Kampuni ya tiGO kutumia Nguvu kubwa kulazimisha Watanzania kuweka salio kwenye namba zao za simu

snipa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
4,437
Reaction score
2,043
Ni jambo la kushangaza kidogo, kwasabu ni jambo ambalo halipo kisheria, hata katika makubaliano wakati unasajili laini laini za Tigo.

Hii Leo nimepokea ujumbe unaonilazimisha kuweka Salio ndani ya siku tatu, ikiwa Leo ni tarehe 2 mwisho tarehe 5.

Na naambiwa laini yangu itafungiwa kupiga simu kwasabu sijaweka Salio muda mrefu, na kawaida Huwa naweka kupitia tigopesa na hata ninavyopokea ujumbe wao namba yangu Ina Salio. Na kawaida muda mwingi namba inakuwa hewani Sasa wanasema watanifungia, na hakuna lolote zaidi ya ubabe wakijinga kwenye soko,

Huwezi kumfungia mtu namba kama account ya benki, kwanini mteja alazimishwe kuweka Salio hata kama ni kweli haweki, Tigo umekuwa mtandao wa hovyo sana.

Ndugu Mteja, namba yako itazuiliwa huduma ya kupiga simu 05/04/2024 kwasababu hujaongeza salio muda mrefu. Ongeza salio mara kwa mara kuiweka laini hewani
 
Ni sawa kukaa na line unatumia minara yao bila wao kupata faida si poa. Ni mitandao yote hata safaricom ya kenya
Mbona unavyosajili hakuna hizo terms.
Kwani ninavyopigiwa simu hawapati faida ?
Na kumbuka namba ya simu sio kama CR/DB
 
kila mfanya kazi pale kwenye hiyo kampuni uloitaja na zile zingine ambazo hujazitaja amepewa target ya activation kwa dormant accounts mathalani hiyo ya kwako na wengine ambao hawajaricharge line zao kwa kipindi fulani kirefu mathalani miezi4, 3 au 3.

meseji kama hizo ni hatua za kampuni kupushi kazi ngumu sana ya wafanyakazi wao kupambana na wateja ambao wengine ni wanishi na wanatukana mbaya sana πŸ’

these companies needs money,na hiyo ni Miongoni mwa namna zao za kugenarate income ili wakuboreshee wew huduma ya mawasiliano πŸ’
 
Kama njaa za kampuni ndio zinaleta haya yote ni hatari sana, kwasabu wanajichukulia maamuzi ambayo hayapo kwenye t&C,

Leo unamfungia mtu kupiga simu kwasabu hajaweka Salio muda mrefu, na namba anaitumia Kila siku, na inaeleweka kuweka Salio sio lazima, kwasabu Kila mtu ana matumizi yake na namba za simu. Na in my case napokea ujumbe ikiwa namba Ina Salio la kawaida.

Na kama ni Moja ya njia za kugenerate income kutumia force sio suluhisho maana hata kama napigiwa wao pia wanaingiza income sio mpaka nipige.

Inakuaje kwa bibi/Babu kijijini uliyemwelekeza kupokea simu tu na hawezi kupiga Wala kusoma meseji yeye aweke Salio la Nini ?
 
Sidhani kama ushasoma terms kasome utaona. Faida ni wewe kuweka salio pia. Mitandao yote karibu iko hivyo. Lazima uweke salio lisilopungua nadhani 1000 ndani ya miezi 6
Terms on customer side ni hizi hapa hakuna unayosema blah blah za kuweka sijui buku ndani ya miezi sita, ndiomana nasema wanatumia Nguvu zakijinga.

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
actually, sio kuifunga paseeei, ingawa ni kweli baada ya muda fulani usipoitumia line yako wanaifunga, lakini pia anaweza pewa mtu mwingine aitumie kwa kusitisha usajili wako na akamilikishwa msajiliwa mwingine πŸ’

lakini pia sio force, ni mbinu ya kuchochea uricharge dormant line yako. Na kuna kipindi huzizima kweli kwa muda ili tu uwatafute, na ukiwapata watakachokushauri ni kununua vocha waweza kuapdate line yako kwa system zao otherwise unaweza pata tena changamoto ya kutokua hewani πŸ’
 
actually,
sio kuifunga paseeei, ingawa ni kweli baada ya muda fulani usipoitumia line yako wanaifunga, lakini pia anaweza pewa mtu mwingine aitumie kwa kusitisha usajili wako na akamilikishwa msajiliwa mwingine πŸ’
Usipoitumia laini kwa muda flani ni kweli wanaweza kuifungia, na mara nyingi ni kama endapo huiweki kabisa hewana ikawa dormant for more than 3 months+

Hii hata kisheria ni sahihi kwasabu wameweka kwenye terma zao hapa nanukuu πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

The CUSTOMER shall not be entitled or have a right to any specific mobile phone number(s) and MIC reserves the right with justifiable reasons to offer, withdraw and change such mobile phone number(s) as may be allocated upon giving adequate notice to the CUSTOMER.

na hapa

That the CUSTOMER shall at all times be responsible and accountable to MIC for the proper use and preservation of the SIM card and the PIN code. In the event the CUSTOMER continuously neglects to use the SIM card or the number provided for a period of 90 days MIC may suspend the number and re-allocate the number for use by any other CUSTOMER.






Hii Sasa ndio haipo kisheria, na ni janja janja za kijinga, na uhuni.
 
Tigo niliacha kutumia kwa sababu zifuatazo

1. Network yao ni shida sana hasa upande wa internet

2. mara nyingi kuna changamoto kwenye meseji mtu anaweza kuambia nimekutumia meseji hujaona, kumbe meseji yenyewe haujapata unaingia kwenye lawama

Tangu nimehamia Airtel mambo ni mswano. Laini ya tigo ninayo na walishanitumia meseji ya kufungiwa hata wakifunga sina presha Airtel yupo
 
Si uweke tu mkuu ujiunge hata kifurushi cha Jumbe we kila siku unataka upigiwe tu.
Em nikuulize kama hiyo line unaitumia mtu akikutumia ujumbe unamjibu na nini?

Nampigia au kumtext kwenye mtandao mwingine.
 
Sasa we tumia huo mtandao mwingine hiyo line ya tigo waachie wampe mtu ambae atanufaisha mtandao mana huna matumizi nayo..
Mbona matumizi ni mengi mkuu mbali na kuweka vocha. Na naitumia mara nyingi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…