Kampuni ya Samsung yaacha kuuza vifaa vyake vyote vya kielektroniki vya nyumbani nchini China

Kampuni ya Samsung yaacha kuuza vifaa vyake vyote vya kielektroniki vya nyumbani nchini China

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
Kampuni ya Samsung hivi karibuni ilitangaza kuwa itaacha kuuza vifaa vyake vyote vinavyotumika nyumbani nchini China. Chapa ya Samsung ilikuwa alama ya vifaa vya kielektroniki vya nyumbani vya hali ya juu na vyenye ubora wa juu zaidi, lakini sasa imeshindwa kabisa na kampuni za ndani za China.

Ukiritimba wa awali wa kampuni ya Samsung kwenye soko la China ulitokana na teknolojia zake zilizojumuishwa. Kwa mfano televisheni, Samsung ilitengeneza skrini na chip yenyewe. Ingawa bei ya televisheni zake ilikuwa ghali, lakini zilikuwa zinakaribishwa sana na wateja wa China. Hata hivyo, katika muongo mmoja uliopita, sekta ya utengenezaji ya China imepiga hatua kubwa. Kampuni za skrini za China, zinazowakilishwa na BOE na CSOT, si kama tu zimevunja ukiritimba wa Korea Kusini, bali pia zimepata udhibiti wa teknolojia za kizazi kijacho. Katika tasnia ya chip, haswa katika chip za vifaa vya nyumbani, kasi ya uvumbuzi ya China iko mbele sana duniani.

Vifaa vya kielektroniki vya nyumbani ni mfano mmoja tu, bidhaa mbalimbali za “Made In China” tayari zimeshika nafasi kubwa katika soko la kimataifa. Kama jarida la Marekani Eurasia Review lilivyosema hivi karibuni, tunashuhudia “China Products 2.0”, lakini mara hii, vilivyojaa duniani si vifaa vya kuchezea vya plastiki vya bei rahisi tena, bali ni vifaa vya nyumbani vyenye ubora wa juu, magari ya umeme, na masuluhisho ya kijani yenye utaratibu.

Katika Siku ya Chapa za China ya mwaka 2026 iliyofanyika hivi karibuni, mwelekeo muhimu umefuatiliwa: chapa za China zimeingia katika “wakati wa DeepSeek”, zikibadilika kutoka bidhaa za bei nafuu hadi chapa za hali ya juu za kimataifa. Kwa mfano magari ya umeme, katika robo ya kwanza ya mwaka 2026 mauzo ya nje ya magari hayo ya China yaliongezeka kwa asilimia 77.5, na kuwa bidhaa muhimu sana katika masoko kama vile Brazil na Mexico. Huu si ushindani wa kibiashara tu, bali pia ni nguvu kubwa katika kutimiza malengo ya kimataifa ya kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa .

Kuondoka kwa Samsung ni matokeo yasiyoepukika kutokana na maendeleo ya kiviwanda ya China katika miaka arobaini iliyopita. Ikiwa muongo uliopita ulikuwa muongo ambao Samsung na Apple ziliongoza bidhaa za kiumma, basi muongo ujao utashuhudia chapa zaidi za Kichina kama TCL, Hisense, na BYD, ambazo uwezo wake wa kipekee wa bidhaa unaboreshwa siku hadi siku kupitia ushindani mkali.
VCG111639724010.jpg
 
Huu ndio ubaya wa China, yaani ukiweka tu bidhaa yako sokoni ni ikawa na soko, nao watacopy, kwao ni fursa.

Innovationz zinafanyika huko Ulaya, America n.k ila baada ya muda China huyo hapo.
 
Back
Top Bottom