KERO Kampuni Star Employment Service TZ nirejesheeni 11.2M nilizowapa mnitafutie ajira nje

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna jamaa hapa aliona mzigo umeandikwa jina lake, namba yake ya simu , ndani kuna dollar, laptop na iphone , nikamkanya ..Akaanza kuniamba , wewe mtanga haupendi maendeleo ya watu na kunikejeli juu, nikamuacha maana nilimuelewesha , akaambiwa atapigiwa simu mzigo ukifika.

Ila alipigwa kama laki tano hivi 😀 😀 😀.
 
Nakuamini yaani hata biashara za mtandao tumefeli sana .
 
acha kujfanya kondoo na wewe nisikuunganishe na yeye. Kwel unaamin hata wewe angekosa cha kufanya na hiyo hela. Na umesema vzui kuna watu wanatoboa hata kwa laki, je kwa nin yeye asiwe huyo wa laki
Mkuu kifupi ni kuwa siyo kila mmoja anaweza zungusha pesa na kutoboa. Wengine toka wanazaliwa wanawaza kuajiriwa tu. Kuzungusha pesa na ikazaa hicho ni kipaji au experience ambayo siyo kila mtu anayo. Wasaafu wengi wameishia wapi babaya sana baada ya kupata mafao yao na kujiingiza kwenye mambo ambayo hawana uzoefu nayo
 
na ndio maana ntazd kusema kuwa hana akili coz yeye akili yake ilkuwa kwene ajira na matokeo yake ndio hayo sasa. Mda mwingne mtu anafeli kwa kupenda mteremko ndugu yangu. Tatizo hata sio kukosa biashara ya kufanya no, ni pale uhonge ili upate kazi na umesoma tena nje ya nchi ndugu yangu hata wewe kweli inakuingia akilini. 11m ushindwe kutoboa tz utarajie utatoboa kwingne ndugu yangu hizo n ndoto
 
Nje ya nchi ulikuwa intern au? Pili unalipa pesa ya mtaji ili utafutiwe ajira huko huko Ujerumani uliokuwa akili zako zipo sawa kweli?
 
Aisee kobaz tulikuwa mbele ya muda
cc loose Nut Busu la Kenge


View: https://www.youtube.com/watch?v=B7E_I8FXLcg
 
Tatizo la wanawake ni uvivu na kuamini haraka, hata ukifuatilia sahv biashara nyingi za online wateja wengi ni wanawake, yani hawapendi kuhangaika kabisa na huamini kwa haraka sana, nafkiri pia nature yao ndo inachangia

Tukurudi kwa huyu muhanga wetu, nimejaribu kufikiria nje ya box inawezekana plans zake kubwa ilikua ni kuishi nchi za nje mazima, so akaona atafute ajira ya kueleweka ndo ameingia kwenye huo mkenge

Huko mtaani kwao sahv watakua washaanza kumuuliza kwann haolewi na umri unazidi kwenda? + akifikiria na 11.2m alizopoteza kijinga basi anazidi kuchanganyikiwa
 

Nyie mnaoitwa Anonymous guest thread zenu mnazingua kweli wewe umetapeliwa mil 11.2 yule mwenzako mwingine ametimuliwa kwenye usaili kisa kavaa jeans na kapelo,kuna mmoja nae kaachwa airport kisa alikuwa anamalizia kula.​

Na wana ushahidi wa kweli kabisa ni hawa hawa wanaokua wakali na kutukana tukiwaambia jambo wakipigwa wanakuja na Anonymous guest huyu kama alienda Germany hata huko alienda kwa mfumo huo huo na mbaya zaidi kama anaweza kutoa pesa ujue wahuni wanaweza kumpitia hata yeye na huku wakijua kazi hakuna..
 
Daah labda wamsumbue tu polisi kosa ulilifanya ukiwa Germany maana ulituma pesa ukiwa ardhi ya Ujerumani kesi ifunguliwe Germany uwatumie Interpol ndio wahusike nae hapo hilo litawezekana kwa kutumia kitengo chao makao makuu yao Dodoma..
Kulikua na kesi inafanana na utapeli huo jamaa akiwa Tanzania aliwatumia jamaa matapeli wa mtandaoni Tsh 53m akitaka kununua trekta baada ya kutapeliwa ndio akanitafuta mimi ili nimsaidie uzuri nilikua Pretoria kipindi hicho nikaenda hapo Makao makuu ya Interpol SA wakaangalia nyaraka wakasema jamaa katuma hela kwenye ardhi ya Tanzania afungue kesi huko tumtafutie wezi wake na kwenye vituo vyao walikataa kufungua kesi vile vile na mzala kwa majibu hayo akasamehe hela na alikuja kwangu akitaka ushauri wa hela ya Bima wahuni walitaka awaongezee ndio nikamwambia hao ni matapeli usitume chochote baada ya muda kukaa akagundua wahuni wameenda na hela mpaka kesho kapoteza hiyo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…