Hivi mbona watawala hawajifunzi? Hivi mbona wanatuchukulia poa sana?
Mr.Clean Benjamini Mkapa, alifanya yake na Anben yake, akajimilikisha na mgodi wa makaa ya mawe ya Kiwira...sijui alikuwa anawaza nini kichwani mwake wakati anafanya hayo, labda ni ile imani yake kwamba Watanzania ni malofa.
Haya, akaja JK na mambo yake ya Home Shopping Center na Lugumi...pesa na raha za muda mfupi hadi sasa Lugumi nyumba zinauzwa, na hadi wametuletea Dr.Louis Shika.
Sasa, amekuja mkali wa kufight corruptions(sic)...corruptions is a cancer... mapema tu kashfa nzito zinarindima, mara Mayanga mara Madege mabovu mara Uwanja wa Ndege kijijini...tunaelekea wapi? Hivi anatuchukuliaje? Kwanini watawala hawajifunzi? Kwanini hawaogopi kufanya haya madudu?