kijana wa leo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2011
- 2,921
- 7,173
Mnamo mwezi wa nne mwaka 2024, Kampuni ya kuchimba madini ya Barick walitoa barua kupitia wizara ya TAMISEMI kuwataarifu juu ya kufadhili ujenzi wa madarasa, mabweni na vyoo katika shule mbalimbali nchini. Serikali kupitia kwa wakuu wa shule na wakurugenzi wa halmashauli zote zilizopokea barua hizo, wakaandaa mchakato wa zabuni na kuwapata wakandarasi, local fundi pamoja wazabuni. Baada ya mchakato wa manununuzi kukamilika na mikataba kusainiwa, moja ya condition ya hii mikataba ni kwamba mkandarasi, fundi au mzabuni ni kuanza kazi kwa pesa zao bila malipo ya awali kwa makubaliano kwamba kazi ikifika stage fulani kunakua na malipo.
Sasa ndugu zangu, wakandarasi, wazabuni na mafundi wazalendo wakatumia pesa zao na wengi wao kutumia mikopo kutekeleza miradi hiyo, lakini kitu cha kushangaza watu wamemaliza au kufikia stage ya malipo kwa mujibu wa mikataba toka mwezi wa saba na wa nane mwaka 2024 ila hadi leo mwezi February hakuana mtu yeyote aliyelipwa hata senti tano na mbaya zaidi hakuna majibu yoyote yanayoeleweka kutoka kwa wahusika.
Ndugu zangu hili jambo linasikitisha sana na kutia hasira, tunaiomba serikali isaidie hawa wakandarasi, wazabuni na mafundi wazawa wapate malipo yao ambayo ni haki yao, mana ni kama Barick inatumika kuhujumu nguvu kazi ya taifa.
Inasikitisha sana, watu wanaugua hadi magonjwa ya pressure kutokana na kutolipwa malipo ya pesa waliyowekeza, na mbaya zaidi na TRA nao wanadai kodi mana wakati wa kudai malipo Barick walitaka risiti za machine.
Hili swala linasikitisha sana, serikali isaidie watu wake.