Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Mkurugenzi wa Kampuni ya Almasi, Gift Ngowi, amesema kampuni hiyo imepata fursa ya kushiriki katika utoaji wa huduma za picha, video, kurekodi na kurusha mubashara shughuli mbalimbali za Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika jijini Arusha.
Ngowi amesema kampuni hiyo ilipata zabuni ya kutoa huduma hizo kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), ambapo ilihusika katika kuratibu na kusambaza maudhui ya mkutano huo katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali, katika kipindi chote cha mkutano kulikuwa na zaidi ya vikao 70 vilivyohitaji huduma za kitaalamu za picha na video, pamoja na kurekodi na kurusha matangazo mubashara ili kuwezesha shughuli hizo kuwafikia watu kupitia majukwaa mbalimbali.
Ameongeza kuwa kuendelea kufanyika kwa mikutano mikubwa nchini kunafungua fursa kwa kampuni za Kitanzania kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali kukuza vipaji vya vijana na kuongeza uzoefu wao katika sekta ya habari, teknolojia na uzalishaji wa maudhui.