Kampuni ya Barick imeshindwa kulipa Wakandarasi, wazabuni na mafundi walitekeleza miradi ya ujenzi wa Madarasa, Mabweni na Vyoo katika shule t nchini

kijana wa leo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2011
Posts
2,921
Reaction score
7,173
Mnamo mwezi wa nne mwaka 2024, Kampuni ya kuchimba madini ya Barick walitoa barua kupitia wizara ya TAMISEMI kuwataarifu juu ya kufadhili ujenzi wa madarasa, mabweni na vyoo katika shule mbalimbali nchini. Serikali kupitia kwa wakuu wa shule na wakurugenzi wa halmashauli zote zilizopokea barua hizo, wakaandaa mchakato wa zabuni na kuwapata wakandarasi, local fundi pamoja wazabuni. Baada ya mchakato wa manununuzi kukamilika na mikataba kusainiwa, moja ya condition ya hii mikataba ni kwamba mkandarasi, fundi au mzabuni ni kuanza kazi kwa pesa zao bila malipo ya awali kwa makubaliano kwamba kazi ikifika stage fulani kunakua na malipo.
Sasa ndugu zangu, wakandarasi, wazabuni na mafundi wazalendo wakatumia pesa zao na wengi wao kutumia mikopo kutekeleza miradi hiyo, lakini kitu cha kushangaza watu wamemaliza au kufikia stage ya malipo kwa mujibu wa mikataba toka mwezi wa saba na wa nane mwaka 2024 ila hadi leo mwezi February hakuana mtu yeyote aliyelipwa hata senti tano na mbaya zaidi hakuna majibu yoyote yanayoeleweka kutoka kwa wahusika.
Ndugu zangu hili jambo linasikitisha sana na kutia hasira, tunaiomba serikali isaidie hawa wakandarasi, wazabuni na mafundi wazawa wapate malipo yao ambayo ni haki yao, mana ni kama Barick inatumika kuhujumu nguvu kazi ya taifa.
Inasikitisha sana, watu wanaugua hadi magonjwa ya pressure kutokana na kutolipwa malipo ya pesa waliyowekeza, na mbaya zaidi na TRA nao wanadai kodi mana wakati wa kudai malipo Barick walitaka risiti za machine.
Hili swala linasikitisha sana, serikali isaidie watu wake.
 
Pesa itakuwa imepewa serikali, Barrick hawezi kulipa wakandarasi direct.
Hii ni tofauti, form zote za malipo zilitolewa na Barick na serikali kazi yao ni kuidhinisha tu wao Barick wanafanya malipo directly........
 
serikali imesha kula hiyo pesa, halafu kukopa ili ufanye deal na miradi ya jamii hiyo ni zaidi ya suicide mission ambayo kutoboa ni maajabu.
 
Hii ni tofauti, form zote za malipo zilitolewa na Barick na serikali kazi yao ni kuidhinisha tu wao Barick wanafanya malipo directly........
Shida mwenye mradi ni serikali, yeye barrick ana weza toa pesa, ila serikali Ina weza sema hawa tuna wajua mki wapa hela hawafanyi kazi.

Hivyo hizo hela tupeni sisi, ili tuwa peleke kwa style tunayo ona sawa.
 
serikali imesha kula hiyo pesa, halafu kukopa ili ufanye deal na miradi ya jamii hiyo ni zaidi ya suicide mission ambayo kutoboa ni maajabu.
Wakati wanaitangaza, wanakuhakikishia hii miradi pesa yake ipo ndo mana Barick wanalipa direct, lakini siamini kama serikali ilishalipwa mana Barick wangetoa hayo majibu, mana kwa sasa lawama zote ni kwa Barick
 
Shida mwenye mradi ni serikali, yeye barrick ana weza toa pesa, ila serikali Ina weza sema hawa tuna wajua mki wapa hela hawafanyi kazi.

Hivyo hizo hela tupeni sisi, ili tuwa peleke kwa style tunayo ona sawa.
Daaah ikiwa hivo ni shida sana, mana watu wote wameshafanya sehemu kubwa ya hiyo miradi na wengine wamemaliza kwa asilimia 💯 kwa kutumia pesa zao
 
Tatizo hapo litakuwa ni aina ya kiwango ambacho kimejengwa kwenye hiyo miradi.
Tunaijua sifa kubwa ya wakandarasi wazawa nayo ni upigaji.
Barrick kama wao....janja janja huwa haina nafasi.Halafu nikushairi ufuatilie huko kwa wahusika badala ya kuja huku kwa Maxence Mello!
 
Wakati wanaitangaza, wanakuhakikishia hii miradi pesa yake ipo ndo mana Barick wanalipa direct, lakini siamini kama serikali ilishalipwa mana Barick wangetoa hayo majibu, mana kwa sasa lawama zote ni kwa Barick
huyo mhasibu au mtekeleza majukumu upande wa barrick aki pewa asilimia 30 ya pesa, halafu aka ambiwa akae kimya.

Nyie mta piga kelele, ila wao Hawana Cha kusema maana Wana elewa what's going on .
 
Daaah ikiwa hivo ni shida sana, mana watu wote wameshafanya sehemu kubwa ya hiyo miradi na wengine wamemaliza kwa asilimia 💯 kwa kutumia pesa zao
Iko Barrick kamwe haiwezi fanya uhuni wa aina yoyote hawa jamaa wako streight mno na pesa ipo siyo ya kuuliza.

Nakupa mfano.
Miaka ya nyuma barabara zile za vumbi kutoka kakola mgodini hadi nyamtukuza kwenye machine zao za ku-pump maji na kutoka kakola hadi Ilogi kama sio zaidi ya hapo zilikuwa zinatengenezwa na mgodi na utakubaliana nami njia ile kupita No9,bumanda,karumwa hadi nyamtukuza kwenye source ilikuwa nzuri na inapitika kwa urahisi japo ya vumbi.

Miaka ya 2010+ wahuni (serikali) ikasema hela zote za bajeti ya barabara iwe inapewa halimashauri na halimashauri ndo inafanya ukarabati wa barabara Barrick wakaanza kufanya hivyo. Nakwambia kwa sasa barabara ilivyo sina haja ya kuelezea hapa japo nikuambie tu kuwa wakati wa masika unaweza panda mpunga wako katikati ya barabara hadi ukaivisha au ukafuga samaki bila shida yoyote ile.

Soma hapa
 
Wakati wanaitangaza, wanakuhakikishia hii miradi pesa yake ipo ndo mana Barick wanalipa direct, lakini siamini kama serikali ilishalipwa mana Barick wangetoa hayo majibu, mana kwa sasa lawama zote ni kwa Barick
Barrick hawanaga show mbovu kwenye malipo uliza contractors wao wooote kama kuna siku wamelilia malipo, changamoto ni serikali kuweka mkono wake, ukute serikali ilishalipwa na ndiyo maana Barrick wako kimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…