Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) yavikana vichwa vya Treni, yataka virudishwe vilipotoka

ni vya kwangu..
nataka nivitumie kwa trip za dar kibiti..
serikali ya ccm punguzeni uzushi...
mnakana vinyesi vyenu ili tuwaone wasafi ?
binafsi 2020 kura yangu hamuwezi kuipata..
labda muendelee na bao la mkono.
Kula yako mpee mange huko insta , ccm hawaitaki
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!
Ni kwamba wewe tayari ulishajiwekea jibu unalolitaka. Licha ya juzi kusikia hilo, akili yako ilishasema unataka jibu lako, sasa ulikuwa unasubiri yeyote aongee utakavyo ufurahi, sasa umefurahi! Haya kanywe maji ya dasani!
 
Hivi vichekesho balaa...Nahisi kuna watu wanakimbia majukumu yao kwa maana haileti maana eti vichwa vinaletwa halafu mmiliki au aliyeviagiza hayupo
 
Tatizo la shamba la bibi kila mtu ana mamlaka ya kupanda na kuvuna apendacho hata kama hali ya hewa na udongo haviruhusu. Ili mradi uonekane umelima.
 
Vichwa vinavyoonyeshwa hapa vililetwa mitatu iliyopita na vinafanya kazi,
Kama huna picha basi wote tumesikia sio lazima tuone ili tuamini
Ninyi si ndio mnaodai ni timu weka picha?
Pia tumia ufahamu wako kidogo kung'amua. Hiyo taarifa nimeipresent vipi?
 
hiyo inaitwa ngedere kamkataa mwane..
mpaka hatua hiyo uje polini hakukalikai tena....
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Engineer Deusdedit Kakoko amesema vichwa vya treni vinavyodaiwa kutelekezwa bandarini ni mali ya shirika la Reli nchini TRL na kwamba vina nembo ya TRL (Tanzania Railway Limited). Kakoko amesema TRL walinunua vichwa hivyo bila kufuata utaratibu kutoka kampuni ya EMD ya nchini Marekani, lakini vimetengenezwa na kampuni ya DCD ya nchini Afrika Kusini.

Maelezo ya Kakoko yanahitimisha taarifa "zilizovumishwa" hivi karibuni kuwa vichwa hivyo havina mwenyewe. Kwa lugha rahisi ni kwamba Engineer Kakoko amesema SI KWELI kwamba vichwa hivyo havina mwenyewe. Kakoko anasema ni vya TRL na vina nembo ya TRL.

MyTake:
Nimetafakari sana maelezo ya Kakoko nikakumbuka zile tambo za juzi kwamba tumekamata vichwa vya treni ambavyo havina mwenyewe. Nikajiuliza lengo la tambo zile lilikua nini? Kama Kakoko alijua vichwa ni vya TRL ilikuaje "mwenye nyumba" akasema havina mwenyewe? Hakumuuliza Kakoko? Alidanganywa? Alijua ukweli lakini akatupotosha? Ili iweje? Kwa faida ya nani?

Kwani angesema ni vya TRL lakini vilinunuliwa bila kufuata utaratibu kungekua na tatizo gani? Kwanini aseme uongo kuwa havina mwenyewe wakati vina nembo ya TRL? Ina maana hakuona hata nembo? Au hiyo nembo iliwekwa baada ya "mwenye nyumba" kuondoka? Anyway tuendelee kumuombea.!!

washauri nao wawe makini kwenye kumpelekea ubuyu mkuu..
vinginevyo ni kuwachonganisha mkuu na wasaidizi wake...
 
hii picha ni rahisi sana kumjua mwenye vichwa,ila issue apa ni maigizo ndo kinatusumbua watanzania kwasababu una aanza na mesina nani aliwalipa freght mpaka apa? pia manfest inasema jina gani tra na linaendana na la kwenye b/l iliyotoka mesina mbona kazi ambayo ata masaa 2 utumii kupata jibu
 
[emoji2][emoji3] *Nchi ya neema ni ya neema tu Tuna Madini..Bahari ...maziwa...Milima mikubwa..nasasa Mungu katushushia vichwa vya tren ghafla tu vimeingia bandarini na kwa mshangao kila mtu anajiuliza vya nani kwani baada ya kukosekana muagizaji.. huyo niroho mtakatifu jamani ametenda miujuza*
 
Bilioni sabini na ushee wamelipa leo wanasema hawawezi kukiuka sheria ya manunuzi sasa hela ilitokaje?

Nani aliidhinisha zikatoka huyo ndiye anapaswa ajibu khoja
 
Messina shipping line si wapo? waweke copy ya bill of lading hapa tuione
 
ni vya kwangu..
nataka nivitumie kwa trip za dar kibiti..
serikali ya ccm punguzeni uzushi...
mnakana vinyesi vyenu ili tuwaone wasafi ?
binafsi 2020 kura yangu hamuwezi kuipata..
labda muendelee na bao la mkono.
Sharif kwani kura yako ni turufu??
 
[emoji2][emoji3] *Nchi ya neema ni ya neema tu Tuna Madini..Bahari ...maziwa...Milima mikubwa..nasasa Mungu katushushia vichwa vya tren ghafla tu vimeingia bandarini na kwa mshangao kila mtu anajiuliza vya nani kwani baada ya kukosekana muagizaji.. huyo niroho mtakatifu jamani ametenda miujuza*
duh! Safi sana
 
Ila hii nchi inayoitwa Tanzania ni kiboko! Ina maana kuna mtu aliagiza/alinunua hivyo vichwa vya train bila serikali kujua, na akala 10% yake vilevile! Only in Tanzania![emoji3]
 
Hizo ni mbinu za siasa

Mwisho wa picha hilo ni magu kuyataifisha hayo mavichwa na kutumika na serekari

Alafu tutaandaa maandamano ya kumpongeza.

Yaana director wa hizi movies ameshaanza kuchuja maana movies zake zinakuwa kama bongo movies, yaani picha likianza ushajua mwisho wake itaishaje
 
Back
Top Bottom