Kampuni nyingi za Wachina unakuta Ni share ya watu hata 500

Ni kweli wachina wana ushirikiano sana nimefanya na wachina kazi ya wik 3 hvi nimeona hilo lakini pia hata sisi hiyo hofu ya kuzimana ni kweli ipo ndo maana tuna kampuni nying lakin haziend mbele sababu ya mitaji mi nazani mkiunda kampuni kuna haja kuwa makubaliano yaliyopo kwenye memart mnakubaliana nayo hasa upande wa kuweka share sawa.......
 
Mkuu kwenye paper work hakuna tatizo, tatizo lipo kwenye kutekeleza mliyoweka kwenye makubaliano. Tarehe ya kutoa fedha hizo kidogo zije mezani, unaanza kusikia udhuru. Ama, awamu ya kwanza mnatoa fresh, baada ya pale wadau wanaingia chaka, wakiona dalili fresh wanaanza kurudi kimya kimya na vitu vya ajabu.
 
Waafrica Ni shida sana,culture yetu Ni ya kutaka mafanikio ya faster tu. Wivu,uvivu ndo vimejaa mwetu. Lakin nahisi kuna njia ya kuweza kuandaa kizazi kijacho kikaanza kubadilka. Kuliweka kwenye mfumo wa elimu kwenye elimu ya uraia lakin pia Kwa kuweka Sheria Kali ya kudhibiti wa saliti . Na mahakama zetu zisiwe na upendeleo. Hiyo inaweza kusaidia Ila sijui lini litafanyika. Wenzetu hata wazungu wanalindana kazini lakin waafrica kazi kusutana, kuchongeana Kwa boss na kufukuzana tu Basi. Mungu atunusuru tu. But wachache mjaribu it can work
 
Yote uliyosema upo sahihi kabisa ndugu, niongezee tu haya:
1.Watz wengi hupenda kufanya KAZI KIDOGO na kufanya STAREHE SANA (tatizo)
2. Kukosa vision na msimamo (tatizo kubwa)
3.Kupenda shortcuts/overnight success

Now, what should be done? Change must begin with us. Kupitia hii thread we can do sth to change this.

Hapa jukwani tuna watu muhimu sana and they/we can change the course.Imagine wakiungana watu kama Chasha, Malila and Bavaria... I believe watafika mbali sana.
 
Nakuelewa mkuu.
 
Baba yangu mkubwa ni Engineer alianzisha kampuni ya ujenzi wa nyumba baadae akawaingiza watoto wake wawili mmoja kama mhasibu maana alisoma uhasibu TIA na mwingine ndo msimamizi msimamizi wa kampuni ili baadae waje kuwa warithi wa kampuni hiyo!
Baada ya miaka 3 akagundua mtoto wa kike alikua anachukua hela na kujenga gorofa bila yeye kujua!! Wakati wa kiume alianzisha Kampuni nyingine ya ujenzi kwa siri
unaelewa nn?
 
ni tatizo sana. mkuu unakuata mmeanzisha kampuni la ujenzi na ww ni fundi bomba lakini unataka kukaa ofisini
mhasibu hataki kufanya kazi nyigine kwa ajili ya maendeleo ya kmpuni zidi ya kukaa ofisini. kila mtu anataka kua boss
 
Kuna mdau mmoja nilifanya nae project ya ufuta morogoro.

Aliniudhi hadi ile project nikaiachia njiani nikaenda kuanzisha nyingine peke yangu Kisarawe.

Kila week anatafuta sababu zisizoeleweka.

Toka wakati huo nikasema sifanyi mradi wowote na mtanzania mwenzangu. Wanamihemko mwanzoni. Badae wanakimbia ukifika muda wa mavuno ndo wanaanza kuulizia mmepata nini.
 
Ndo changamoto zetu hizo
 
ni tatizo sana. mkuu unakuata mmeanzisha kampuni la ujenzi na ww ni fundi bomba lakini unataka kukaa ofisini
mhasibu hataki kufanya kazi nyigine kwa ajili ya maendeleo ya kmpuni zidi ya kukaa ofisini. kila mtu anataka kua boss
Dah wachina hapo ndo wanapo tupigia bao. Sijui tutafanyaje
 
Dah very Sad, shida yetu nini hasa? Sijui tumezaliwa na Tamaa au vipi
 
Haya mambo yanahitaji commitment sana, kama Malila anavuo sema yaani kuna changamoto sana sasa tunafanya nini?
 
Sio kuweka kwenye soma la Ulai, shida ni Mind set zetu na kutaka kuonekana sana.

Mtu anataka akienda sehemu waseme fulani ana kampuni na si waseme fulani.wana kampuni.

Cheki basi la Ndugu yetu na si Cheki basi la kampuni na mmoja wa wamiliki ni ndugu yetu
 
Hahaha Malila ni kweli halafu watu tunakuwa na Over expectations, na tunataka mafanikio hata kesho, ila ukiwaambia tutaanza kuona mafanikio baada ya 10 years hakuna anaye taka. Hii ndo shida kubwa sana tulio nayo.
 
Mkuu shida sio Makubaliona hata mgeenda kuapishana kwa Raisi wa nchi bado kutakuwa na shida. Tatizo ni tabia zetu.

Mentality zetu ndo shida tuna utamaduni wa ajabu sana, tunawaza mabaya tu muda wote
 
Hapo kwenye Uvimilivu ndo kuna shida kubwa sana na pia hapo kwenye wivu na tamaa.

Mnaunda kampuni lakini hapo hapo wanajikata tena wawili wanaunda kikampuni ndani ya kampuni hao wawili tena wao kwa wao bila kujuana kila mmoja ataunda tena kijikampuni chake ndani ya kijikampuni ndani ya kampuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…