Kampuni ya mtandao wa YAS imeajiri matapeli!?

Kampuni ya mtandao wa YAS imeajiri matapeli!?

Juzi nilikuwa nabishana na Mbaga Jr, kuhusu hili. Dah! Hawa watu wasio waadilifu kwenye haya makampuni watatumaliza.
Nimeliishi hili kwa zaidi ya miezi 6,tena nikienda sehem nikamkuta wakala mgeni ndio huwa kazi nyepesi au mtoto. Nilikuja kujichanganya kuna sehemu nilishapigaga nikarudia kwenda tena baada ya miezi kadhaa,jamaa akanikumbuka😄
 
Kifupi nilikuwa na combination na IT wa mtandao fulani hapa bongo,kwahiyo kazi yangu ilikuwa ni kwenda kwa wakala na kumwambia nataka kutoa hela kwenye mtandao husika(ambao IT wangu anafanyia kazi) akisema toa,nachukua namba ya wakala naituma kwa IT,baada ya dakika 1 wakala atapokea meseji kuwa fulani ametoa milion moja au hata laki 5, basi wakala bila waswas atanipa pesa,nao doka ila akiangalia salio ndio atagundua kapigwa,maana hizi meseji za mchongo ukaa kwa dk 5 au 10 alafu zinafutika.
Kwahiyo nipo sahihi nikisema makampuni ya simu yanaajiri matapeli!?
 
Mnaweza kuhisi hivyo ila hawa matapeli wala hawajuani na waajiliwa wa mitandao ya simu bali wanabahatisha tu
Kuna comment hapo jamaa amesema alikuwa anashirikiana na IT anayefanya kazi katika kampuni ya mtandao wa simu kufanya utapeli.
Sasa sijui unalizungumziaje hilo!?
 
Kuna comment hapo jamaa amesema alikuwa anashirikiana na IT anayefanya kazi katika kampuni ya mtandao wa simu kufanya utapeli.
Sasa sijui unalizungumziaje hilo!?
Hili la kushirikiana nahisi ni kweli kwasababu kuna wakala moja aliibiwa pesa : tapeli alitafuta simu inayofanana na ya wakala akaenda kwa wakala kutuma pesa, wakala akajisahau akampa simu ili aweke namba huyo jama akabadilisha simu, ndani ya dak 5 alivotoka hapo kwa wakala pesa ilikua imeshahamishwa, hapo unajiuliza alijua je namba ya siri ya simu ya wakala bila kua na koneksheni na watu wa mtandao?
 
Nilichojiuliza, inawezekanaje huyu tapeli kujua kiasi cha fedha kilichopo kwenye simu yangu bila kumtajia!?
Benki wanajua salio na nywila yako wanaijua vyema tu. Huyo tapeli kapewa information yako na mtu wa ndani wa YAS.

Viongozi wa Serikali wapo kwa kufanya kazi kwa ajili ya wananchi ila wizi hatari. Kila anae fanya kazi si mfanyakazi wengine ni wizi/majambazi ila anaingia kwa mgongo wa ajira.
 
Huyo jamaa alikufanyeje? Ulitoka salama?
Nilikuwa baa najipongeza baada ya kazi ya siku nzima...
Mpe yule yule muluke,kibubu kikakata ikabidi niende kwa wakala kufanya jambo tena,sasa coz ya pombe nikasahau kuwa pale nishapigaga,nikauliza namba ya wakala akataja ili nimtumie jamaa yangu.. nikatoa wakati anahesabu hela akajifanya anajizungusha zungusha kumbe kamtumia text boss wak,yuko njiani anakuja,alooh nilichezea kichapo,nikaja kuokolewa na majamaa ambao nawapaga ofa mara kwa mara,nikapelekwa kituoni. Yani waliniitia mwizi.
 
Experience yangu inasema Hawa wanaosajili line mtaani wengine ni wezi .

Pale anapokusajilia anakuwa access za information zako , Mimi Kuna siku wale wasajili line walikuja kunipandishia line yangu kuwa 4g nikawatajia Nida na taarifa nyingine .

Mimi mwenyewe mtoto wa town walivyoondoka nikaingia Tigo pesa yangu app kwenye device connected nikaona Kuna simu ipo siitambui , nikamLog out kumbe jamaa alikuwa na access ya kuona miamala yangu kupitia app ya Tigo pesa yake alivyokuwa nayo baada ya Mimi kumtajia taarifa zangu aliLogin bila kujua
Huwa wanafanya hivyo Hasa akiwa Na Nida yako...
 
Nilikuwa baa najipongeza baada ya kazi ya siku nzima...
Mpe yule yule muluke,kibubu kikakata ikabidi niende kwa wakala kufanya jambo tena,sasa coz ya pombe nikasahau kuwa pale nishapigaga,nikauliza namba ya wakala akataja ili nimtumie jamaa yangu.. nikatoa wakati anahesabu hela akajifanya anajizungusha zungusha kumbe kamtumia text boss wak,yuko njiani anakuja,alooh nilichezea kichapo,nikaja kuokolewa na majamaa ambao nawapaga ofa mara kwa mara,nikapelekwa kituoni. Yani waliniitia mwizi.
We unajua umeshindikana🙆🏽‍♀️
 
We unajua umeshindikana🙆🏽‍♀️
Ni mapitio ya maisha ndugu yangu,na wakati nayafanya hayo yote nilikuwa chuo mwaka wa pili utumishi Mtwara,..
Maisha ya chuo starehe,zikanifanya niingie kwenye huo utapeli ili nitambe vizuri.
Hata wazazi wanapigiwa simu niko polisi walishangaa,maana wanajua niko chuo nasoma na huwa sina mambo mengi.
 
Back
Top Bottom