Kampuni ya Apple kutouza bidhaa zake Urusi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1646209519806.png

Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine.

Wafanyabiashara wengine wakubwa wa teknolojia kama Google na Twitter pia wamepunguza biashara zao nchini Urusi ‘tunaungana na wote wanaotaka amani duniani’ imeeleza taarifa ya Apple.

Pamoja na kusitisha uuzaji wa bidhaa, Apple inasema duka lake la programu za simu linazuia upakuaji wa RT News na Sputnik News kutoka nje ya Urusi zikiituhumu mitandao hiyo kuwa inarusha habari za propaganda kutokea Ofisi za Serikali ya Urusi.

Apple pia imesitisha kutuma location za moja kwa moja kwenye ramani za Apple nchini Ukraine kama hatua ya usalama, sawa na hatua ambayo tayari Google imechukua.
 
Wakati marekani ilipovamia Sirya Libya Afaghanistani Iraq hao Apple walikuwa likizo?

Russia inajitosheleza kwa kila kitu acheni kuweweseka
 
Wasiuze tu kwani wao ndio MUNGU pumbavu sana. Marekani anajiona mungu sana fala huyu. Yeye kuwawekea wenzake vikwazo ila sio yeye kuwekewa vikwazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine...
Apple nyambafu sana wakati dunia inashughudia maangamizi Itaq syria Linya na Afghanstan walikua wanaona ni sawa?

Kwa mwenendo huu ni kujitia kitanz kwa kampuni za ulaya na marekani sasa nchi nyingi zitaweka juhudi kwenye kuunda teknolojia zao mbadala ili kuondokana na huu upuuzi
 
Putin anaendelea kupata mapigo kote, na Warusi wengi ukiingia kwenye mitandao yao wamenza kumchukia na sio muda mrefu watamgeuka hali ikizidi kuwa ngumu.
Dunia iendelee kumpa vikwazo vya kila aina. Pakistan alishasema hatomlipa madeni yake, asusiwe na wote....
 
Hahaha sasa mbona kama Pakistan katafuta upenyo wa kutolipa madeni?
 
Yeye kaanzisha, wengine wanacheck kwa mbali kama atafanywa chochote, Putin akimpotezea na wao pia watasema hawalipi.
 
Russia hataweza kustahimili haya mapigo na mwisho wa siku ataomba poo kwani hakuna nchi inayoweza kuishi kama kisiwa. Wananchi wa Russia tayari wameshaanza kapanga foleni kununua bidhaa kama ilivyokuwa wakati wa USSR. Ruble imeshapoteza asilimia 30 ya thamani yake.
 
Hivi hadi sasa kuna kauli yoyote kutoka kwa putin
 
Russia hataweza kustahimili haya mapigo na mwisho wa siku ataomba poo kwani hakuna nchi inayoweza kuishi kama kisiwa. Wananchi wa Russia tayari wameshaanza kapanga foleni kununua bidhaa kama ilivyokuwa wakati wa USSR. Ruble imeshapoteza asilimia 30 ya thamani yake.
Mkuu vikwazo vinapiga kote kote, aliewekewa anaumia na alieweka anaumia.
 
Mataifa ya k'islam yanapigwa kila siku hamsemi lolote utafikir huko wanauwa mbuzi...

Makafir wanafk sana.
 
Wakati marekani ilipovamia Sirya Libya Afaghanistani Iraq hao Apple walikuwa likizo?

Russia inajitosheleza kwa kila kitu acheni kuweweseka
Mkuu Apple ni kampuni kutoka nchi gani? Je kuna kampuni yoyote ya kutoka Urusi iliyoacha kuiuzia Urusi bidhaa yake kwa sababu imeivamia Ukraine? Kama jibu ni hapana basi umeshapata jibu la swali lako kama Apple walikuwa likizo ama lah
 
Wasiuze tu kwani wao ndio MUNGU pumbavu sana. Marekani anajiona mungu sana fala huyu. Yeye kuwawekea wenzake vikwazo ila sio yeye kuwekewa vikwazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hata Tanzania mnaweza kumwekea Marekani vikwazo, yeye hazuii nchi yoyote kumwekea vikwazo. Wew weka kama unao uwezo wa kuishi bila yeye.
 
Back
Top Bottom