Kama ni hivyo madikteta ni wengi sokoni na stendi za mabasi maana wizi ni mwingi tena wa nguvu. Kwani hapa JF hujaweza kuongeza ufahamu wako kutokana na mijadala yetu? Maana haya unayoandika, dah! ni Elimu ya uraia kule Shule za msingi.
Ndio matokeo ya watu kutenda bila ya kufikiria. Tundu Lissu alisema haya lakini watu toka mtaa wa Lumumba wakamkejeli vilivyo. Ndio maana Mchungaji Peter Msigwa aliwaambia kuwa ccm wanachukua muda mrefu sana kuelewa vitu wanavyoambiwa kwa muda huo.
Asipobadilisha hizo sheria na akakaidi hukumu za arbitrators tusubiri vikwazo vya uchumi.
LIsu alisema wapi? Mbona Lisu anageuzwa ndo kichwa cha taifa. Hadithi ya Lisu ilikuwa Makinikia. Tulishitakiwa kama alivyosema na kutisha utadhani ndo aligundua sheria?
Swali ni je, wapinzani wakichukua uongozi wa nchi, watazifuta hizo sheria zinazolalamikiwa na hao wawekezaji? Watakuwa na ujasiri wa kuwaeleza wananchi juu ya hilo?
Jee Umilele wa CCM Kutawala Tanzania Milele, Unatokana na Nini?.
Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu kuiteua CCM na kuipatia hati miliki ya milele kuitawala Tanzania, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM. Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
Kidumu Milele Chama Cha Mapinduzi.
Pascal
Wanabodi, Leo tena naendelea na zile Makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Topic yangu ya leo ni kutuhusu sisi Watanzania, ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tujifunze kuupokea na kuubali ukweli halisi ulipo, ukweli bayana, hata huo ukweli ukiwa mchungu vipi, ukweli ni ukweli tuu, na siku...
Mungi Mkuu ondoa shaka huyu jamaa anaangukia katika kundi la pili. Kuna mambo mawili nina mashaka nayo kwa huyu jamaa, One he is not serious, and second huyu jamaa inawezekana hayuko sawa!
siyo kila kitu kilichotokea kwingineko lazima kitokee Tz. Hamna lolote hapo.. Kama unadhani ruzuku ndiyo inawaweka madarakani kamuulize daniel arap moi na kanu yake
Sometimes nawaza, Rais wetu anasingiziwa au hana ufahamu...alitupa vitabu mara baada ya graduu...
Suala la Madini, kuchimba, kuuza, kupanga.kupandisha na kushusha bei za Madini ni la Mabeberu Duniani kote,tangu miaka dahari.
Familia moja kubwa Duniani, yenye hati miliki inajua kila penye kutoa madini, mfano;
Sangreal international,
La Medis families nk,
Ki kawaida wamegawana umiliki eg: Standard oil international mafuta tu ni wao!
Africa yote hakuna anayenunua wala kutumia madini zaidi ya hii familia ya ki-Beberu. Wakitaka lao ni limekuwa lao.
Familia hii na nyingine za Westerner ndiyo wamebeba serikali za weupe waidhinisha misaada. House of Lords nk, ni hawa mtupu.
Ndiyo huamua nani apigwe nani asipigwe!
Hizo sijui kampuni hii mara hii nk. Ni sub-branch tu! Ya kuwachanganya wanasheria vilaza. Basically wamejipanga! Kitambo!
Mabara tajiri yote Duniani yanaendeshwa na familia hizi tangu enzi za Alexander Mkuu.
Wako tayari kukuyumbisha kiuchumi, kisiasa kma uki-violet mikataba yao! Huuzi wala kununua. Na wana umoja ktk hili!
Yaani Rais hajui.anakurupuka tu kweli? Si mnipe mimi?
Hakimu Mfawidhi,
Mkuu Hakimu Mfawidhi,
Kwanza usiwe na wasiwasi wowote, hivi ni vitisho tuu, hawa jamaa hawawezi kutufanya chochote wala hawawezi kutushitaki popote kwasababu tumeisha badili sheria zetu za uwekezaji kwenye sheria mpya ya madini, kwenye extractive industries tumeweka kipengele hiki View attachment 1324713
Hivyo hawa jamaa kama wana malalamiko yoyote, waende mahakama zetu za kizalendo.
Ila ile siku tulipo badili sheria, kuna watu tuliuliza humu
Wanabodi, Kwanza naunga mkono marekebisho ya sheria hizi kufanyika, kwa sababu yanafanyika kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na maslahi ya Watanzania badala ya maslahi ya wawekezaji, japo siungi mkono miswada hii kuletwa kwa hati ya dharura kwa sababu tayari kuna mikataba mingi iliyopo...
Hiyo sheria imekuja baada ya hao mabwana kuwa tayari wamesain mkataba nasi kwa hiyo hivyo vifungu ni irrelevant hapo na usifikiri kuwa hao wawekezaji hawalijui hilo.
Huwezi ukabadili sheria za mchezo katikati ya mechi baada ya kuona unaelemewa, hilo halipo.
Vifungu hivyo vitahusu wale wawekezaji watakaotaka kuja kuwekeza baada ya hiyo sheria kuwa effective kinyume cha hapo ni serikali kuwa liable kuvunja mkataba ambalo ni kosa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.