Kampuni ya Madini ya Montero kuishitaki Serikali ya Tanzania ikidai fidia kwa mradi wa Wigu Hill



Mlisema tuna wachelewesha kwenye maendeleo?
 
Mkuu ,

Usiseme CCM ni ile ile, unapaswa kusema kwamba watanzania tunapaswa kubadilika kwani sio watendaji wote wa serikali ni wanachama wa CCM , serikali kuu umeundwa na wanachama wa vyama mbali Mbali.
Uko sahihi mkuu. Wakati naiunga mkono chadema (ile ya dr slaa) nilikuwemo serikalini, na hata sasa wakati siungi mkono chama chochote bado nimo serikalini; wamo pia wanachama na waungaji mkono wa chadema tunafanya nao kazi.
 
Should I sympathize with a government that disregards, not only international law, but even the laws that are promulgated by the very government, not to mention the Constitution of the country. THE ANSWER IS NO.
 
Tuwaache wakapambane na serikali huko mahakamani tu.

Lakini sio mahakama zetu hizi za Kitanzania.
Sawa Tumesikia Wasaliti wa nchi wakishirikiana na mabeberu kumuhujumu Watanzania.
Tundu Lissu tunayajua unayoyataka
 
Hii pesa hata isipoenda kwa wazungu, itaenda kuijrnga Chato, kwa maeneo mengine ya nchi, hawataona utofauti.

Kodi ya nchi nzima sasa, ya wamatumbi, wayao, wandengereko, wandali, n.k. inapelekwa kwenda kuinufaisha Chato pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haki ya nchi kufanya mabadiliko ya sheria inatambuliwa vipi?

Kwani Mining Act ilipofanyiwa amendment hapa Tanzania hakukuwa na freezing clauses? Mpaka hawa jamaa wanaenda mahakamani?
Kuna maamuzi ya mahakama yanayotambua haki ya nchi kufanya mabadiliko ya Sheria .

Mining act ilifanyiwa marekebisho kwenye maswala kadhaa ikiwemo aina za leseni.

Nilizungumzia freezing clauses nikihusianisha na Bilateral Agreement baina ya Canada na Tanzania.

Sijafanikiwa kuiona hiyo agreement so I can not comment.
 
Je, huu mkataba serikali na Montero kufanya utafiti hapa nchini ulifanyika kwa choice gani ya sheria na mamlaka za kimahakama?
 
Mjifunze kabla ya kufuta hizo sheria muwe mnatazama kwanza athari zitakazotokana na hayo maamuzi, sio mnakurupuka tu halafu mnalia lia mabeberu wameanza, ukweli nyie ndio mliowaanza wao wanamalizia.
He kwani tayari wameshashinda kesi?
 
KWA KWELI WATU WANAOTUINGIZA HUKU WANATAKIWA KUNYONGWA
 
Je, huu mkataba serikali na Montero kufanya utafiti hapa nchini ulifanyika kwa choice gani ya sheria na mamlaka za kimahakama?
Sidhani kama kulikuwa na mkataba baina ya serikali na Montero ila anacholalamika Montero ni kufutiwa leseni yake jambo analosema linakiuka makubaliano yaliyoingiwa baina ya serikali na Serikali ya Canada kuhusiana na maswala ya uwekezaji.

Mara nyingi kunapotokea disputes huwa dispute inaweza pelekwa mahakamani au kwa Arbitrator, ukiangalia hii taarifa utaona kwamba huu mgogoro unapelekwa kwa Arbitrator hivyo kuna uwezekano mkubwa Sana hiyo agreement ilitaka kunapotokea dispute matter ipelekwe kwa arbitrator.

Mara nyingi huwa disputes za aina hii zinakwenda The London Court of International Arbitration au Permanent Court of Arbitration , Vienna.
 
Kama kuna kipindi serikali iliingia mikataba ya hovyo,ni awamu iliyopita.
Na haitatuacha salama.
Hakuna mkataba mbovu ulioingiwa na awamu ya 4 au awamu zilizotangulia. Mkataba ni nipe nami nikupe baada ya makubaliano. Tafsiri ya mkataba mbovu ni hisia binafsi. Na ukihisi mkataba mbovu dawa ni kujitoa kwa mujibu wa matakwa ya mkataba husika na sheria za nchi au sheria za kimataifa.

Shida inatokea wakati mwendawazimu mmoja anayejifanya ana maono kuliko watangulizi wake anapovunja mikataba bila kufuata taratibu.
 
Tatizo lililopo ni kwamba serikali hii hutoa tu amri kwa kumuamuru mwanasheria mkuu wa serikali kupeleka muswada bungeni na yeye haruhusiwi kuhoji chochote na matokeo yake ndiyo haya.

Huo ulikuwa ni mkataba halali kabisa ulioingiwa kati ya mwekezaji na serikali lkn ilipokuja serikali hii ya sasa ndio ikabadilisha sheria za mchezo katikati ya mechi.

Na hapo lazima nchi italizwa tena, tutalazimika kulipa damages for the breach of contract and we shall be liable to pay all legal costs.
 
He kwani tayari wameshashinda kesi?
Lazima watashinda. Mabadiliko yale ya Kabudi yalikuwa ya hovyo kabisa japo wajinga wengi wanasifia bila ya kujua kilichomo ndani, faida na hasara yake.

Yeye mwenyewe Kabudi na Serikali kwa ujumla wanajua walivyoharibu, ndiyo maana kwenye makubaliano na Barrick, imebidi serikali iondoe mambo mengi ya hovyo ndani ya mkataba wa makubaliano ambayo sheria ya madini inayatambua. Sasa Barrick wana haki ya kuishtaki serikali mahakama za nje, wakati mabadiliko ya Kabudi yalikuwa yanazuia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada usiwe kama vijana wa Chadema ambao uwezo wao wa kujua mambo ni mdogo.

Hii ishi ni ndogo sana, hawa mabebeu hawawezi kutoboa maana ilikuwa ni voidable contract.
Njoo huku wewe pimbi uje useme hayo maneno tena. Kimeumana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…