Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,238
Ni hivi majuzi tu nilileta hapa jamvini mada ya kujadili kuhusu uhalali na busara ya serikali yetu tukufu kuipatia mabilioni ya bail-out kampuni ya usafiri wa anga ya Precision Air.
Hatimaye Precision Air imetangazia wanahisa na wadau wake kwa ujumla, kuwa kampuni hiyo imepata hasara ya shilingi za kitanzania Bilioni 30.4 kwa mwaka wa fedha ulioishia Machi 2013. Hasara hiyo ni wastani wa hasara ya TZS 189 kwa kila hisa moja.
Hasara hii inamaanisha kuwa mwekezaji aliyenunua hisa za kampuni mwaka huu kwa bei ya TZS 450 kwa hisa moja, atakuwa amepata hasara ya shilingi 164 ikiwa angeamua kuuza hisa zake leo tarehe 6 September 2013 (Bei ya soko ikiwa ni TZS 475 kwa kila hisa). Hii ni sawa na hasara ya asilimia 36.4 kwenye kiasi alichowekeza. Kwa uwiano huo huo, inamaanisha kuwa mwekezaji aliyekuwa amewekeza shilingi milioni 10 atakuwa amepata hasara ya shilingi milioni tatu na laki sita (TZS 3,640,000).
Ufuatao ni mtiririko wa faida na hasara za kampuni ya Precision Air kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
[TABLE="width: 800"]
[TR]
[TD]Mwaka
[/TD]
[TD]2009
[/TD]
[TD]2010
[/TD]
[TD]2011
[/TD]
[TD]2012
[/TD]
[TD]2013
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Faida/(Hasara) kabla ya kodi (TZS bilioni)
[/TD]
[TD] 2.82
[/TD]
[TD] 1.92
[/TD]
[TD] 2.16
[/TD]
[TD] 2.23
[/TD]
[TD]
(30.40)
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo bwana Michael Shirima, Hasara iliyopatikana mwaka wa fedha wa 2013 imetokana na sababu nyingi ikiwemo ongezeko la gharama za ukodishaji ndege, kushuka kwa thamani ya shilingi kulikosababisha fedha za kitanzania zilizolipwa kama mikopo ya ndege tajwa kuongezeka, ongezeko la mishahara ya wafanyakazi na kupanda kwa gharama ya matura ya ndege.