Kampuni ya China Tanzania Security yafafanua madai ya Walinzi wa Vituo vya Mwendokasi kutolipwa mishahara ya miezi mitatu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinst.app_12558267_946209818803396_1698594827_n_1080.jpg
Uongozi wa Kampuni ya China Tanzania Security umetoa ufafanuzi kuhusu madai ya Mwanachana wa JamiiForums.com aliyeandika kuwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambao ni Walinzi wanaosimamia Vituo kadhaa vya Usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi mitatu na kuwa wakidai hawapati majibu ya kueleweka.

Mwanachama huyo alieleza kuwa mbali na hali hiyo kumekuwa na changamoto nyingine mbalimbali ikiwemo Wafanyakazi kutosikilizwa na kutojaliwa inapotokea wanapata changamoto wakiwa kazini.

Kusoma zaidi alichoandika Mdau huyo, bonyeza hapa ~ Walinzi tunaosimamia Vituo vya Mwendokasi hatujalipwa mshahara kwa miezi mitatu, tukifuatilia tunapigwa danadana

Ufafanuzi wa CHINA TANZANIA SECURITY
Administration Officer wa Kampuni hiyo, Pascal Temba amezungumza na JamiiForums na kufafanua hoja zilizowasilishwa na Mdau kwa kusema:

Kuhusu suala la Mshahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu, hiyo inatokana na changamoto ambayo tunapitia ambayo inaweza kutokea katika ofisi yoyote ile.

Suala hilo kwanza halijawahi kutokea huko nyuma nadhani hata kwenu hii itakuwa taarifa ya kwanza kuhusu sisi inayozungumzia mishahara.

Suala la Mikataba siyo kweli kuwa hawana mikataba, yote iliyopo ni Mikataba ya maandishi.

Jambo lingine ni kuwa ofisi inashughulika na changamoto nyingine kadhaa za Wafanyakazi kuanzia mtu mmojammoja, na sio kweli kuwa malalamiko yao hayashughulikiwi sio kweli, naomba niweke vizuri kuhusu hilo.

Pamoja na suala hilo la mishahara lakini masuala ya nidhamu bado yanasimamiwa vizuri, unaweza kukuta kuna mfanyakazi anaanza kukiuka taratibu kwa kutofika kazini, mtu anapochukuliwa hatua za kinidhamu anaweza kwenda mbele na kuzungumza vitu vingine ambavyo havipo.

Pia soma:
~
Walinzi kampuni ya Asgard Security hatujalipwa mishahara kwa miezi miwili, tukifuatilia uongozi unatishia kutufuta kazi

~ Upigaji, utapeli, uliojifichika kwenye kofia ya Kampuni Binafsi za Ulinzi
 
Chura yuko za zake kariakoo kula chakula cha mchana.Sina uwakika kama anaweza kuwackiliza watanganyika.Tena kampuni yenyewe sasa CHINA -TANZANIA.
Lipeni jasho la wafanyakazi wenu!!
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Uongozi wa Kampuni ya China Tanzania Security umetoa ufafanuzi kuhusu madai ya Mwanachana wa JamiiForums.com aliyeandika kuwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambao ni Walinzi wanaosimamia Vituo kadhaa vya Usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi mitatu na kuwa wakidai hawapati majibu ya kueleweka.

Mwanachama huyo alieleza kuwa mbali na hali hiyo kumekuwa na changamoto nyingine mbalimbali ikiwemo Wafanyakazi kutosikilizwa na kutojaliwa inapotokea wanapata changamoto wakiwa kazini.

Kusoma zaidi alichoandika Mdau huyo, bonyeza hapa ~ Walinzi tunaosimamia Vituo vya Mwendokasi hatujalipwa mshahara kwa miezi mitatu, tukifuatilia tunapigwa danadana

Ufafanuzi wa CHINA TANZANIA SECURITY
Administration Officer wa Kampuni hiyo, Pascal Temba amezungumza na JamiiForums na kufafanua hoja zilizowasilishwa na Mdau kwa kusema:

Kuhusu suala la Mshahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu, hiyo inatokana na changamoto ambayo tunapitia ambayo inaweza kutokea katika ofisi yoyote ile.

Suala hilo kwanza halijawahi kutokea huko nyuma nadhani hata kwenu hii itakuwa taarifa ya kwanza kuhusu sisi inayozungumzia mishahara.

Suala la Mikataba siyo kweli kuwa hawana mikataba, yote iliyopo ni Mikataba ya maandishi.

Jambo lingine ni kuwa ofisi inashughulika na changamoto nyingine kadhaa za Wafanyakazi kuanzia mtu mmojammoja, na sio kweli kuwa malalamiko yao hayashughulikiwi sio kweli, naomba niweke vizuri kuhusu hilo.

Pamoja na suala hilo la mishahara lakini masuala ya nidhamu bado yanasimamiwa vizuri, unaweza kukuta kuna mfanyakazi anaanza kukiuka taratibu kwa kutofika kazini, mtu anapochukuliwa hatua za kinidhamu anaweza kwenda mbele na kuzungumza vitu vingine ambavyo havipo.
Walipeni stahiki zao.
 
Kwa kauli ya administrator officer, Kuna uwezekano wakawafukuza hao wafanyakazi walio andamana Kwa kosa la ukosefu wa nidhamu kazini, na wasiwalipe salary Yao.
 
Kampuni za Ulinzi zooote Bongo mizinguo hasa hasa hizi za watu Private yaan kampuni binafsi tu stupid kabisa mishahara hawalipi hapo HR na Mwasibu wanavimba km kampuni ya Baba yao pumbavu, mnachukua hela za walinzi mnaenda kumalizia mijengo yenu huko Goba huku walinzi hamuwalipi pumbavu na ubaya zaidi Walinzi hawana pa kusemea isipokua Mahakama Kuu tu yaan wanatakiwa wapewe elimu kuhusu hilo wakipeleka mahakamani wanalipwa mara 2 ya mishahara yao shenzi kabisa hao pumbavu
 
So technically ni kweli bwana Temba hujalipa mishahara staff wako, tena miezi 2! Kama nimeelewa vizuri, mwezi December na January (kwa mujibu wa majibu yako ) hujalipa mishahara? So Christmas na mwaka mpya watu wamepiga pass ndefu na bado unao ujasiri wa kuja na kujitetea? Interesting. Mmeweza kuona utovu wa nidham wa wafanyakazi lakini hamtaki kujishughulisha na chanzo cha UTOVU wa nidhamu? Strange.
Halafu...., kwamba hadi kampuni za ulinzi nazo tunahitaji from China? Daaa
 
Uongozi wa Kampuni ya China Tanzania Security umetoa ufafanuzi kuhusu madai ya Mwanachana wa JamiiForums.com aliyeandika kuwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambao ni Walinzi wanaosimamia Vituo kadhaa vya Usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi mitatu na kuwa wakidai hawapati majibu ya kueleweka.

Mwanachama huyo alieleza kuwa mbali na hali hiyo kumekuwa na changamoto nyingine mbalimbali ikiwemo Wafanyakazi kutosikilizwa na kutojaliwa inapotokea wanapata changamoto wakiwa kazini.

Kusoma zaidi alichoandika Mdau huyo, bonyeza hapa ~ Walinzi tunaosimamia Vituo vya Mwendokasi hatujalipwa mshahara kwa miezi mitatu, tukifuatilia tunapigwa danadana

Ufafanuzi wa CHINA TANZANIA SECURITY
Administration Officer wa Kampuni hiyo, Pascal Temba amezungumza na JamiiForums na kufafanua hoja zilizowasilishwa na Mdau kwa kusema:

Kuhusu suala la Mshahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu, hiyo inatokana na changamoto ambayo tunapitia ambayo inaweza kutokea katika ofisi yoyote ile.

Suala hilo kwanza halijawahi kutokea huko nyuma nadhani hata kwenu hii itakuwa taarifa ya kwanza kuhusu sisi inayozungumzia mishahara.

Suala la Mikataba siyo kweli kuwa hawana mikataba, yote iliyopo ni Mikataba ya maandishi.

Jambo lingine ni kuwa ofisi inashughulika na changamoto nyingine kadhaa za Wafanyakazi kuanzia mtu mmojammoja, na sio kweli kuwa malalamiko yao hayashughulikiwi sio kweli, naomba niweke vizuri kuhusu hilo.

Pamoja na suala hilo la mishahara lakini masuala ya nidhamu bado yanasimamiwa vizuri, unaweza kukuta kuna mfanyakazi anaanza kukiuka taratibu kwa kutofika kazini, mtu anapochukuliwa hatua za kinidhamu anaweza kwenda mbele na kuzungumza vitu vingine ambavyo havipo.
Wahisani wa maendeleo a.k.a wawekezaji
 
Back
Top Bottom