Kampuni nyingi za Wachina unakuta Ni share ya watu hata 500

Ndo nasema sisi sijui tulikosea wapi, yaani kuna sehemu tulikosea kabisa
 
Malila hapo kuna kuwa na Uzuru wa kufa mtu. Utasikia Mtoto kalazwa, kuna msiba, Kuna vikao vya kifamilia.

Yaani ni uzuru juu ya Uzuru
 
Ubinafsi haujawahi na hutatuacha salama...Well said friend..well said.
 
Mkuu unaona hata viongoz wa dini nao ni wasaliti
Wanapanga mambo wakiwa wote badae anazunguka wengne nakusema sikuhusika Ila nashangaa Jina langu kuwepo, period kabsa wanaudh Sana
Kazi kujipendekeza kuchongea wengne tuu unafiki mwanzo mwisho
Halafu ni wazee unafikir sisi vijana tutajifunza nn kama sio kuwaiga tuu japo ni upumbavu
USHAURI
Kuwepo sheria Kali Sana ya kudhibiti usalit wa Aina yoyote ile
 
Wabongo selfish inatumaliza. .lakini shida tulionayo na hatutaki kufikiri mbali au hutuwez kuhimili pressure au challenges zinazokuja mbele yetu.
Utaanzisha biashara lakini kabla ya ku take off tayari watu wanakuja nyuma na shida kibao.
Uki wa ignore chuki zina anza huku wewe bado hujawahi kuiona faida hata kidogo lakini wao wanajua unapata saaana.
Kingine ni uvumilivu hatuna, biashara mpaka isimame jamani sio mchezo.
Wengine tunafeli sababu ya kuibebesha ofisi mzigo usio stahili. Ajiri wafanyakazi kulingana na mahitaji sio sababu mdogo wako anashida ya Ajira unamuweka pale.
Biashara itakufa tu
 
ipo hivyo kaka somali people wakiwa ughaibuni, mfano Uingereza wanachangishana kama watu kumi pound 1000. Tayari wanakuwa na pound 10,000/= wanafungua mgahawa wao wenyewe ndio wanakuwa wafanyakazi pia wao wenyewe wanakuwa suppliers wa mahitaji ya mgahawa,mfano nyama, nyanya,mafuta nk nk kwa kugawana.Baada ya muda mgahawa ukichanganya wanaajiri watu na wao wanaendelea kuwa ma suppliers maisha yanakwenda
 
Haya huku inawezekana sema sijui tulikoseaga wapi.

Watu 20 wakichangishana laki 5 kila mmoja ni Miliom 10. Zinatosha wanafungua mgahawa.

Kwenye hao 20 watakuqepo wakupika, kuosha vyombo, cashier, kila kotu na wanakuwa wanapeana zamu.

Dah tuna matatito sana
 
Hao unawaeleza ukweli haina haja ya kiwadanganya..waambie tu. Bora lawama kuliko hasara
 
Haina haja ya sheria kama watu wenyewe hawana Uaminifu ni hawana tu
 
Uzi mzuri sana, kama alivyosema kaka Malila hapo juu kipindi namaliza chuo tukapanga na mdau mmoja tuingie poli kwenye kilimo, tumepanga vizuri na bajeti kabisa. Sasa tunamalizia makubaliano na kuhitimisha tuingie field jamaa ananiambia amepata mishe so atatoa pesa tu ila huko shamba siku moja moja ndio ataweza fika ila sio full time, sikupepesa macho nikamchinjia baharini, so hii ni changamoto kubwa sana mtu anataka aone pesa bila kutoa jasho.

Lakini kingine naona tunakatishana sana tamaa, unaweza ukaomba ushauri wa kibiashara kwa mtu majibu utayopewa ni so negative, au unaweza kuanzisha biashara lakini hao hao unadhani ni marafiki au ndugu wanaanza ku curse kwa tutaona jamaa hafiki mbali biashara yenyewe hiyo.

Wabongo wengi hatupendi kuona mtu anapanda ngazi, me nshaamuaga kuwachinjilia mbali watu wote wanaoleta negative energy katika hustle zangu.
 
Aisee kweli Wabongo tuna tatizo tena tatizo kubwa sana na kwa hili sijui ka tutakuja kuendelea asee

Ubinafsi na tamaa ni tatizo kubwa sana.

Lakini chanzo cha yote haya ni Umasikini,,Unakuta mtu keshapigika Zaidi ya miaka 5 labda bila mchongo cku akiote mchongo anaona kashachelewa sana so cha kwanza kufikiria ni kupiga ili aende sawa na wengine
 
Nipo. Umepotea sana mkuu sikusikii
Kaka nipo sana, ndo maana nimekusoma nikaona nichangie kidogo.
Nimejichimbia Njombe naotesha parachichi za kikundi tangu 2016 mpaka 2018 ndo namalizia awamu ya kwanza ya upandaji. Ukiachia mbali majukumu ya kikundi, lakini na mimi mwenyewe nilikuwa naotesha miti ya mbao na parachichi.
 
Niliamua kufanya mchezo wa hatari kwa kujitolea kupiga kazi kwa niaba ya wenzangu kwa miaka mitano hivi. Kuna Watz waliniunga mkono vizuri, ndo nikajua uwepo wa matatizo la wadau kutopenda kufanya kazi. Nilifanya nao miradi kadhaa ya binafsi. Na miradi mitatu ya pamoja. Miradi miwili ya pamoja imefanikiwa vizuri ikiwemo parachichi na samaki. Mmoja umekwama sbb ya siasa, tumeusitisha kabisa. Miradi ya watu binafsi mingi imedorora sana, kisa watu hawataki hata kwenda kuona mradi wake ukoje. Anataka kuona kwa njia ya picha tu.

Kwa hiyo, kama unataka kujitolea kufanya kazi kwa niaba ya Watz, pesa ipo, wewe toa mchanganuo vizuri. Lakini utakutana nao kwenye kugawana faida tu.
 
Walionywa mfano wakandarasi...... Kuna kazi nyingi wameanza kujifunza na kushirikiana, mfano kuna daraja liligharumu bilioni 10 waliungana wakandarasi 10 hivi
 
Walionywa mfano wakandarasi...... Kuna kazi nyingi wameanza kujifunza na kushirikiana, mfano kuna daraja liligharumu bilioni 10 waliungana wakandarasi 10 hivi
Hiyo waliungama kwa kazi moja na baada ya hapo kila mtu anashika zake.

Hii mchi Makandarasi Wazawa wangeungana na kuwa na hata Kampuni 5 tu au 4 zingetosha kabisa na wangeweza kushindana na wachina
 
Na lawama juu, na baada ya kugawana faida hutawaona tena kila mtu atakuambia anapumzika kwanza au ngoja kwanza ajipange upya. Au mambo yanaingiliana
 

mkubwa yaani hii yako nimekutana nayo live sijui umeijuaje mzee. watz kwa visingizio ni balaa
 
Hao watoto ni ma ndoroooooobo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…