Magonjwa Mtambuka
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 32,246
- 31,176
Ok 😎Tuipende nchi yetu, hakuna mwingine wa kuiendeleza isipokua sisi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ok 😎Tuipende nchi yetu, hakuna mwingine wa kuiendeleza isipokua sisi
"Kuhusu suala la Mshahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu," Kwa hiyo wafanyakazi wanakula mawe?Uongozi wa Kampuni ya China Tanzania Security umetoa ufafanuzi kuhusu madai ya Mwanachana wa JamiiForums.com aliyeandika kuwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambao ni Walinzi wanaosimamia Vituo kadhaa vya Usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi hawajalipwa mishahara kwa muda wa miezi mitatu na kuwa wakidai hawapati majibu ya kueleweka.
Mwanachama huyo alieleza kuwa mbali na hali hiyo kumekuwa na changamoto nyingine mbalimbali ikiwemo Wafanyakazi kutosikilizwa na kutojaliwa inapotokea wanapata changamoto wakiwa kazini.
Kusoma zaidi alichoandika Mdau huyo, bonyeza hapa ~ Walinzi tunaosimamia Vituo vya Mwendokasi hatujalipwa mshahara kwa miezi mitatu, tukifuatilia tunapigwa danadana
Ufafanuzi wa CHINA TANZANIA SECURITY
Administration Officer wa Kampuni hiyo, Pascal Temba amezungumza na JamiiForums na kufafanua hoja zilizowasilishwa na Mdau kwa kusema:
Kuhusu suala la Mshahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu, hiyo inatokana na changamoto ambayo tunapitia ambayo inaweza kutokea katika ofisi yoyote ile.
Suala hilo kwanza halijawahi kutokea huko nyuma nadhani hata kwenu hii itakuwa taarifa ya kwanza kuhusu sisi inayozungumzia mishahara.
Suala la Mikataba siyo kweli kuwa hawana mikataba, yote iliyopo ni Mikataba ya maandishi.
Jambo lingine ni kuwa ofisi inashughulika na changamoto nyingine kadhaa za Wafanyakazi kuanzia mtu mmojammoja, na sio kweli kuwa malalamiko yao hayashughulikiwi sio kweli, naomba niweke vizuri kuhusu hilo.
Pamoja na suala hilo la mishahara lakini masuala ya nidhamu bado yanasimamiwa vizuri, unaweza kukuta kuna mfanyakazi anaanza kukiuka taratibu kwa kutofika kazini, mtu anapochukuliwa hatua za kinidhamu anaweza kwenda mbele na kuzungumza vitu vingine ambavyo havipo.
Cha ajabu Jeshi la Polisi na Wiraza ya Ulinzi wanaosimamia na kuratibu hizo kampuni ziweze kufanya kazi inavystahiri hukuti wakizungumzia sababu wanaosimamia na wamiliki ni watu wao ambao moja kwa moja wanahusika na Serikali"Kuhusu suala la Mshahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu," Kwa hiyo wafanyakazi wanakula mawe?
Wamezingua sana, watu wanapenda kuchukulia poa sana watuUnamlazaje mtu miezi miwili bila mshahara! Waache kujitetea wakalipe mishahara! Miezi miwili mfanyakazi anakula nini??? Unaweza kuta mshahara wenyewe ni 250k! Ni mambo ya ajabu sana
So technically ni kweli bwana Temba hujalipa mishahara staff wako, tena miezi 2! Kama nimeelewa vizuri, mwezi December na January (kwa mujibu wa majibu yako ) hujalipa mishahara? So Christmas na mwaka mpya watu wamepiga pass ndefu na bado unao ujasiri wa kuja na kujitetea? Interesting. Mmeweza kuona utovu wa nidham wa wafanyakazi lakini hamtaki kujishughulisha na chanzo cha UTOVU wa nidhamu? Strange.
Halafu...., kwamba hadi kampuni za ulinzi nazo tunahitaji from China? Daaa