Kampuni ya ndege ya Precision Air yapata hasara maradufu..

Kampuni ya ndege ya Precision Air yapata hasara maradufu..

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
1,948
Reaction score
1,238
air.jpg

Ni hivi majuzi tu nilileta hapa jamvini mada ya kujadili kuhusu uhalali na busara ya serikali yetu tukufu kuipatia mabilioni ya bail-out kampuni ya usafiri wa anga ya Precision Air.
Hatimaye Precision Air imetangazia wanahisa na wadau wake kwa ujumla, kuwa kampuni hiyo imepata hasara ya shilingi za kitanzania Bilioni 30.4 kwa mwaka wa fedha ulioishia Machi 2013. Hasara hiyo ni wastani wa hasara ya TZS 189 kwa kila hisa moja.

Hasara hii inamaanisha kuwa mwekezaji aliyenunua hisa za kampuni mwaka huu kwa bei ya TZS 450 kwa hisa moja, atakuwa amepata hasara ya shilingi 164 ikiwa angeamua kuuza hisa zake leo tarehe 6 September 2013 (Bei ya soko ikiwa ni TZS 475 kwa kila hisa). Hii ni sawa na hasara ya asilimia 36.4 kwenye kiasi alichowekeza. Kwa uwiano huo huo, inamaanisha kuwa mwekezaji aliyekuwa amewekeza shilingi milioni 10 atakuwa amepata hasara ya shilingi milioni tatu na laki sita (TZS 3,640,000).
Ufuatao ni mtiririko wa faida na hasara za kampuni ya Precision Air kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
[TABLE="width: 800"]
[TR]
[TD]Mwaka
[/TD]
[TD]2009
[/TD]
[TD]2010
[/TD]
[TD]2011
[/TD]
[TD]2012
[/TD]
[TD]2013
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Faida/(Hasara) kabla ya kodi (TZS bilioni)
[/TD]
[TD] 2.82
[/TD]
[TD] 1.92
[/TD]
[TD] 2.16
[/TD]
[TD] 2.23
[/TD]
[TD]
(30.40)
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo bwana Michael Shirima, Hasara iliyopatikana mwaka wa fedha wa 2013 imetokana na sababu nyingi ikiwemo ongezeko la gharama za ukodishaji ndege, kushuka kwa thamani ya shilingi kulikosababisha fedha za kitanzania zilizolipwa kama mikopo ya ndege tajwa kuongezeka, ongezeko la mishahara ya wafanyakazi na kupanda kwa gharama ya matura ya ndege.
 
MIKOPO YA MA BENKI ni sumu,nawashauri wana jf wenzangu kama una biashara yako unapata faida sh 10000 kwa siku jitahidi hivyo hivyo ukuze mtaji wako,ukidanganyika ukakope bank eti upate faida 50000 IMEKULA KWAKO,BANK WATACHUKUA HATA ULE MTAJI WAKO WA AWALI
 
Mkuu Prisoner nlifuatilia ile taarifa uliyoweka ya awali, thenx for this developing story. Heshima mbele kwako mkuu.

Mimi najiuliza, kwani mwanzoni Shirima yeye binafsi sia alikuwa na ndege zake nne? Kwa sababu nasikia aliingia ubia na wakenya, wakamshauri aongeze route eg south africa ambayo ilikuwa inaoperate kwa hasara kubwa.

Pia wakamshauri aongeze boeing kwa mkopo. So ndege alizoongeza zote ni mkopo. Mimi ninavyooelewa shirima anachoweza kufanya ni kukubali ameshindwa kurudisha mkopo kw nini asiache hizo ndege alizokopa zitaifishwe na benk abakie na zile ndege nne za awali, aende na ile biashara yake ya awali.

Pia alikokosea alikataa kuingia ubia na serikali akawaona wakenya ni muhimu, ila nnachoelewa wakenya pale Precision wanalipwa international rate, kias administration ni ghali why asiwapige chini? Mkuu kama unaweza nitoa tongotongo. Kwa mara nyingine. Heshima mbele. Mia
 
Wewe sio BONGOLALA ila ni BONGOAMKA ulichoeleza nisawa mabenk yanafilisi mpk mtaji nahile ni RIBA kam ilivokatazw ktk uislam huwez kwenda mbele,Shirima labda hakua na taarifa kam kenya airways inaendeshw kw hasara,Shirima kidog chako nibora kuliko kikubwa cha shirika
 
Hivi Presicion Air hawana Kitengo cha Mawasiliano (Publicity/Public Relations or whatever it is called) ili waje kutoa maelezo ya "upande wa pili wa shilingi) na kuutaarifu Umma nini kinafuata?
Siku zote binafsi huwa ninaihusisha Precision na kifo cha Kampuni yetu pendwa ya ATC(L) (ni hisia tu), lakini sifurahii vilevile Kampuni na Biashara za Wazawa zinapopiga mbizi kama hali inavyoelekea kwa Precision!
 
Faida ilikuwa stead kwa kipindi chote, ghafla an ABNORMAL BIG LOSS. Kupata hasara kwa Public Listed Company na kugawana au kuathiri Price Per Share si ajabu kwa kuwa Shareholders wanashirikishwa katika maamuzi makubwa yanaweza kuleta matokeo yenye faida au hasara kwa kampuni. Taarifa fupi ya Prisoner 46664 ingekamilika kama angeleta major investment decisions kwa miaka mitatu ya nyuma na jinsi ilivyo perform. A complete set of 3 years Financial Statement could tell the reason the reason as to why this BIG and HUG loss.
 
Hii habari sio nzuri kwa kila upande investors(wenye hisa) na suppliers.nina uhakika precision itakuwa na madeni makubwa ya makampuni ya mafuta.kama govenment itashindwa kubail out maanake next step itatangazwa mufilisi na itakuwa kilio kikubwa sana kwa Watanzania.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bye bye kamtaji kangu nilikowekeza huko.
Mungu akipenda tutaonana. Naandika kwa uchungu sn.
 
Mkuu Prisoner nlifuatilia ile taarifa uliyoweka ya awali, thenx for this developing story. Heshima mbele kwako mkuu.

Mimi najiuliza, kwani mwanzoni Shirima yeye binafsi sia alikuwa na ndege zake nne? Kwa sababu nasikia aliingia ubia na wakenya, wakamshauri aongeze route eg south africa ambayo ilikuwa inaoperate kwa hasara kubwa.

Pia wakamshauri aongeze boeing kwa mkopo. So ndege alizoongeza zote ni mkopo. Mimi ninavyooelewa shirima anachoweza kufanya ni kukubali ameshindwa kurudisha mkopo kw nini asiache hizo ndege alizokopa zitaifishwe na benk abakie na zile ndege nne za awali, aende na ile biashara yake ya awali.

Pia alikokosea alikataa kuingia ubia na serikali akawaona wakenya ni muhimu, ila nnachoelewa wakenya pale Precision wanalipwa international rate, kias administration ni ghali why asiwapige chini? Mkuu kama unaweza nitoa tongotongo. Kwa mara nyingine. Heshima mbele. Mia

Ni kweli kabisa mkuu. sixgates,..Precision kama ni kupona hili tetemeko basi inahitaji kupata mkakati mpya kabisa wa kibiashara..mkakati ambao ni lazima uhusishe ku'downsize' kwa kupunguza idadi ya ndege walizo-lease, idadi ya wafanyakazi na matumizi mengineyo...sasa hatari kubwa kuliko zote itakuwa kama huyu Mkenya aliwaongoza kusaini mikataba isiyovunjika kirahisi ('non-cancellable lease agreements'). Ikiwa ni hivyo, inaweza kuwa ni gharama kubwa zaidi kwa wao kuvunja hiyo mikataba kuliko kuendelea nayo, hivyo watalazimika kubakia na hizo ndege kubwa walizozipata sasa hivi na kujaribu kurudi kwenye ushindani kwenye soko la nyumbani na la nje kwa wakati mmoja...a lose-lose situation to me.. Kinacholeta utata zaidi kwenye hili suala la bail-out ni ukweli kuwa huu mkakati wa kuitoa PW hapa ilipo bado haujawekwa wazi...lakini bado hela ya serikali inatakiwa...sad but true.
 
Last edited by a moderator:
Bye bye kamtaji kangu nilikowekeza huko.
Mungu akipenda tutaonana. Naandika kwa uchungu sn.
ha ha...pole sana mkuu...unajua kuna sehemu nimekuona ukimwaga elimu ya "PHD" kuhusu anga na ndege leo, ni vipi hamkuwahi kuuza share zenu mara tu fast-jet ilipotangaza strategy ya bei rahisi?..Nilishangaa sana kuona share za precision hazikushuka bei wakati ule...too bad, sasa hivi kuna hisa nyingi sokoni kila mtu anataka kuuza na mnunuzi hakuna...
 
hivi ni kazi sana mtu kuanzisha kampuni ya ndege iwapo ukitafuta wafadhili nchi za nje??
Nitajitoa mhanga mimi kwa kujairibu
hebu mwenye idea yeyote tulizungumze hili
wataalamu ninawasubiri
 
Hii habari sio nzuri kwa kila upande investors(wenye hisa) na suppliers.nina uhakika precision itakuwa na madeni makubwa ya makampuni ya mafuta.kama govenment itashindwa kubail out maanake next step itatangazwa mufilisi na itakuwa kilio kikubwa sana kwa Watanzania.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Imapro,...tunarudi pale pale tulipokuwa mara ya mwisho...serikali inunue asilimia 51 ya hisa za PAL kwa kutumia hiyo 51 billion wanayotaka na tuachane na mpango wa kupeana hela za bure za mikopo ambayo haitakaa ilipike..hao waTanzania unaowasema watakuwa wamesaidika hapo kwa njia ambayo haitaumiza sana hawa waTanzania wengine waliobaki....
 
Last edited by a moderator:
Bongo sasa ni sanaa tupu nico nao walikuja na mbwe mbwe za kuuza hisa kama ivo na mwisho wake ukawa kama precition wanaoufanya na wakiondoka sokon itakuwa neema kwa fast jet ambayo bila kukosea ni kampun ya nje
 
fastjet na bei zao chee nayo ilichangia precision kupata hasara...mwaka jana kulikua na inflation kubwa plus kushuka kwa mapato daah ndo ivo tena....msiwalaum kwa kuingia ubia na kenya airways coz at that time business was booming for kenya airways na walikua vzur
 
Faida ilikuwa stead kwa kipindi chote, ghafla an ABNORMAL BIG LOSS. Kupata hasara kwa Public Listed Company na kugawana au kuathiri Price Per Share si ajabu kwa kuwa Shareholders wanashirikishwa katika maamuzi makubwa yanaweza kuleta matokeo yenye faida au hasara kwa kampuni. Taarifa fupi ya Prisoner 46664 ingekamilika kama angeleta major investment decisions kwa miaka mitatu ya nyuma na jinsi ilivyo perform. A complete set of 3 years Financial Statement could tell the reason the reason as to why this BIG and HUG loss.
Mkuu kaburu..walichofanya precision air kwa mwaka juzi ni naive investing..kama mimi kipindi kile naanza kufanya biashara ambapo nlikuwa napiga mahesabu na kuweza kumshawishi mtu kabisa kuwa naweza kugeuza milioni moja kuwa 5 ndani ya mwezi mmoja...kumbe kuna so many other factors yet to be considered... Ukiwauliza precision wanaweza wasijue ni kwanini walikuwa chaguo la watu wakati wa nyuma..watashindwa kujua kuwa sababu kuu ni kuwa walikuwa hawana mshindani, kwa hivyo wasafiri walikuwa hawana choice..ilikuwa ni kawaida sana kwa watu kulalamika kila siku kuwa ndege zinachelewa mara nyingi lakini hakuna kilichokuwa kinafanyika..kwa style hii, kuna uwezekano kuwa fast jet wangeweza kuja na strategy tofauti kabisa na hii ya bei..wakahakikisha tu within 6 months ya kuanza kwao kuna excellent customer care na hakutakuwa na flight - delays hata siku moja..I assure you, precision would have gone to its knees still...
 
Hivi sie wazawa hatuwezi kuanzisha makampuni yetu ya ndege na yakawa yako strong??
Tatizo nini? Au ufadhili kutoka makampuni ya nje??

Mie nitajitoa mhanga aisee kwa kutafuta makampuni ya nje
wataalamu nipeni consultation kwa hili
 
hivi ni kazi sana mtu kuanzisha kampuni ya ndege iwapo ukitafuta wafadhili nchi za nje??
Nitajitoa mhanga mimi kwa kujairibu
hebu mwenye idea yeyote tulizungumze hili
wataalamu ninawasubiri
Sio kazi boss,...tafuta hela ya kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa miaka mitatu..,halafu uwe tayari kupata hasara ya miaka miwili...na uwe na market penetration strategy..na bei yako iwe chini ya fast jet..ndege watakukodisha tu hakuna shida...hapo kwenye pricing, na mbinu ya kuingilia sokoni ndiko kunakozuia kila mtu asifanye biashara, sio tu ya ndege, bali nyingine nyingi...
 
Mkuu kaburu..walichofanya precision air kwa mwaka juzi ni naive investing..kama mimi kipindi kile naanza kufanya biashara ambapo nlikuwa napiga mahesabu na kuweza kumshawishi mtu kabisa kuwa naweza kugeuza milioni moja kuwa 5 ndani ya mwezi mmoja...kumbe kuna so many other factors yet to be considered... Ukiwauliza precision wanaweza wasijue ni kwanini walikuwa chaguo la watu wakati wa nyuma..watashindwa kujua kuwa sababu kuu ni kuwa walikuwa hawana mshindani, kwa hivyo wasafiri walikuwa hawana choice..ilikuwa ni kawaida sana kwa watu kulalamika kila siku kuwa ndege zinachelewa mara nyingi lakini hakuna kilichokuwa kinafanyika..kwa style hii, kuna uwezekano kuwa fast jet wangeweza kuja na strategy tofauti kabisa na hii ya bei..wakahakikisha tu within 6 months ya kuanza kwao kuna excellent customer care na hakutakuwa na flight - delays hata siku moja..I assure you, precision would have gone to its knees still...

Thank you for your input, from the little I know, I think loss of customers will only erode sales (revenue), for airline industry will be hit by capacity charges just like their fellows in energy industry, since they will be having little to do with fixed costs. For this I don't think that will bring that huge loss, as far as their variable cost are still within their manageable capability. I do believe there are other decision they made
 
Back
Top Bottom