Mimi nadhani kama nchi tumekwishaingia kichakani, lililopo ni kutafuta njia ya kutoka huko.
Tusipoweka tahadhari na kuelewa haya yanayoendelea, tutajikuta ndio tunaingia kwenye msitu wenyewe na sio kichaka tena.
Maana yangu hapa ni hii; hizi kesi zinazoibuka sasa hivi ndizo zinazoweza kuvuruga hata uongozi tutakaotaka tuwe nao baada ya uchaguzi mkuu ujao kwa pande zote mbili, kwa ubaya au kwa uzuri.
Ni rahisi sana kwa Magufuli kuzitumia kesi hizi na kuwahadaa wananchi aendelee kubaki madarakani, kwa huruma za wananchi, au kwa ujinga wao wa kutoelewa mambo yalivyo.
Sijui kama upinzani wanao uwezo wa kuzitumia kesi hizi kuonyesha ubovu alioufanya Magufuli, na wananchi hao wakawa na upeo wa kuelewa wanayoelezwa na kumwadhibu aliyevuruga mambo.
Swali ni je, wapinzani wakichukua uongozi wa nchi, watazifuta hizo sheria zinazolalamikiwa na hao wawekezaji? Watakuwa na ujasiri wa kuwaeleza wananchi juu ya hilo?
Pendekezo ambalo naweza kulitoa kuhusu kesi hizi - ili tusiendelee kuzongwazongwa na hawa wawekezaji, tukubali kwenda kwenye usuluhishi, na huko ndiko tutafute njia za kuwabana hawa.
Mengi ya makampuni haya hayajagundua chochote. Hayachimbi madini sehemu yoyote hapa nchini. Mikataba hii ina masharti yake na ukomo wake. Tuyaangalie masharti hayo na tujikite huko katika kuwabana wasituletee rabsha na kutupa sifa mbaya kama taifa zima.