Kampuni ya China yaanzisha kiwanda cha kutengeneza magari ya betri nchini Rwanda

Kampuni ya China yaanzisha kiwanda cha kutengeneza magari ya betri nchini Rwanda

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1.jpg
2.jpg

Kampuni ya China ya Tailing Electric Vehicle imeanzisha kiwanda cha kutengeneza pikipiki na baiskeli za magurudumu matatu nchini Rwanda kwa nia ya kuchangia kupunguza hewa chafu duniani na kukuza uchumi wa kijani.

Kiwanda hiki kilichopo eneo la viwanda la Gahanga, wilayani Kicukiro kimeanza kuunganisha, kuuza na kuhudumia magari mapya yanayotumia nishati ya umeme. Bidhaa za kampuni hiyo ni pamoja na baiskeli za umeme, skuta za umeme, na baiskeli za magurudumu matatu ya umeme.

"Tofauti na magari yanayotumia mafuta, magari ya betri yanayozalishwa na kampuni yetu yanatumia asilimia 100 ya injini za betri ambazo zinahitaji usambazaji wa mara kwa mara wa nishati kutoka kwa betri," Tiger Hoo, mkurugenzi mkuu wa mtambo huo, alisema.

Alisema lengo ni kuwawezesha Wanyarwanda kuhamia mfumo endelevu, safi na bora wa usafiri ambao ni wa gharama nafuu. Anaona kuwa magari ya umeme yatasaidia serikali ya Rwanda kujenga mfumo wa uchukuzi wa kijani na kutotoa hewa chafu, katika sekta yake ya uchukuzi.

"Bidhaa zetu zitaboresha mahitaji ya usafiri kwa Wanyarwanda kwa sababu magari yanayotumia betri yameundwa kwa kuzingatia mazingira ya Rwanda," alisema Hoo.

Alisema tayari kampuni hiyo imefungua maeneo ya maonyesho na mitambo ya kuunganisha katika nchi za Afrika ambazo ni Afrika Kusini, Misri, Kenya, Tanzania na Rwanda. Mwaka jana, Rwanda ilizindua mradi wa majaribio wa pikipiki za umeme katika mji mkuu wa Kigali ili kusaidia nchi hiyo kuwa na uchumi usiotumia kaboni ifikapo mwaka wa 2050.

Ripoti ya mwaka wa 2018 ya Orodha ya Vyanzo vya Uchafuzi wa Hewa nchini Rwanda na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Rwanda ilionyesha kuwa moshi wa magari ndio chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa huko Kigali na maeneo mengine ya mijini katika nchi ya Afrika ya kati.

Tayari nchini Rwanda, siku ya kutotumia gari ilianza kama hafla ya kila mwezi mwaka wa 2016 kama mpango wa Jiji la Kigali, lakini mwaka mmoja baadaye ilifanywa kila baada ya wiki mbili, kwa pendekezo la Rais Paul Kagame.

Kwenye maadhimisho ya siku hii, watoto na watu wazima wa tabaka mbalimbali hujumuika katika kukimbia, kuendesha baiskeli, kutembea kwa miguu na kufanya mazoezi ya viungo vya mwili katika maeneo ya Kigali yaliyotengwa ili kuhamamsisha umma kukumbatia utunzaji wa mazingira kwa kutumia vifaa visivyotoa hewa ya kaboni. Hakuna injini zinazoruhusiwa kusonga kwa angalau masaa manne.

Ingawa haitoshi kutatua matatizo ya uchafuzi wa mazingira ya miji, wananchi wanaona mpango huu kama mwanzo mzuri na siku ya kufurahia. Ni mfumo ambao umeanza kufanyiwa majaribio na mataifa mengine ya Afrika kama vile Uganda, Zimbabwe na Ethiopia.
 
Bila shaka Hiki ni kiwanda kingine cha magari Rwanda. Congrats Kagame
 
Tusipokua makini na sheria zetu za biashara tutaendelea kua SOKO la watu hadi tukome; imagine idadi ya watu tuliopo bongo halafu mwekezaji anakwenda kuwekeza kwenye kinchi ambacho kina watu less than 12M na wala hakina resources nyingi za kiuchumi. Nampongeza sana Magufuli kwakua alianza kupunguza baadhi ya URASIMU wa baadhi ya sekta.
 
Wanaokasirika na wakasirike ila hongera sana majirani zetu mnaotumia vizuri fursa za uwekezaji na kupelekea vijana wengi kupata ajira ukweli usemwe tu, sisi ndio kwanza tunaelekeza nguvu kwa Mboe eti ndio tunashindana nae na upinzani wake, sisi wengine ni wakweli hatutaki unafik
 
Tanzania urasimu ni mkubwa sana, pamoja na hela yako mfukoni utazungushwa wee na rushwa za ajabu ajabu hadi ushangae...
 
Tusipokua makini na sheria zetu za biashara tutaendelea kua SOKO la watu hadi tukome; imagine idadi ya watu tuliopo bongo halafu mwekezaji anakwenda kuwekeza kwenye kinchi ambacho kina watu less than 12M na wala hakina resources nyingi za kiuchumi. Nampongeza sana Magufuli kwakua alianza kupunguza baadhi ya URASIMU wa baadhi ya sekta.
Ila pale wawekezaji wengi soko lao ni Congo mkuu
 
Wanaokasirika na wakasirike ila hongera sana majirani zetu mnaotumia vizuri fursa za uwekezaji na kupelekea vijana wengi kupata ajira ukweli usemwe tu, sisi ndio kwanza tunaelekeza nguvu kwa Mboe eti ndio tunashindana nae na upinzani wake, sisi wengine ni wakweli hatutaki unafik
Kagame unamjua wewe?? Hakuna mpinzani anayeishi mbele ya macho ya kagame. Watanzania na serikali yetu ni wapole sana mbowe bado yupo mahabusu anapumua, alafu umafananisha tz ya samia na Rwanda ya kagame
 
Ila pale wawekezaji wengi soko lao ni Congo mkuu
Unadhani itaishia Congo tu mkuu? Tenbelea Bukoba, Geita, Ngara, Biharamulo na baadhi ya maeneo ya Mwanza, kuna pilipili zinaitwa AKABANGA zinatengenezwa Rwanda, SOKO Bongo. Sisi acha tuendelee kuwekeza kwenye siasa, nadhani huko tunakumudu vizuri sana.
 
Tanzania tuna bandari, eneo kubwa la ardhi nk lakini wawekezaji wanatukimbia.

Nchi hii sera za uwekezaji ni mbovu sana na haziko stable, CCM ni Chanzo Cha Matatizo
 
Ipo siku tutanunua makapi (secondhand) toka kwao

Kwao ni kawaida wataendesha mapya ila yakichoka tutaanza kununua tu maana sisi tuko nyuma kwa kila kitu
Nchi kubwa hamna ubunifu kuna wazee wamo serikalini miaka hata kubuni kitu hawezi yupo yupo tu
 
Back
Top Bottom