KERO Kampuni Star Employment Service TZ nirejesheeni 11.2M nilizowapa mnitafutie ajira nje

KERO Kampuni Star Employment Service TZ nirejesheeni 11.2M nilizowapa mnitafutie ajira nje

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 20+ naweza kujiita ni muathirika wa tukio ambalo naona linaelekea kuwa la “kitapeli” uliotendwa na kampuni inayojitangaza kutoa fursa za kazi na mafunzo nje ya nchi inayoitwa Star Employment Service Tanzania.

Nilianza mawasiliano na Mkurugenzi wa kamouni hiyo kupitia Intaneti baada ya kuona matangazo ya nafasi za kazi kwenye ukurasa wao. Awali, nilikuwa mwanafunzi niliyefanya kazi na kampuni nyingine nikiwa nchi za nje, lakini baadaye nilitamani kupata fursa ya kwenda kufanya kazi rasmi nchini Ujerumani.

Mkurugenzi huyo alinihakikishia kuwa ana uwezo wa kunipatia nafasi hiyo ya kazi sekta ya mifugo nchini Ujerumani.

Aprili 2026 alinitumia nyaraka za malipo (invoice) pamoja na maelekezo ya taratibu zote zilizopaswa kufanyika, akidai kuwa mchakato huo ungetua muda mfupi tu.

Nilifanya malipo kwa installment mbili, jumla ya gharama zote ni Shilingi Milioni 11.2, ni kiasi cha fedha ambachi nilikikusanya muda mrefu na nilikomba akiba yangu yote.

Baada ya malipo, Mkurugenzi huyo alinieleza nirejee nchini Tanzania kutoka huko nilikokuwa ili kukamilisha taratibu ndogondogo zilizobaki, akiahidi kuwa kufikia Julai 2026 kila kitu kingekuwa kimekamilika na ningekuwa nimeshaondoka.

Niliporejea Tanzania, mambo yalianza kubadilika, alianza kukwepa kupokea simu zangu, na kila alipopatikana alitoa sababu zisizoeleweka.

Hadi leo hii Agosti 20, 2026 sijapewa mkataba wowote wa kazi wala nyaraka za safari kama alivyoeleza, nikienda kwenye ofisi zao kupata ufumbuzi, nakutana na wafanyakazi wa pale wananieleza kuwa Mkurugenzi wao hajafika ofisini kwa zaidi ya miezi mitatu, na mawasiliano yao naye yanafanikika kwa simu tu.

Mwezi uliopita, baada ya kuona mchakato umekuwa mgumu na haueleweki, nilifika ofisini na kuwaambia warejeshe fedha zangu (refund) ili nitafute fursa nyingine, walikubali na kunipa barua iliyogongwa muhuri Julai 24, 2026, kupitia Mkurugenzi huyo nikaahidiwa kunirudishia fedha zangu ndani ya siku nne zinazofuata.
Screenshot 2026-08-20 113005.jpg

Screenshot 2026-08-20 113322.jpg

WhatsApp Image 2026-08-18 at 21.09.22.jpeg
Zimeshapita wiki kadhaa Mkurugenzi huyo ameendelea kunipiga chenga, akiniahidi "njoo Ijumaa, njoo Jumamosi," bila mafanikio na muda mwingi hapokeo simu.

Hali hii imenirudisha nyuma sana kiuchumi na kisaikolojia, kwani fedha hizo zilikuwa akiba yangu yote niliyojinyima wakati nikiwa mwanafunzi.

Nimejaribu kutafuta ushauri wa kisheria ili kuchukua hatua za kumpoti Polisi au kufungua shauri, na sasa naomba msaada wa mamlaka husika na jamii ili niweze kurudishiwa fedha zangu zote na haki yangu ipatikane.
 
😀 😀 😀 😀 Biashara za utumwa hizo , watu wanapigwa kinoma noma ...Tulia sasa , wengine kazi kudanganya wenzao eti kuna ajira nje , wabongo kwa kupenda udalali.

Ushauzwa hapo , hifadhi namba zake za simu kama umepewa fake basi mswalie Mtume.!
 
11m unatoa uajiriwe kazi na umesoma my sister? Surely hata wewe kwel unajiskia?

My friend, 11m ukakosa kuzifanyia kaz ukahonga na sasa unalalamika kweli mdogo wangu sijui mkubwa wangu! Hayo ndio madhara ya kupenda kitonga sasa.

Anyway pole sana. Hiyo pesa hata ungesema unaizungusha kwa sasa ungekuwa na hela nzuri tu. Kimekulamba
 
11m unatoa uajiriwe kazi na umesoma my sister? Surely hata wewe kwel unajiskia? My friend 11m ukakosa kuzifanyia kaz ukahonga na sasa unalalamika kweli mdogo wangu cjui mkubwa wangu! Hayo ndio madhara ya kupenda kitonga sasa. Anyway pole sana. Hiyo pesa hata ungesema unaizungusha kwa sasa ungekuwa na hela nzuri tu. Kimekulamba
Invoice kama za wale jamaa wa kutuma mzigo , halafu wanakuambia umeishia kenya so utume pesa ili utumwe JNIA , 😀 😀 😀
 
Nchi hii utapeli kila kona, nafikiri tatizo ni kwa sababu huenda wana mianya mingi ya kukwepa kushughulikiwa kisheria au ugumu wa michakato ya kisheria kushughulikia matukio ya kitapeli.

Pole.
 
11m unatoa uajiriwe kazi na umesoma my sister? Surely hata wewe kwel unajiskia? My friend 11m ukakosa kuzifanyia kaz ukahonga na sasa unalalamika kweli mdogo wangu cjui mkubwa wangu! Hayo ndio madhara ya kupenda kitonga sasa. Anyway pole sana. Hiyo pesa hata ungesema unaizungusha kwa sasa ungekuwa na hela nzuri tu. Kimekulamba
Inasikitisha sana, na elimu yake ila kimemulamba duh!
 
Invoice kama za wale jamaa wa kutuma mzigo , halafu wanakuambia umeishia kenya so utume pesa ili utume JNIA , 😀 😀 😀
watu wengne cjui wanaishi dunia gani ndugu yangu. Mim hata kama ni mkopo nahitaji afu uniambie nitangulize pesa ndo unipe mkopo kaa nao au ukate kiasi unachotaka then unipe hizo zingne then tupigiane hesabu sasa. Kwel nitoe 11m ati ni ajira afu mwisho wa siku nipate kaz ya kulipwa 2m hapo kwel hizo hesabu zinaingia hata kwa mtu ambaye hajasoma? Huyu angekuwa karbu na mimi na huu upuzi ningemfunga na kamba niite ambulance maana sio kwa akili hizo
 

Nyie mnaoitwa Anonymous guest thread zenu mnazingua kweli wewe umetapeliwa mil 11.2 yule mwenzako mwingine ametimuliwa kwenye usaili kisa kavaa jeans na kapelo,kuna mmoja nae kaachwa airport kisa alikuwa anamalizia kula.​

 
Sikulaumu na sitapenda uchukulie kama tusi, kejeli au dhihaka. 11m kama umeshindwa toboa Tz basi hata huko ulikotaka kwenda ungerudi na lugha tu! Wengine hapa hapa kwenye umri huo ambao upo na pesa kiasi kidogo tu biashara mnazoita zakichuuzi zilituinua
 
11m unatoa uajiriwe kazi na umesoma my sister? Surely hata wewe kwel unajiskia? My friend 11m ukakosa kuzifanyia kaz ukahonga na sasa unalalamika kweli mdogo wangu cjui mkubwa wangu! Hayo ndio madhara ya kupenda kitonga sasa. Anyway pole sana. Hiyo pesa hata ungesema unaizungusha kwa sasa ungekuwa na hela nzuri tu. Kimekulamba
Upo sahihi sana mkuu, kama mtu ameshindwa kuizungusha 11m ikamletea manufaa, hela ataishia kuiona kwa wenzie endapo hata badili akili yake
 
Back
Top Bottom