Kampuni nyingi za Wachina unakuta Ni share ya watu hata 500

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Wachina inapo kuja swala la Ushirikiano wako juu sana. Viwanda vyao vingi na hata kampuni zinazo kuja kuwekeza huku na kupewa tenda za kujenga Barabara na Majumba ni muunganiko wa watu wengi walikaa na kuunda.

Unakuta kampuni au kiwanda kimeanzishwa na watu 100 au hata 500 na kila mmoja ana majukumu yake. Katika watu 500 kuna Ma injinia humo, kuna watu wa masoko kuna kila aina ya mtalamu na wote wana piga kazi.

Unakuuta malengo yao ni kuwa na viwanda hata 500 ambapo baada hata ya miaka 30 Wote watakuwa na viwanda.

Hufanya hivyo ili kuunganisha nguvu/mitaji yao na kuwa na nguvu moja.

KIBONGOBONGO

Hilo bongo haliwezekani kila mtu anataka aonekane yeye, watu wanawaza kudhurumiana tu kuibiana na kadhalika.

Unakuta mtu ana kampuni ya ujenzi wa Barabara muda wote wa uhai wake ataishia kujenga barabara za vijijini tu make hana mtaji wa kushika tenda kubwa na pia hataki kuungana na wenzake na wenzake pia hatawaki kuungana.

Ni vigumu sana kushindsna na Wachina wenye nguvu kubwa sana na walio ungana. Ndo maana wameshika tenda Africa nzima za kujenga majumba na Barabara.
 
Changamoto kubwa ni watu kutopenda kazi kabisa. Tunaweza jadili mpaka mwakani, lakini watu wanataka kuokota dodo tu lakini kuuotesha mwembe hawataki. Hapa ndio shughuli ilipo. Mnaungana na mdau, kwenda site hataki ila anataka paper work tu ndo afanye, halafu wewe ulete data toka site.
 
Hii ni changamoto kubwa sana... mfano... kuna masoko ya bidhaa yana lipa sana... mbao (China india nk) lakini hakuna wakutuletea fursa waliopo huko nje na kutueleza ni bidhaa zipi toka kwetu hapa zinaweza pata masoko makubwa sana na kuingiza kipato kizuri kwa wafanyabiashara walio jikusanya kufanya hizo biashara husika
 
hili swala lina hitaji mjadara mpana sana... hasa tukianzisha humu na kupata suruhu humu ita leta uhamsho wa kupiga hatua kwenda mbelee...
Nimefanya kautafiti kadogo, nimekuja kuona wengi wetu tunakuwa na picha ndogo sana ya kitu tunachotaka. Ukipata harufu tu ya unachotaka basi unabweteka na kujiona umefika. Tunapenda shoti kati sana, matokeo yake wenye mamlaka wakija kufuatilia unakuta kamradi kanakufa.
 
yeah ni kweli... uwa kuna mkumbo fulani wa kusikia kitu fulani kina lipa basi... watu wote watakimbilia huko... baada ya muda utasikia nimeacha hakuna soko... nk...
 
Hiki kilichopo ndio kimeoza, hakijiwezi kabisa. Sasa kitawezaje kuonyesha njia?
Hapa ndipo kwenye tatizo... Jaribu kuona kuwa waTZ wengi vipaumbele vyao ni udaku... na wachache wanatumia huo mwanya kuingiza pesa na wengine kutumika kama chumio bila kujijua au kwa kujijua...

ila ukileta mada yenye kuleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo japo ina magumu ndani yake na ina itaji uvumilivu na kujitoa... nazani kwa uzoefu wako uta ungana na mimi kuwa hauto pata mtu...
 
Kwa mara ya kwanza watakuja kama nzige, baada ya miezi utasikia, nina udhuru, mtoto wa binamu ana sendoff siwezi kukosa sbb familia haitanielewa. Wa pili atakwambia leo Man U anakipiga na Real siwezi kosa hiyo mechi. Wa tatu atakwambia jumapili ni komunio sitafika site. bla bla bla mpaka kundi linaishia.
 
Kuna shida ya watu kutamani pesa za chap chap Hasa sisi vijana tunaomaliza chuo.unakuta MTU kapata kazi Fulani lakini kule hakuna kazi nyingi na hi hutokea sana serikalini MTU anaenda wiki nzima ila Massa anayofanya kazi ni kidogo sana na mshahara anapata.sasa watu walio nje ya mfumo huo wanaona ya Nini kutumia nguvu na akili Wakati Kuna dodo chini ya mpera.
Kuna msemo usemao ukitaka kwenda mbali nenda mwenyewe ila ukitaka kwenda mbali zaidi nenda na mwenzako huu usemi umefanikiwa kwa jamii baadhi kama wahindi,waarabu.Jews. na wachaga kidogo.Tazama biashara za wahindi kama wale wa TATA holding wanapeana mashavu kila bara waendalo.hata hawa wa hapa wanaungana na kuanzisha biashara ndogo mpaka inakuwa kubwa.
Ni mjadala mkubwa sana huu
 
Wachina inapo kuja swala la Ushirikiano wako juu sana. Viwanda vyao vingi na hata kampuni zinazo kuja kuwekeza huku na kupewa tenda za kujenga Barabara na Majumba ni muunganiko wa watu wengi walikaa na kuunda.

Unakuta kampuni au kiwanda kimeanzishwa na watu 100 au hata 500 na kila mmoja ana majukumu yake. Katika watu 500 kuna Ma injinia humo, kuna watu wa masoko kuna kila aina ya mtalamu na wote wana piga kazi.

Unakuuta malengo yao ni kuwa na viwanda hata 500 ambapo baada hata ya miaka 30 Wote watakuwa na viwanda.

Hufanya hivyo ili kuunganisha nguvu/mitaji yao na kuwa na nguvu moja.

KIBONGOBONGO

Hilo bongo haliwezekani kila mtu anataka aonekane yeye, watu wanawaza kudhurumiana tu kuibiana na kadhalika.

Unakuta mtu ana kampuni ya ujenzi wa Barabara muda wote wa uhai wake ataishia kujenga barabara za vijijini tu make hana mtaji wa kushika tenda kubwa na pia hataki kuungana na wenzake na wenzake pia hatawaki kuungana.

Ni vigumu sana kushindsna na Wachina wenye nguvu kubwa sana na walio ungana. Ndo maana wameshika tenda Africa nzima za kujenga majumba na Barabara.
We kweli unaona bali sana, kwenye suala hili wabongo kushirikiana ni tatizo kubwa sana ndio maana hatuendelei shida kubwa ni hizi:
1. Uaminifu ni sufuri
2. Uchapakazi ni sufuri
3.Uvumulivu ni sufuri
4. Tunapenda shortcut 100%
5. Wivu usiokuwa na maana
6.Ubinafsi wa hali ya juu.
In short hatupendani na sio wazalendo ndo maana hata kiongozi akipata kaupenyo anapiga ileile.
Tukumbuke UMOJA NI NGUVU. mfano mtu ana 4M , akimshirikisha mwenzie mwenye 4M si mtaji wa 8M huo mnafanya biashara kubwa yenye mwelekeo. kampuni nyingi za kibongo au wabongo wanaoshirikiana wengi huishia kufarakana tu.
Tubadilikee.
 
Back
Top Bottom