Kampuni ya MI CASA yaamriwa kulipa Tzs milioni 20 kwa kuvunja faragha ya mtu

Kampuni ya MI CASA yaamriwa kulipa Tzs milioni 20 kwa kuvunja faragha ya mtu

Karangwa T

New Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
4
Reaction score
10
Katika hatua ya kusimamia Haki ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi za watu nchini, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imeiamuru Kampuni ya MI CASA kumlipa Wakili Abdul Naumanga Milioni 20 kama fidia kwa kutumia picha na ‘video’ zake katika akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa Instagram bila idhini yake.

Tukio hilo lilifanyika kati ya mwezi Februari mpaka Aprili 2023, na Maamuzi hayo yametolewa tarehe 10/07/ 2025 kutokana na Malalamiko Namba 8 ya 2024 yaliyofunguliwa na Mlalamikaji (Abdul Naumanga ambaye pia ni Wakili na mwanachama wa JamiiForums).

Mlalamikaji aliwasilisha maombi yake katika uongozi wa Kampuni ya MI CASA ili waweze kuondoa maudhui hayo lakini Walalamikiwa (MI CASA) hawakufanya hivyo, ndio akafikia hatua ya kufikisha malalamiko yake mbele ya Tume.

Japokuwa Mlalamikaji aliomba fidia ya Milioni 400, Tume imeamuru alipwe Milioni 20 pamoja na kuondolewa kwa maudhui hayo.

Vitendo vya kukiuka Faragha za Watu hasa kwenye baa, kumbi za starehe au kwenye sherehe mbalimbali vimekithiri nchini huku watu wengi wakilalamikia matumizi ya picha na video zao bila idhini kwa Watoa huduma kujinufaisha kibiashara bila kuzingatia kama zinavunja sheria.

Hatua iliyochukuliwa na Tume ni njia ya kuwakumbusha wanaokusanya na kuchakata taarifa binafsi za watu kusimamia Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kama inavyoelekezwa kwenye Katiba na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022

Kwa upande mwingine, Wananchi wanapaswa kuelewa Taarifa zao ni Utu wao na kuwa sasa Faragha na Taarifa zao Binafsi zinalindwa na ikitokea mtu amekiuka anaweza kuchukuliwa hatua mbalimbali zikiwemo zilizochukuliwa katika Shauri hili ili kuhakikisha haki zao hazivunjwi kiholela.
 

Attachments

Abduli yupo micasa kwenye hot chair....waliua vibe
 
Back
Top Bottom