KERO Kampuni Star Employment Service TZ nirejesheeni 11.2M nilizowapa mnitafutie ajira nje

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Invoice kama za wale jamaa wa kutuma mzigo , halafu wanakuambia umeishia kenya so utume pesa ili utume JNIA , 😀 😀 😀
Ndugu yangu wa kike aliambiwa mzigo wake umetumwa Airport Zanzibar. Akawa anahangaika kutafuta hela ya kutuma ili aletewe mzigo. Rafiki yake alinisanua, ikabidi nimuambie kuwa upo ktk process za kutapeliwa....akawa anabisha sababu anadai jamaa yake 'Mzungu' wamekutana mtandaoni siku nyingi ndiye aloyemtumia huo mzigo wa laptop, iphone na dollar kadhaa. 😀 Na picha ya mzigo ulivyofungwa akanionesha. Nikamwambia ingia mtandaoni e.g JF halafu andika neno 'UTAPELI' kisha soma nyuzi moya baada ya nyingine....
 
Sasa hiyo milion 11 si ndio ulikuwa mtaji wako we umampa mtu akutaftie kazi🤣🤣🤣🤣
 
Pole sana

Wakuu baada ya kumuelekeza nini afanye ili kùmsaidia ndugu yetu tumeishia kumnanga tu
ndugu yangu huyu hata sio wa kusaidiwa ni wa kupiga viboko afu achangiwe hela afanyiwe upasuaji wa kumbadilishia kichwa maana ni kama kilijazwa funza badala ya elimu. Kweli na usomi wote wa kusomea nje ya nchi anaingizwa mkenge hivyo.
 
Yani kama ungekuwa ni ndugu yangu ningekupiga mingumi Hadi uzimie ili ukizinduka useme kuwa ulikuwa unaota na sio kweli Yani badala ungemhonga hata boyfriend wako yule winga wa kariakoo afungue goli lake wewe unatapeliwa
 
Kosa lako kubwa kuliko yote ilikuwa ni kukubali kurudi Tanzania, naamini haukuomba ushauri kwa watu wenye experience. Dunia ya sasa hakuna ulazima wa physical presence ili ufanikishe jambo lako, your naiveté has costed you big time.
 
Pole sana kuna jamaa yangu nae anakwenda kutapeliwa muda si mrefu. Kuna maagent wamemuahidi atapata kazi ya mshahara mnono ya Denmark malazi bure. Jamaa hashauriki tumeamua kukaa kimya damu zimtoke masikioni. Kuna hela keshatoa napambana kutafuta kiasi kilichobaki.
 

Ungejiongeza kwa kuwasiliana na waajiri kibao moja kwa moja dunia hii ya TEHAMA, au hata kuvuka border kwenda kutafuta badala ya uvivu wa kusubiri kuunganishiwa

Kwa uandishi wako unaonekana una elimu ya kutosha, imebakia kujiongeza

Cheki video za watu wa zamani wazee wetu walivyojiongeza walipokuwa na ajira nchini Tanzania na akiba ya fedha kiasi kama chako walivyochukua maamuzi bila woga ...

Exclusive Interview with msomi Ahmed Ally Manyuka
View: https://m.youtube.com/watch?v=EwxrFJE-bYE safari yake ya kuondoka Tanzania na kwenda kutafuta maisha nje ya nchi, changamoto alizokutana nazo, na sababu zilizomfanya aamue kurejea nyumbani.

WAHENGA NA ADVENTURE ZAO, SOMO TOSHA KWA KIZAZI CHETU CHENYE TEHAMA KIGANJANI
Kutoka ndoto za maisha bora ughaibuni hadi uhalisia wa changamoto za ugenini, Salim anafunguka bila kificho kuhusu uzoefu wake akiwa baharia, maisha ya nje ya nchi, na maamuzi magumu aliyopitia. Je, maisha ya nje ni rahisi kama wengi wanavyodhani? Ni nini kilimrudisha Tanzania?

View: https://m.youtube.com/watch?v=WRtWjISvCes
 
Angeizungusha kwenye nini? Msipende kurahisisha mambo. Kuna watu laki moja tu anatoboa na wengine hata awe na 200m hatoboi
 
Pascal Mayalla natumaini atakusaidi
 
Watu weusi kuaminika bado ni changamoto, kila sehemu ni shida; wenzetu wazungu kwenye uaminifu wametuzidi. Unaweza ukakopa fedha bank zetu leo na ukarudisha mkopo wote, lakini bado wakaendelea kukukata.
Cha kufanya, tafuta ofisi yoyote ya wakili anayejitegemea, ili aweze kukupa utaratibu wa kisheria ili kufaniisha hitaji lako.​
 
Angeizungusha kwenye nini? Msipende kurahisisha mambo. Kuna watu laki moja tu anatoboa na wengine hata awe na 200m hatoboi
acha kujfanya kondoo na wewe nisikuunganishe na yeye. Kwel unaamin hata wewe angekosa cha kufanya na hiyo hela. Na umesema vzui kuna watu wanatoboa hata kwa laki, je kwa nin yeye asiwe huyo wa laki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…