tukasikilize sera. Au kama vipi mtuletee wagombea wajinadi maofisini

Kumbe ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni Wagombea wanatupiana vijembe kwa kupondana kivyama, hawasemi lolote linalomsaidia Mwananchi.

Mfano, Mgombea aliyeonekana ni wa CCM nimemsikia akimnadi Rais Samia pamoja na kuwaponda wapinzani na kuwaita watu wa fujo

Mgombea wa CHADEMA nimemsikiliza sera zake ni za kulalamikia uonevu kutokea chama Tawala na kusisitiza Wananchi wapige kura ya hapana kwa Mgombea aliyepitishwa.

Hakika sijasikia neno lolote lenye tija kwa Wananchi, huko kwenu vipi? Wagombea wamemwaga madini? Hawa wakwetu aisee wote hakuna kitu.

Till next time,

Wenu Liyongo Kitamkali
 
Back
Top Bottom