Kampuni ya betika ni halali kweli au matapeli?

Kampuni ya betika ni halali kweli au matapeli?

NOKIALUMIA

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
396
Reaction score
278
Ndugu zangu, hasa wale wanacheza michezo ya kubahatisha, kampuni hii ya Betika ni matapeli lakini Bodi ya Bahati Nasibu bado ina wacheki tu.

1. Kampuni inaruhusu kudeposit tu! Hata milioni we deposit ila kutoa hela hairuhusu hata siku moja.

2. Hairuhusu withdraw yoyote ile hivyo ukiweka fedha hata ukachezaa ujue huwezi kuitoa hata iwe elfu moja haitoki inabaki kwao. Wanakupa wanavyotaka wao ukipiga utaskia subiri tu utaingia siku yoyote ile (non sense).

3. Poor customer care, ukipiga tu simu wanakudanganya, halafu wanakuwa wakali ukionesha kutoelewa jibu fulani.

4 . Wanamasoko mazuri ili wakukamate.

Kuwen makini

Serikali iingiilie kati hawa ni DECI MPYA
 
Ujinga wenu kudhania mtatoka kwa michezo ya kamali; hakuna hata siku moja utakuja fanikiwa bila kufanya kazi na eti ukategemea hiyo michezo!!! Utapewa tamaa tu kuwa siku moja utakuja pata JACKPOT na hiyo siku haitakuja kamwe!!! Zinduka acha ujinga wa kuwatajirisha matapeli.
 
Ndugu zangu, hasa wale wanacheza michezo ya kubahatisha, kampuni hii ya Betika ni matapeli lakini Bodi ya Bahati Nasibu bado ina wacheki tu.

1. Kampuni inaruhusu kudeposit tu! Hata milioni we deposit ila kutoa hela hairuhusu hata siku moja...
Michezo yote ya kubeti ni wizi wa kawaida. Ushaambiwa ni michezo ya kubahatisha japo hawataki kusema ukweli ni ya kubabaisha. Hakuna cha utapeli au nini wote ni wezi tu
 
Ujinga wenu kudhania mtatoka kwa michezo ya kamali; hakuna hata siku moja utakuja fanikiwa bila kufanya kazi na eti ukategemea hiyo michezo!!! Utapewa tamaa tu kuwa siku moja utakuja pata JACKPOT na hiyo siku haitakuja kamwe!!! Zinduka acha ujinga wa kuwatajirisha matapeli.
mbona hua tunashinda sasa mindset zako ni za hovyo kweli 😂😂
 
Sio kila anayecheza kamari hana kazi ndugu acha kukariri..
 
Mkuu nipo nao office moja hapa makumbusho jengo linaitwa "derm plaza "

Kama upo serious kabisa njoo inbox tuwapandie juu .....

Wanapaki nje hapa magari yao na matisheti ya betika kumbe hawana uwezo wa kulipa mtu akila .....

Nicheki tukawawashie Moto ....najuana na customer wao mmoja ni mhindi bonge harafu bitozi ,msela ,mhuni ,anavuta sigara hatari .......
 
mbona hua tunashinda sasa mindset zako ni za hovyo kweli 😂😂

Wewe mbwiga kwa ujumla wenu wacheza kamali mgekuwa mnashinda; hawa matapeli wangekwisha funga hayo maduka yao kwani wangekuwa wanapata hasara!! Serikali inawaruhusu hawa matapeli kuwafilisi wananchi na kutorosha fedha nje ya nchi kwa kuamini kuwa eti wanapata kodi!! Hiyo kodi wanayopata is insignificant ukifananisha na jinsi Wananchi wanavyofukarika na jinsi haya maduka ya kamali yanavyotumiwa kutorosha fedha ambayo ingetumika hapa nchini!!
 
Ujinga wenu kudhania mtatoka kwa michezo ya kamali; hakuna hata siku moja utakuja fanikiwa bila kufanya kazi na eti ukategemea hiyo michezo!!! Utapewa tamaa tu kuwa siku moja utakuja pata JACKPOT na hiyo siku haitakuja kamwe!!! Zinduka acha ujinga wa kuwatajirisha matapeli.
Jadili hoja mkuu.

Kamari ipo na itakuwepo na wa kubeti atabeti.

Hatuwezi kufanana mtazamo Wala kuwaza kunakofanana. Ndivyo maisha yalivyo.

Kumbuka kuna watu wanasomesha watoto na kujenga kwa kamari. Wengine Ni kazi.
 
Ninatoa tahadhari hii out of the experience niliyoiona kwa Afisa mstaafu mmoja wa shirika kubwa sana nchini aliyekuwa na nyumba TATU huko Oysterbay, Masaki na Mbezi beach. Huyu bwana baada ya kustaafu akaanza kushinda kwenye hizo kamali zenu na mwishowe akaishia kuuza nyumba zote na baadae kufa kihoro!!!! You become addicted halafu unasema wengine ni kazi; sio kazi ni ugonjwa!!!
 
Wewe mbwiga kwa ujumla wenu wacheza kamali mgekuwa mnashinda; hawa matapeli wangekwisha funga hayo maduka yao kwani wangekuwa wanapata hasara!! Serikali inawaruhusu hawa matapeli kuwafilisi wananchi na kutorosha fedha nje ya nchi kwa kuamini kuwa eti wanapata kodi!! Hiyo kodi wanayopata is insignificant ukifananisha na jinsi Wananchi wanavyofukarika na jinsi haya makuka ya kamali yanavyotumiwa kutorosha fedha ambayo ingetumika hapa nchini!!
Ni wivu tu
 
Kwanza kamli Dhambi
Ni kweli bhna kamali ni dhambi [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Hio ni account yangu ya sport pesa
Screenshot_20211202-011608.jpg
 
Back
Top Bottom