Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 20+ naweza kujiita ni muathirika wa tukio ambalo naona linaelekea kuwa la “kitapeli” uliotendwa na kampuni inayojitangaza kutoa fursa za kazi na mafunzo nje ya nchi inayoitwa
Star Employment Service Tanzania.
Nilianza mawasiliano na Mkurugenzi wa kamouni hiyo kupitia Intaneti baada ya kuona matangazo ya nafasi za kazi kwenye ukurasa wao. Awali, nilikuwa mwanafunzi niliyefanya kazi na kampuni nyingine nikiwa nchi za nje, lakini baadaye nilitamani kupata fursa ya kwenda kufanya kazi rasmi nchini Ujerumani.
Mkurugenzi huyo alinihakikishia kuwa ana uwezo wa kunipatia nafasi hiyo ya kazi sekta ya mifugo nchini Ujerumani.
Aprili 2026 alinitumia nyaraka za malipo (
invoice) pamoja na maelekezo ya taratibu zote zilizopaswa kufanyika, akidai kuwa mchakato huo ungetua muda mfupi tu.
Nilifanya malipo kwa installment mbili, jumla ya gharama zote ni Shilingi Milioni 11.2
, ni kiasi cha fedha ambachi nilikikusanya muda mrefu na nilikomba akiba yangu yote.
Baada ya malipo, Mkurugenzi huyo alinieleza nirejee nchini Tanzania kutoka huko nilikokuwa ili kukamilisha taratibu ndogondogo zilizobaki, akiahidi kuwa kufikia Julai 2026 kila kitu kingekuwa kimekamilika na ningekuwa nimeshaondoka.
Niliporejea Tanzania, mambo yalianza kubadilika, alianza kukwepa kupokea simu zangu, na kila alipopatikana alitoa sababu zisizoeleweka.
Hadi leo hii Agosti 20, 2026 sijapewa mkataba wowote wa kazi wala nyaraka za safari kama alivyoeleza, nikienda kwenye ofisi zao kupata ufumbuzi, nakutana na wafanyakazi wa pale wananieleza kuwa Mkurugenzi wao hajafika ofisini kwa zaidi ya miezi mitatu, na mawasiliano yao naye yanafanikika kwa simu tu.
Mwezi uliopita, baada ya kuona mchakato umekuwa mgumu na haueleweki, nilifika ofisini na kuwaambia warejeshe fedha zangu (
refund) ili nitafute fursa nyingine, walikubali na kunipa barua iliyogongwa muhuri Julai 24, 2026, kupitia Mkurugenzi huyo nikaahidiwa kunirudishia fedha zangu ndani ya siku nne zinazofuata.
Zimeshapita wiki kadhaa Mkurugenzi huyo ameendelea kunipiga chenga, akiniahidi "njoo Ijumaa, njoo Jumamosi," bila mafanikio na muda mwingi hapokeo simu.
Hali hii imenirudisha nyuma sana kiuchumi na kisaikolojia, kwani fedha hizo zilikuwa akiba yangu yote niliyojinyima wakati nikiwa mwanafunzi.
Nimejaribu kutafuta ushauri wa kisheria ili kuchukua hatua za kumpoti Polisi au kufungua shauri, na sasa naomba msaada wa mamlaka husika na jamii ili niweze kurudishiwa fedha zangu zote na haki yangu ipatikane.