Kampuni ya Askari Metals iliyopata kibali uchimbaji wa Urani Dodoma kupitia Eyasi Uranium Project inamilikiwa na nani?

State Propaganda

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2024
Posts
542
Reaction score
1,286
Kampuni hiyo ya Askari Metals kupitia kampuni yake tanzu ya tanzania ujulikanayo kama Infinum Uranium so far tunaweza kusema imekwisha pata "baraka" zote za uwekezaji kutoka serikali ya SSH.

Kwa kuanza, kampuni hiyo itafanya utafiti wa sampuli za miamba na geographia kabla ya kuanza uchimbaji katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mramba 292 lililopo kilomita 320 magharibi mwa mkoa wa Dodoma.

Ningependa kujua mmiliki/wamiliki wa kampuni hii maana madini haya ya Urani (Uranium) sio kama madini mengine amabayo tumezoea kuona yakichimbwa nchini.

Na hii ndio mara ya kwanza kwa taifa letu tokea yagunduliwe ndii yanaenda kuanza kuchimbwa.

Madini ya uranium katika ulimwengu wa sasa ni 'lulu' kwani huweza kutumika katika uzalishaji wa nishati ya umeme kupitia vinu vya nyuklia au hata pia katika kutengeneza silaha za maangamizi kama mabomu ya nyuklia.

Hali kadhalika, kama uchimbaji wake hautazingitia utaratibu maalum wa kisanyansi, hatari ya uchafuzi wa kimazingiria na maafa makubwa kwenye ikolojia yanaweza kutokea na kuleta madhara makubwa vizazi na vizazi.

Chanzo

tuweke rekodi sawa....kuna sehemu ndani ya hifadhi ya mwalimu nyerere likuyu, namtumbo, ruvuma, mpaka plant wameshajenga warusi...now watakua wanachimba mdogo mdogo inaondoka...hawa warusi hadi hapo dodoma walishafika...rosatom ya urusi ndo inamiliki vitalu vingi vya hayo madini hapa tanzania.
 
Back
Top Bottom