Kampuni ya mtandao wa YAS imeajiri matapeli!?

Kampuni ya mtandao wa YAS imeajiri matapeli!?

Ni mapitio ya maisha ndugu yangu,na wakati nayafanya hayo yote nilikuwa chuo mwaka wa pili utumishi Mtwara,..
Maisha ya chuo starehe,zikanifanya niingie kwenye huo utapeli ili nitambe vizuri.
Hata wazazi wanapigiwa simu niko polisi walishangaa,maana wanajua niko chuo nasoma na huwa sina mambo mengi.
Duhh aisee pole! Kwahiyo tangu hapo haujawahi kutamani kurudia tena? Duh maisha yanatufunza vingi..
 
Leo nimepigiwa simu na tapeli aliyejitambulisha kuwa anapiga simu kutoka makao makuu ya kampuni ya mtandao wa YAS, baada ya salamu tapeli huyo ananitishia kuwa laini yangu ya simu itafungwa baada ya muda mfupi.
Nikamjibu fungeni tu wala hamna tatizo, nitasajili laini nyingine.

Alichonijibu tapeli sasa, nilishangaa sana. Tapeli akanijibu kuwa wanatoa na pesa zangu zote, tena akanitajia na salio langu lote kama lilivyo kwenye laini ya simu. Kabla sijamuuliza chochote akakata simu.

Nilichojiuliza, inawezekanaje huyu tapeli kujua kiasi cha fedha kilichopo kwenye simu yangu bila kumtajia!?

Ina maana taarifa zetu hazipo salama, wafanya kazi waliopo kwenye makampuni ya mitandao ya simu wanauza taarifa zetu kwa matapeli!?
MTU anaweza jua taarifa za salio laki ikiwa umeeka application za backup usizozijua ama kuziamini ama akiwa na access na email yako etc. Kila ukitoa hela msg ya salio lililobaki inakuja, hivyo sio lazima awe ni mfanyakazi tigo kujua.
 
Ina maana taarifa zetu hazipo salama, wafanya kazi waliopo kwenye makampuni ya mitandao ya simu wanauza taarifa zetu kwa matapeli!?
Nakuhakikishia hazipo salama, ushahidi ni kuwa;
  1. Kuna waganga wa kienyeji wanatuma meseji kila siku kutangaza kazi zao
  2. Kuna makampuni ya mikopo yanatuma meseji kila siku kututaka tukakope
  3. Kuna makampuni ya biashara yanashawishi tukanunue bidhaa kwao kila muamala ukiingia
Swali:
Namba zetu wanazipata wapi
Nani huwaambia kuna muamala umeingia kwenye line fulani?
 
Kwahiyo Kuna matapeli wanaobahatisha na matapeli wansoshirikiana na customer service ya yas
 
Experience yangu inasema Hawa wanaosajili line mtaani wengine ni wezi .

Pale anapokusajilia anakuwa access za information zako , Mimi Kuna siku wale wasajili line walikuja kunipandishia line yangu kuwa 4g nikawatajia Nida na taarifa nyingine .

Mimi mwenyewe mtoto wa town walivyoondoka nikaingia Tigo pesa yangu app kwenye device connected nikaona Kuna simu ipo siitambui , nikamLog out kumbe jamaa alikuwa na access ya kuona miamala yangu kupitia app ya Tigo pesa yake alivyokuwa nayo baada ya Mimi kumtajia taarifa zangu aliLogin bila kujua
Wa mitaani nakataa kwa herufi kubwa kwasababu hio kazi ni ngumu kujua salio lako labda waliokwenye mfumo hao ndo uhakika
 
Nilikuwa baa najipongeza baada ya kazi ya siku nzima...
Mpe yule yule muluke,kibubu kikakata ikabidi niende kwa wakala kufanya jambo tena,sasa coz ya pombe nikasahau kuwa pale nishapigaga,nikauliza namba ya wakala akataja ili nimtumie jamaa yangu.. nikatoa wakati anahesabu hela akajifanya anajizungusha zungusha kumbe kamtumia text boss wak,yuko njiani anakuja,alooh nilichezea kichapo,nikaja kuokolewa na majamaa ambao nawapaga ofa mara kwa mara,nikapelekwa kituoni. Yani waliniitia mwizi.
Dah! Pole aisee!
 
Mnaweza kuhisi hivyo ila hawa matapeli wala hawajuani na waajiliwa wa mitandao ya simu bali wanabahatisha tu. Ila huyu anayesema wametaja salio kwa usahihi, inawezekana yeye mwenyewe kuna mahali alijiingiza kingi kwasababu kwa maelezo yake inaonekana kuna namna anaamini kuwa wanaompigia ni waajiliwa wa YAS.
Matapeli wengi sana huwa wanapatikana Katindiuka, Ifakara. Ukienda hiyo eneo wapo bize vibaya mno na kupiga piga simu lakini sijui kwanini hawachukuliwi hatua.

Lingine kwa wanaotumia hizi apps za miamala, muwe makini na kutotoa msimbo wauda (OTP)usimpe mtu hata kama akikwambia anatokea ofisi ya hii mitandao ya simu.
Ifakara kule relini duuh🤣🤣🤣 wanakula na police
 
Back
Top Bottom